Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt, Batilda Buriani akitoa salamu za Serikali leo wakati aliposhiriki ibada ya kumbukumbu ya miaka mitano ya marehemu Spika Mstaafu Mhe. Samwel Sitta ilifanyika katika Kanisa la Moravian mjini Urambo.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt, Batilda Buriani akitoka Kanisani leo baada ya kushiriki ibada ya kumbukumbu ya miaka mitano ya marehemu Spika Mstaafu Mhe. Samwel Sitta ilifanyika katika Kanisa la Moravian mjini Urambo.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt, Batilda Buriani (wa pili kutoka kushoto) akiwa katika pichha ya Pamoja na Askofu wa Kanisa la Moravian Jimbo la Tanganyika Charles Katale (wa tatu kutoka kushoto)mara baada ya kumalizika kwa ibada ya kumbukumbu ya miaka mitano ya marehemu Spika Mstaafu Mhe. Samwel Sitta ilifanyika katika Kanisa la Moravian mjini Urambo.
Picha na Tiganya Vincent
………………………………………………..
NA TIGANYA VINCENT
MKUU wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda amesema Serikali imekusudia ifikapo mwaka 2025 wakazi wengi wa mjini Wilayani Urambo wanapata maji safi na salama.
Amesema kupitia mpango wa kutoa maji toka Ziwa Victoria Serikali itahakikisha wakazi wanaoishi mjini wanapata maji safi na salama kwa asilimia 95 na wanaoishi vijijini kwa asilimia 85.
Balozi Dkt, Batilda Buriani amesema hayo leo wakati akitoa salamu za Serikali kwenye ibada ya kumbukumbu ya miaka mitano ya marehemu Spika Mstaafu Mhe. Samwel Sitta ilifanyika katika Kanisa la Moravian mjini Urambo.
Amesema Serikali ya Awamu ya Sita inaongoza na Mhe. Samia Suluhu Hassan imekusudia imekusudia kupeleka maendeleo na kuwasogezea huduma muhimu karibu na wananchi.
Balozi Dkt, Batilda amesema Serikali kupitia Mpango wa Maendeleo na Ustawi wa Tiafa na Mapambano dhidi ya UVIKO 19 imetoa fedha nyingi kwa Mkoa wa Tabora kwa ajili ya maendeleo ya wananchi kupitia huduma mbalimbali ikiwemo elimu , afya , miundombinu na upatikanaji wa maji safi na salama.
Amesema kupitia mpango huo Serikali imetoa zaidi ya shilingi bilioni 21.7 kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya madarasa katika Shule za Sekondari na Msingi na sekta ya afya na bilioni 33 ya ujenzi wa miundombinnu yam aji kwa ajili kufikisha kwa wananchi.
Balozi Dkt, Batilda amesema kupitia fedha hizo Serikali itapeleka maji kutoka Ziwa Victoria kwa wakazi wa Urambo na Kaliua.
Mkuu huyo wa Mkoa wa Tabora amewashukuru Madaktari Bingwa ambao wamekwenda Wilayani Urambo kwa ajili ya kutoa huduma mbalimbali za kujitolea.