Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe.Kafulila akitoa maelekezo kuhusu AMCOS wakati wa kikao cha Baraza -Halmashauri ya Wilaya ya Maswa.
Kuanzia kulia Mkuu wa Wilaya Halmashauri ya Wilaya ya Maswa Mhe. Aswege Kaminyoge, Mkuu wa mkoa wa Simiyu Mhe. David Kafulila, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Simiyu Bi. Shamsa Mohamed na mwenyekiti wa Baraza Maswa Bw. Paul Saimon wakisikiliza maelekezo wa mkuu wa mkoa.
Viongozi kutoka ofisi ya mkuu wa Mkoa na Wilaya ya Maswa wakifuatilia kikao
Waheshimiwa madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa wakifuatilia maelekezo ya Mkuu wa mkoa.
…………………………….
Mkuu wa Mkoa Simiyu leo amelekeza Kamanda wa PCCB mkoa kukagua malipo yote ya AMCOS kubaini AMCOS zote zilizoshirikiana na Maofisa ushirika kukiuka taratibu za malipo ya fedha, wenyeviti na makatibu wake kuwajibishwa sambamba na maofisa ushirika watakaobainika kushiriki mchezo mchafu huo.Maelekezo hayo aliyatia wakati wa hotuba yake aliyoitoa wakati wa kikao cha baraza la madiwani wilayani Maswa.
Aidha Kafulila amewataka wakulima wote wa Pamba kujiunga na ushirika kwa kuwahakikisha kuwa ataondoa virusi wote kuanzia maofisa ushirika halmashauri mpaka viongozi wa AMCOS.
Lengo ni kuhakikisha kuwa , lengo la Serikali la kuhakikisha ushirika unamkomboa mkulima mdogo linafikiwa kama ilivyokuwa miongo kadhaa baada ya