Mkuu wa mkoa wa Arusha ,John Mongela akizungumza na vyombo vya habari Leo jijini Arusha kuhusiana na maadhimisho hayo yatakayofanyika kitaifa mkoani Arusha,pembeni yake ni Katibu Tawala wa mkoa wa Arusha,Athuman Kihamia (Happy Lazaro) Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakimsikiliza mkuu wa mkoa jijini Arusha.(Happy Lazaro) Meneja mpango wa Taifa wa kuzuia na kudhibiti magonjwa yasiyoambukiza kutoka wizara ya Afya ,Daktari Omary Ubuguyu akizungumza katika semina ya kuwajengea uwezo wanahabari kuhusu magonjwa yasiyoambukiza .(Happy Lazaro) *****************************
Happy Lazaro, Arusha
Arusha.WAZIRI wa Michezo na Utamaduni Innocent Bashungwa,kesho anatarajiwa kuzindua rasmi maadhimisho ya kitaifa ya magonjwa yasiyoambukiza yatakayofanyika kwenye Uwanja wa mpira wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha .Mkuu wa mkoa wa Arusha, John Mongela, ameviambia vyombo vya habari kuwa maandalizi ya maadhimisho hayo yamekamilika na kwamba kulingana na takwimu za mwaka 2016,za shirika la afya Ulimwenguni, WHO, watu milioni 57 sawa na asilimia 71% walikufa kutokana na magonjwa yasiyoambukiza.
Aidha watu milioni 4.7 sawa na asilimia 33% nchini waliokuwa na magonjwa yasiyoambukiza na waliweza kupata huduma ya magonjwa hayo.
Mongela amesema Rais Samia Suluhu Hassan,wakati akiwa Makamu wa Rais alikuwa akiongoza juhudi za kupambana na magonjwa yasiyoambukiza na. tangia amekuwa Rais na ameendelea na. jitihada hizo ambazo zimewezesha kujengwa ,ICU, Ex -Ray ,CT-scan lengo kuokoa maisha ya watu.
Amesema kuwa ,miongoni mwa mawaziri wengine watakaoshiriki kwenye maadhimisho hayo ambayo kilele chake kitakuwa ni Novemba 13 ni pamoja na Waziri wa Elimu, Profesa Joyce Ndalichako, na Waziri wa Tamisemi,Ummy Mwalimu hukun mgeni rasmi kwenye kilele hicho akiwa ni Waziri wa afya Daktari Doroth Gwajima.
Mongela,amesema ajenda ya maadhimisho hayo ni pamoja na kufanya mazoezi huku akatumia fursa hiyo kuwaasa wananchi kuwa makini kwenye lishe na kula vya kula visivyokuwa na mafuta mengi,chumvi nyingi ,na kuhamasisha ufanyaji wa mazoezi.
Naye Meneja mpango wa Taifa wa kuzuia na kudhibiti magonjwa yasiyoambukizwa kutoka wizara ya Afya, Daftari Omary Ubuguyu amesema kuwa, ongezeko la magonjwa yasiyoambikiza yanachangia asilimia 71% Vifo vya watu nchini hivyo yanatakiwa kupewa kipaumbele katika kuyatibu na kuyatokomeza .
Ubuguyu ameyasema hayo katika.semina ya wanahabari ikiwa na lengo la kuwajengea uelewa kuhusu magonjwa hayo yasiyoambukiza nchini katika kuelekea maadhimisho hayo ambayo yatafanyika kitaifa mkoani Arusha.
Amesema kuwa, bara la afrika linachangia Vifo vinavyotokana na magonjwa yasiyoambukiza kwa asilimia 20 % huku nchi zilizoendelea za Itali na Japani zinachangia asilimia 10% tu ya magonjwa hayo yasiyoambikiza na waathirika ni wazee wenye umri wa miaka 70.
Naye Katibu tawala wa Mkoa wa Arusha,Athumani Kihamia,amesema kuwa ,mfumo wa maisha unachangia watu kupata magonjwa hayo yasiyoambukiza ambayo yanachangiwa na kutokufanya mazoezi.Amesema kuwa,semina hiyo itatoa mwanga kwa wanahabari kuelewa kwa kina magonjwa hayo yasiyoambukiza athari zake na namna yanavyoweza kuzuilliwa hivyo akasisitiza mpangilio wa vyakula na ufanyaji wa mazoezi.
Akitoa mada katika semina hiyo Daktari bingwa wa magonjwa ya Figo,mkoani Arusha Daktari Rose Mende,amesema magonjwa yasiyoambukiza hayana vimelea vya maambukizi vinavyoweza kusababisha akil