

**************************
Na Silvia Mchuruza,
Bukoba,Kagera.
Kampuni ya Tembo Nickel Corporation (Tembo Nickel) imekutana na Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Meja Jenerali Charles Mbuge Kwa ajili ya kujitambulisha rasmi Ili kuanza UCHIMBAJI WA MADINI katika halmashauri ya wilaya ya ngara.
Akizungumza na uongonzi wa mkoa wa kagera pamoja na waandishi wa habari Meneja mkazi hapa nchini wa Tembo Nickel, Benedict Busunzu katika Mkutano uliofanyika mjini Bukoba katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa amesema kuwa atahakikisha uchimbaji huo unaenda vizuri bila kuwabughudhi wananchi.
Hata hivyo, amesema kuwa baada ya kukabidhiwa Leseni Maalum ya uchimbaji wa Madini kampuni hiyo itaanza rasmi kuwashirikisha wanajamii wanaoishi katika vijiji vinavyozunguka eneo la mradi ili kuanza kazi Rasmi.
“Tunategemea mwaka ujao shunghuli Kuu zitahusisha marejeo ya upembuzi yakinifu wa uchimbaji Madini kabla ya kuanza shunghuli nzima za ujenzi ambapo, shughuli tunazozitegemea kuanza mara moja zitahusisha mpango mdogo wa uchorongaji na kukamilisha utafiti kwaajiri ya mtambo wa uchenjuaji, ikiwa nipamoja na kushirikisha jamii katika mpango wa makazi mapya kupisha eneo la mradi.
“Katika kipindi cha ujenzi takribani ajira 1,000 kupitia wakandarasi wetu zitahitajika na kipaumbele cha ajira na mafunzo itakuwa kwa Wakazi wa Mkoa huu,” amesema Meneja Busunzu
Aidha, serikali itanufaika na kodi na katika uzarishaji wa Madini itapata asilimia 16 na Tembo Nickel itapata asilimia 84 katika mapato yatakayopatikana Serikali itapata asilimia 50 na Kampuni ya Tembo Nickel itapata asalimia 50.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Meja Jenerali Charles Mbuge amesema kuwa wananchi wa Wilaya ya Ngara watapata mapato na kupata ajira kupitia uchimbaji wa madini hayo.
“Wananchi wa Ngara watapata Fursa ya kufanya shunghuli Mbalimbali za kujiongezea kipato na Serikali inategemea kupata mapato mengi kupitia ushuru wa huduma,” amesema Mbuge.