Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe. Prof. Makame Mbarawa pamoja na Balozi wa Ubelgiji hapa nchini Balozi, Peter Van Acker wakisaini Mkataba wa makubaliano ya kibiashara ya usafiri wa anga kati ya nchi hizo mbili hafla iliyofanyika leo November 3,2021 jijini Dodoma.
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe. Prof. Makame Mbarawa na Balozi wa Ubelgiji nchini Balozi, Peter Van Acker wakibadilisha Mkataba mara baada ya kusaini makubaliano ya kibiashara ya usafiri wa anga kati ya nchi hizo mbili hafla iliyofanyika leo November 3,2021 jijini Dodoma.
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe. Prof. Makame Mbarawa na Balozi wa Ubelgiji nchini Balozi, Peter Van Acker wakionyesha Mkataba mara baada ya kusaini makubaliano ya kibiashara ya usafiri wa anga kati ya nchi hizo mbili hafla iliyofanyika leo November 3,2021 jijini Dodoma.
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe. Prof. Makame Mbarawa akizungumza mara baada ya kusaini Mkataba wa makubaliano ya kibiashara ya usafiri wa anga kati ya Tanzania na Ubelgiji hafla iliyofanyika leo November 3,2021 jijini Dodoma.
Balozi wa Ubelgiji nchini Balozi, Peter Van Acker akisisitiza umuhimu wa ushirikiano huo wakati wa hafla ya utiaji saini hati ya makubaliano ya kibiashara ya usafiri wa anga kati ya Tanzania na Ubelgiji hafla iliyofanyika leo November 3,2021 jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Hamza Johari,akizungumza wakati wa hafla ya utiaji saini wa hati ya makubaliano ya kibiashara ya usafiri wa anga kati ya Tanzania na Ubelgiji hafla iliyofanyika Leo November 3,2021 jijini Dodoma.
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe. Prof. Makame Mbarawa akipokea zawadi kutoka kwa Balozi wa Ubelgiji nchini Balozi, Peter Van Acker mara baada ya kuingia Mkataba wa makubaliano ya kibiashara ya usafiri wa anga kati ya nchi hizo mbili hafla iliyofanyika leo November 3,2021 jijini Dodoma.
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe. Prof. Makame Mbarawa pamoja na Balozi wa Ubelgiji nchini Balozi, Peter Van Acker wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumaliza kusaini Mkataba wa makubaliano ya kibiashara ya usafiri wa anga kati ya nchi hizo mbili hafla iliyofanyika leo November 3,2021 jijini Dodoma.
……………………………………………………………..
Na.Alex Sonna,Dodoma
Tanzania na Ubelgiji wamesaini Mktaba wa makubaliano ya kibiashara ya usafiri wa Anga huku ukishuhudiwa na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe. Prof. Makame Mbarawa na Balozi wa Ubelgiji nchini Balozi, Peter Van Acker.
Akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika leo November 3,2021 jijini Dodoma Prof. Mbarawa ameyataka mashirika ya ndege kuanza fursa hiyo muhimu ili kuwekeza na kuimarisha fursa za uchumi hususani katika nyanja za utalii na biashara.
Makubaliano hayo yatawezesha huduma ya biashara za ndege kati ya Tanzania na Ubelgiji ambapo sasa ndege za Tanzania zitaweza kwenda moja kwa moja Ubelgiji na ndege za Ubelgiji kuja Tanzania.
“Huu ni mwanzo tu, tumejipanga kuhakikisha sekta ya usafiri wa anga inafunguka na kuwaleta wadau wengi wa maendeleo nchini na sisi kutoka kwenda kuangalia fursa huko ziliko”. amesisitiza Prof. Mbarawa.
Kwa upande wake Balozi wa Ubelgiji hapa nchini Balozi, Peter Van Acker amesema chini ya mpango huo, ndege za Tanzania zitakwenda moja kwa moja Ubelgiji na ndege kutoka Ubelgiji zitakuja moja kwa moja Tanzania zikitua katika Viwanja vya Ndege vya Kimataifa vya Julius Nyerere (JNIA), Kilimanjaro (KIA) na Abeid Amani Karume (AAKIA).
Naye Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Hamza Johari,amesema kuwa wamefurahishwa na makubaliano yaliyofikiwa na nchi hizi na kueleza kuwa Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini itaendelea kutafuta fursa kama hizi ili kuifungua Tanzania duniani.