MKURUGENZI wa Taasisi ya
Ebenezer English Medium Primary School za Jijini Tanga Issack Mlangwa akizungumza na waandishi wa habari
………………………………………………………..
NA OSCAR ASSENGA, TANGA.
MKURUGENZI wa Taasisi ya
Ebenezer English Medium Primary School za Jijini Tanga Issack Mlangwa amempongeza
Rais Samia Suluhu kwa kuboresha sekta ya elimu hapa nchini ikiwemo kutoa ajira
kwa walimu kutokana na mahitaji yaliyopo tokea aingie madarakani
Pongezi hiyo alilizitoa
wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu matokeo ya darasa la saba
yaliyotoka hivi karibuni ambapo shule ya Msingi ya Ebenezer English Medium
Primary School iliweza kuongeza kiwilaya na kimkoa kwa kushikaa nafasi ya
kwanza.
Shule hiyo iliibuka kinara
wa matokeo ya darasa la saba kwa miaka mitano mfululizo kuanzia mwaka 2016 mpaka
mwaka 2021 kiwilaya na mkoa wa Tanga huku walipania kuhakikisha wanaendelea
kufanya vizuri ikiwemo kuibuka na kidedea kwenye ngazi ya Taifa kipindi
kijacho.
Alisema wanasifu juhudi
hizo kutokana na awali kulikuwa na uhaba wa walimu huku akimshauri Rais kutoa nafasi nyingi na kuunga mkono
wawekezaji katika sekta ya elimu kwenye
shule wa watu binafasi ili watoto wa kitanzania waweze kupata elimu bora .
“Kutokana na kwamba Serikali
pekee haiwezi kwa hiyo zinahitajika za juhudi za makusudi ziweze kufanyika ili
wawekezaji wengi waliopo kwenye sekta hiyo ili kuweza kuinua ubora mzuri.
Ambapo alisema kwa sababu
Serikali pekee haiwezi kusimamia elimu hivyo juhudi za makusudi zinahitaji ili kuwasaidia
wawekezaji wengi waliopo kwenye sekta hiyo ili kuweza kuleta ushindani nchini.
Mkurugenzi huyo alisema
juhudi hizo zinatakiwa kufanyika ili kuweza kuvutia wawekezaji wengi ambao
watachangia ushindani na hivyo kusaidia
kukuza ubora wa elimu.
Akizungumzia siri ya
kuongoza kimkoa kila mwaka Mkurugenzi huyo alisema kikubwa ni ushirikiano kati
ya walimu,wanafunzi,wazazi na utawala wa shule hiyo.
Alisema pili ni uongozi wa
shule hiyo unajitahidi kumaliza mitaala mapema ili kuweza kupata muda wa
kufanya marudio mara kwa mara na kufanya mitihani mingi kwa wiki wanafanya
mitihani mitatu kwa kufanya marudi mara kwa mara.
Aidha alisema pia
kuimarisha misingi ya nidhamu kwa walimu na wanafunzi ambao wanahudumiwa huku
akielezea program yao ya masomo ya usiku kwa wale wanaokaa bwenini na wakishapata
chakula chao wanapata masomo ya ziada hatua ambayo imeleta mafanikio chanya kwenye
shule yao.
Alisema pia wanajisikia
fahari kwa mafanikio wanayo pata kila siku lakini sio kubahatisha ni uwezo wa Mwenyezi
Mungu ikiwemo baadhi ya walimu na wanafunzi wanajiwekea malengo na mikakati
wanaojiwekea na walimu wao kwa ajili ya kupata matokeo.
“Mafanikio hayo
yamechangia kutokana na walimu waliona waliobobea kwenye ufundishaji na
wafanyakazi ambao wanatimiza wajibu wapo
na wanaamini mafanikio yao yanakuja na umoja na ushirikiana wao”Alisema
Awali akizungumza
Mwalimu wa Shule ya Msingi Ebenezer Lucy Materu alisema wanajitahidi kuwa
fundisha watoto kwa bidii lakini wanafanya mazoezi ya kutosha ambayo yanawezesha
kufanya marudio vitu ambavyo wamefundishwa na walimu wao darasani hatua
inayosaidia kwenye ufaulu wao.
Naye kwa upande wake
Mwalimu Shamuni Hassani wa shule hiyo alisema matokeo ambayo wameyapata
wanamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuwawezesha kupata matokeo hayo na jambo la
kufurahisi kutokana na maandalizi waliyokuwa wameyafanya.
Akionekana kuunga mkono
hoja hiyo Mkurugenzi wa Shule ya Msingi ya Indian Ocean ya Jijini Tanga Judith
Kimbute alisema jambo ambalo angeliomba Serikali iwafikirie shule binafsi kutokana
na kwamba wana mchango mkubwa kwa serikali kusaidia jamii na wazazi wengine
ambao hali zao zipo chini .
Alisema lakini wakati
mwengine wanapambana nao huku wengine hawalipi ada zao kutokana na hali mbaya
na kila mwaka wana madeni hatua ambayo imekuwa ikiwarudisha nyuma.
Mkurugenzi huyo aliiomba
Serikali iwafikirie kwamba hao wanaoendesha shule binafsi wafanyiwe kitu kidogo
ili waweze kuwasaidia ili nao waendelee na kuona kwamba serikali yao
imewasaidia kwani wamekuwa na mchango mkubwa kwenye kukuza elimu nchini.