Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema (kulia) akimkabidhi Mwenyekiti wa PJFCS, Sadick Kibira fedha ya chakula kwa ajili ya Wana Michezo wa Klabu ya Mazoezi maarufu Polisi Jamii Fitness Center Shinyanga (PJFCS) inayokwenda kushiriki katika Mashindano ya Mbio za NBC Marathon yatakayofanyika Novemba 7,2021 Jijini Dodoma
Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP George Kyando wameagana na Wana Michezo wa Klabu ya Mazoezi maarufu Polisi Jamii Fitness Center Shinyanga (PJFCS) inayolelewa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga ambayo inakwenda Jijini Dodoma kushiriki katika Mbio za NBC Marathon zenye lengo la kusaidia akina mama wenye saratani ya shingo ya kizazi yanayotarajiwa kufanyika Novemba 7,2021.
Wanamichezo hao wa Klabu ya Mazoezi maarufu Polisi Jamii Fitness Center Shinyanga (PJFCS) wamefika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga leo Ijumaa Novemba 5,2021 kwa ajili ya kupata baraka za viongozi hao tayari kuanza safari yao kuelekea Dodoma kesho kwa ajili ya kushiriki mashindano hayo.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema amewashukuru Wana Michezo hao kwa kufika ofisini kwake na kumuaga ambapo amewapongeza kuona wana ari ya kuonesha kwamba Shinyanga inaingia kwenye ramani ya Tanzania kuwa Shinyanga ipo vizuri kwenye michezo.
“Nendeni Dodoma mkatuwakilishe kama Wana Shinyanga Mashindano ya Mbio za Marathon Dodoma, Mimi najua Wana Shinyanga mna nidhamu sana kwa hiyo mkienda kule na kwa kuwa mnalelewa na Jeshi la Polisi mna nidhamu ya hali ya juu, nendeni mkaoneshe nidhamu iliyotukuka, Nendeni mkaitangaze Shinyanga kwa mambo mazuri yanayopatikana ikiwemo kilimo, ufugaji na madini”,amesema Mjema.
“Nawatakieni kila la heri huko mnakokwenda,nendeni na Baraka zetu, Mimi kama Mama nawatakia watoto wangu kila lililo jema,lakini muendelee kuchukua tahadhari dhidi ya UVIKO 19 na maradhi mengine”,amesema Mjema.
“Tunataka Shinyanga yote tuiamshe amshe kimichezo, hivyo tutakuwa tunapanga Events kuzunguka kwenye kila halmashauri na sisi tunawategemeeni nyinyi kwa sababu mnajua zaidi kuhusu michezo, sisi kazi yetu ni kuwezesha, Shinyanga tuna vipaji vingi”,ameongeza.
Aidha amewakabidhi shilingi 500,000/= kwa ajili ya chai na kwamba Serikali ya mkoa wa Shinyanga itatengeneza utaratibu mzuri kwa ajili ya Timu zinazowakilisha mkoa wa Shinyanga.
Kwa upande wake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP George Kyando amewaomba Wana michezo hao kwenda kuuwakilisha vyema mkoa wa Shinyanga na kuhakikisha wanarudi na medali pamoja kuitangaza Polisi Jamii Shinyanga.
Makamu Mwenyekiti wa PJFCS, Lucas Moris amewashukuru viongozi wa mkoa wa Shinyanga kwa kutambua kile wanachokwenda kufanya mkoani Dodoma na kuahidi kuwa watakwenda kushiriki kikamilifu ili kuuletea heshima mkoa wa Shinyanga.
“Tumekuja kupata Baraka za Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema na Mlezi wa PJFCS ambaye ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP George Kyando kwenda kuwakilisha mkoa katika mashindano ya NBC Marathon yanayotarajiwa kufanyika Jijini Dodoma Siku ya Jumapili Novemba 7,2021”,ameeleza.
“Tunaondoka Shinyanga kwenda Dodoma tukiwa na timu ya wana mazoezi 25 kati yao wanawake wapo 9 wanaume 16 ambao wote wamejisajili na wanaenda kushiriki katika Mbio hizo za NBC Marathon zenye lengo la kuchangia akina mama wanaosumbuliwa na Saratani ya shingo ya kizazi. Mbio hizi zipo tofauti zipo zenye kilomita 42,21,10 na kilomita 5”,ameongeza Moris.
Amemshukuru Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga kwa ushirikiano na msaada waliowapatia akisema wameonesha wana upendo mkubwa kwa kikundi hicho cha michezo na kwa mkoa.
“Hakika viongozi wetu wa mkoa wametupa motisha ya kwenda kupambana katika mbio za marathon, tumejipanga kikamilifu na sisi tunaamini tunaenda kurudi na ushindi, sasa tunaendelea kujifua zaidi na morali yetu inaongezeka zaidi kwenda kushiriki mashindano hayo”,amesema Moris.
Aidha amemshukuru Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema kwa kuwapatia shilingi 500,000/= kwa ajili ya chakula na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP George Kyando kwa kuwapatia shilingi 200,000/= kwa ajili ya maji pamoja na usafiri kwenda Dodoma kupitia ofisi ya Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Shinyanga.
ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema akizungumza wakati akiagana na Wana Michezo wa Klabu ya Mazoezi maarufu Polisi Jamii Fitness Center Shinyanga (PJFCS) inayokwenda kushiriki katika Mashindano ya Mbio za NBC Marathon yatakayofanyika Novemba 7,2021 Jijini Dodoma. Picha na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema akizungumza wakati akiagana na Wana Michezo wa Klabu ya Mazoezi maarufu Polisi Jamii Fitness Center Shinyanga (PJFCS) inayokwenda kushiriki katika Mashindano ya Mbio za NBC Marathon yatakayofanyika Novemba 7,2021 Jijini Dodoma
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema akizungumza wakati akiagana na Wana Michezo wa Klabu ya Mazoezi maarufu Polisi Jamii Fitness Center Shinyanga (PJFCS) inayokwenda kushiriki katika Mashindano ya Mbio za NBC Marathon yatakayofanyika Novemba 7,2021 Jijini Dodoma
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema (kulia) akimkabidhi Mwenyekiti wa PJFCS, Sadick Kibira fedha ya chakula kwa ajili ya Wana Michezo wa Klabu ya Mazoezi maarufu Polisi Jamii Fitness Center Shinyanga (PJFCS) inayokwenda kushiriki katika Mashindano ya Mbio za NBC Marathon yatakayofanyika Novemba 7,2021 Jijini Dodoma
Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga, Zuwena Omary akizungumza wakati Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema akiagana na Wana Michezo wa Klabu ya Mazoezi maarufu Polisi Jamii Fitness Center Shinyanga (PJFCS) inayokwenda kushiriki katika Mashindano ya Mbio za NBC Marathon yatakayofanyika Novemba 7,2021 Jijini Dodoma

Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga, Zuwena Omary (kushoto) na Wana Michezo wa Klabu ya Mazoezi maarufu Polisi Jamii Fitness Center Shinyanga (PJFCS) wakiwa katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.
Kiongozi wa Kiimani wa PJFCS, Ignas Banyemaa akiomba wakati Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema akiagana na Wana Michezo wa Klabu ya Mazoezi maarufu Polisi Jamii Fitness Center Shinyanga (PJFCS) inayokwenda kushiriki katika Mashindano ya Mbio za NBC Marathon
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema (wa tano kulia) na Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Zuwena Omary (aliyevaa miwani) wakipiga ya pamoja na sehemu ya Wana Michezo wa Klabu ya Mazoezi maarufu Polisi Jamii Fitness Center Shinyanga (PJFCS) inayokwenda kushiriki katika Mashindano ya Mbio za NBC Marathon yatakayofanyika Novemba 7,2021 Jijini Dodoma

Makamu Mwenyekiti wa PJFCS, Lucas Moris (katikati) akielezea kuhusu Ushiriki wa PJFCS kwenye mashindano ya Mbio za NBC Marathon. Kulia ni Mwenyekiti wa PJFCS, Idrisa Kibira, kushoto ni Kiongozi wa Kiimani wa PJFCS, Ignas Banyemaa.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP George Kyando akizungumza wakati akiagana na Wana Michezo wa Klabu ya Mazoezi maarufu Polisi Jamii Fitness Center Shinyanga (PJFCS) inayokwenda kushiriki katika Mashindano ya Mbio za NBC Marathon yatakayofanyika Novemba 7,2021 Jijini Dodoma

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP George Kyando akipiga ya pamoja na sehemu ya Wana Michezo wa Klabu ya Mazoezi maarufu Polisi Jamii Fitness Center Shinyanga (PJFCS) inayokwenda kushiriki katika Mashindano ya Mbio za NBC Marathon yatakayofanyika Novemba 7,2021 Jijini Dodoma
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP George Kyando akipiga ya pamoja na sehemu ya Wana Michezo wa Klabu ya Mazoezi maarufu Polisi Jamii Fitness Center Shinyanga (PJFCS) inayokwenda kushiriki katika Mashindano ya Mbio za NBC Marathon yatakayofanyika Novemba 7,2021 Jijini Dodoma.
Picha zote na Kadama Malunde – Malunde 1 blog