Daktari Bigwa wa Maradhi ya Kinamama na Uzazi kutoka China Xiaoqing Yang, akitoa maelezo kwa Madaktari na Manesi (hawapo pichani) kwa njia ya Mtandao, katika Mkutano wa Kitaalamu wa Kisayansi wa kujadili maradhi mbali mbali ya kina Mama, hafla iliyofanyika Hospitali ya Mnazi Mmoja Mjini Zanzibar.
Mkurugenzi Mkuu Wizara ya Afya Ustawi wa Jamii,Wazee, Jinsia na Watoto Dk.Abdullah Ali Suleiman, akifunguwa Mkutano wa Kitaalamu wa Kisayansi wa kujadili maradhi mbali mbali ya kina Mama, kwa njia ya Mtandao,uliyowashirikisha Madaktari na Manesi, hafla iliyofanyika Hospitali ya Mnazi Mmoja Mjini Zanzibar.
Mkurugenzi Mtendaji Hospitali ya Mnazi Mmoja Dk.Msafiri Marijani,akizungumza na Madaktari na Manesi (hawapo pichani) kwa njia ya Mtandao, katika Mkutano wa Kitaalamu wa Kisayansi wa kujadili maradhi mbali mbali ya kina Mama, hafla iliyofanyika Hospitali ya Mnazi Mmoja Mjini Zanzibar.
Baadhi ya Madaktari na Manesi waliyohudhuria katika Mkutano wa Kitaalamu wa Kisayansi wa kujadili maradhi mbali mbali ya kina Mama, hafla iliyofanyika Hospitali ya Mnazi Mmoja Mjini Zanzibar.
Picha Na Maryam Kidiko / Maelezo Zanzibar.
……………………………………………………………..
Na Kijakazi Abdalla ,Maelezo
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imesema inajivunia kuwepo kwa madaktari wa kichina katika kusaidia matibabu ya magonjwa mbalimbali.
Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mkuu Wizara ya Afya Ustawi wa Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto Dkt Abdallah Ali Suleiman kwa niaba ya Waziri wa Afya Mhe. Nassor Ahmed Mazrui huko Hospitali ya Mnazi Mmoja wakati akifungua Mkutano wa kibingwa unaohusu magonjwa ya uzazi na kinamama.
Amesema uwepo wa Madaktari wa Kichina Zanzibar kumesaidia matibabu mbalimbali ambapo hapo zamani imebidi kusafirisha wagonjwa kwenda nchi za jirani kutibiwa.
Aidha amesema Madaktari hao wa kichina kumewezesha kuwasaidia kujenga uwezo mzuri kwa Madaktari wazalendo kufundisha mbinu za njia halisi za kisasa zenye mafanikio makubwa ya matibabu.
Dkt Abdallah amesema kwa upande wa kina mama Hospitali ya Mnazi Mmoja imeweza kufanya Upasuaji mkubwa kunusuru maisha kwa wagonjwa walokua hatua za kwanza za saratani ya kizazi kwa kufanyiwa upasuaji ili kusaidia kurefusha maisha.
Nae Daktari Bigwa wa Maradhi ya kinamama na Uzazi kutoka China Xiaoqing Yang amesema lengo la Mkutano huo ni kujadiliana na Madaktari wa Hospitali ya Mnazi Mmoja na ya Abdala Mzee maradhi yanayowasumbua akina Mama wa Zanzibar na wakichina.
Aidha amesema Mkutano huo utasaidia sana kufikisha malengo yaliyokusudiwa ili kuondosha kabisa Chngamoto zinazowakabili wakinamama wakati wa kujifungua.
Mkutano huo wa siku moja umeandaliwa na Timu ya 31 ya Madaktari Bigwa wa Kichina wa Maradhi ya Kinamama..