Mbunge wa jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka Akizungumza na wananchi wa kata ya picha ya ndege wakati wa mkutano wa hadhara.
*****************************
NA VICTOR MASANGU,KIBAHA
Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka amemchangia kiasi cha shilingi laki laki tano mwanamke mmoja aliyejulikana kwa jina la Nyangoma James mkazi wa kata ya picha ya ndege baada ya bajaji yake kuibiwa na watu wanaosadikiwa ni majambazi.
Koka amechukua hatua hiyo baada ya kusikia kilio hicho kutoka kwa mwanamke huyo wakati wa mkutano wake wa hadhara na wananchi wa kata ya picha ya ndege kwa ajili ya kusikiliza kero na changamoto zinazowakabili.
Katika mkutano huo Mbunge baada ya kusikia kilio hicho alisikitishwa na tukio Hilo la wizi wa kuiba bajaji kwa mwanamke huyo ambaye ni mlemavu wa miguu na kwamba amekea vikali tabia hiyo.
“Kwa kweli nimesikitishwa Sana na tukio hili ya huyu dada maana alikuwa na bajaji yake alafu watu ambao sio waaminifu bila hata huruma wamekwenda kumwimbia hii sio tabia nzuri hata kidogo na mm ninachangia laki tano kwa kuanzia,”alisema Koka.
Aidha Koka alisema kwamba ataendelea kushirikiana bega kwa bega na dada huyo mlemavu kwa kushirikiana na jeshi la polisi ili wale wote ambao wamehusika waweze kusakwa na kukamatwa ili sheria iweze kuchukua mkondo wake.
Pia katika hatua nyingine Mbunge huyo aliweza kutekeleza ahadi yake kwa kikundi Cha boda boda Cha picha ya ndege kwa kuwezesha kiasi Cha shilingi laki tano ili kiweze kujiendeleza zaidi.
Nao baadhi ya viongozi wa kikundi hicho Cha boda boda wamempongeza Mbunge kwa kuweza kuwachangia fedha hiyo ambayo itawasaidia kwa kiasi kikubwa katika kuongeza mtaji wao.
Awali mwanamke huyo Nyangoma James ambaye anaishi kata ya picha ya ndege alibainisha kuwa bajaji hiyo alipatiwa. na hayati Rais Dk.John Pombe Magufuli mnamo.mwaka 2020 na kwamba imeibiwa mwaka huu na watu wasiojulikana.
Katika ziara ya Mbunge wa Jimbo la Kibaha ambayo ameifanya kwa wananchi wa kata ya Picha ya ndege ameweza kukagua miradi mbali mbali ya maendeleo ikiwemo sekta ya elimu.