…………………………………………………………….
Na Silvia Mchuruza,Bukoba
Ni katika maafari ya 15 ya taasisi za elimu za kaizirege na kemibosi wazazi wameaswa kuwa makini na malezi ya watoto wao kuliko kujali kazi zao zaidi.
Kauli hiyo imetolewa na ostaz Mikidadi Salumu Mbaruku ambae ni mwalimu wa somo la dini la kiislamu katika maafari ya shule hizo za kaizirege na kemibosi.
Akizungumza na wazazi wa wahitimu hao wa kidat Cha nne na darasa la Saba amesema kuwa wazazi walio wengi wamejisahau kwa watoto katika maadili na kujali kazi zao zaidi jambo linalooelekea maadili kwa watoto wao kushuka.
“Niseme tu ukweli Kuna wakati unakuta watoto wanalelewa na Tv pamoja na jamii kuliko wazazi wao wenyewe na pia mda mwingine wazazi wamekuwa wakijisahau kuwafundisha watoto katika maadili ya kidini mtoto unakuta anajua season kuliko mambo ya dini tubadike” alisema ostaz Mbaruku.
Aidha nae meneja wa shule bwana Eurojius Katiti ametoa shukrani zake za dhati kwa uongizi wa shule kwa kuendelea kuboreshwa kwa miundombinu pamoja walimu wenye weredi wa kutosha.
Pia amesema kuwa ujenzi wa chuo kaika taasisi za kemibosi na kaizirege ni mpango ambapo upo unaenddlea kufanyiwa kazi Ili kiweza kuwapa wanafinzi wao elimu iliyo Bora.
” Jambo lengine tunazidi kuwashukuru wadau wetu mbalimbali ikiwemo serikali yetu ya awamu ya aita bila kusahau ofisin ya mkuu wa mkoa wetu wa Kagera, ofisin ya afisa elimi mkoa pamoja na NMB bank,CRDB bank na wengine wengi kwa kisababisha taasisi hizi kuendelea kuwepo”
Hata hivyo nao wahitimu wa darasa la katika risala yao iliyo somwa na moja wa wahitimu Noela Charles amesema wamemamaliza jumla ya wanafunzi 84 wavulan wikiwa 44 na wasichana 40 Kwa ufauru mzuri kwa kuwa 1 kimkoa na wapili kitaifa.
Kwa upande wao wahitimu wa kidato Cha nne ambao wanatarajia kuanza mtihani wao wa kumaliza utakaoanza tarehe 15 mwezi wa 11 mwaka huu kupitia risala yao iliyosomwa na mmoja wa wahitimu hao Ereni Eurojius Katiti wamemshukuru mkurugenzi wa shule Ndg.Yusto Kaizirege Ntagalinda na mama kaizirege Bi.Erizabert Kaizirege kwa kuendelea kuimalisha miundombinu kwa kuwajengea kitu Cha afya Cha kisasa kinachoweza kuwalaza wanafunzi 10 na kuwaudumia zaidi ya wanafunzi 100 bila kusahau daktari mwenye weredi pamoja na wauguzi.
“Tunakushukuru mkurugenzi na mama mkurugenzi mmekuwa wazazi wetu kwa mda tuliokaa hapa tumepata huduma nzuri changamoto azikosi lakini tumezivumili na nyie mmetuvumilia kwa mapungufu yetu tunashukuri” alisema Ereni.