KOCHA mpya wa Simba SC, Mspaniola Pablo Franco Martin akizungumza na kiungo Ibrahim Ajibu alipowatembelea wachezaji Gym kambini kwao, Mbweni nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam leo.
Hapa anazungumza na Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo, Barbara Gonzalez
Hapa anazungumza na Kocha Msaidizi, Suleiman Matola. Katikati ni aliyekuwa Kaimu Kocha Mkuu, Mnyarwanda, Thierry Hitimana.
Pablo amewasili leo asubuhi na kupokewa na Mratibu wa timu, Abbas Suleiman tayari kuanza kuutumikia mkataba wake wa miaka miwili akirithi mikoba ya Mfaransa, Didier Gomes Da Rosa aliyefukuzwa mwezi uliopita.