West Ham United wameibuka na ushindi wa 3-2 dhidi ya Liverpool katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa London.
Mabao ya West Ham la kwanza alijifunga kipa Alisson Becker dakika ya nne, la pili Pablo Fornals dakika ya 67 na Kurt Zouma dakika ya 74, wakati ya Liverpool yamefungwa na Trent Alexander-Arnold dakika ya 41 na Divock Origi dakika ya 83.
West Ham inafikisha pointi 23 na kupanda nafasi ya tatu ikiizidi pointi moja Liverpool na ikizidiwa wastani wa mabao tu na Manchester City na wote wakiwa nyuma ya Chelsea inayoongoza kwa pointi tatu zaidi baada ya wote kucheza mechi 11.