Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Bw. Antony Mtaka akizungumza wakati akizindua mwongozo wa mafunzo yaliyolenga kuwajengea uwezo vijana wa Skauti kutoa elimu ya rushwa ili kupanua wigo zaidi kueneza elimu ya rushwa kwa makundi mengine uliofanyika leo November 3,2021 jijini Dodoma.
Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Dodoma bw. Sosthenes Kibwengo akizungumza wakati uzinduzi wa muongozo wa mafunzo yaliyolenga kuwajengea uwezo vijana wa Skauti kutoa elimu ya rushwa ili kupanua wigo zaidi kueneza elimu ya rushwa kwa makundi mengine uliofanyika leo November 3,2021 jijini Dodoma.
Kamishna wa Skauti Mkoa wa Dodoma Salama Katunda akizungumza wakati uzinduzi wa muongozo wa mafunzo yaliyolenga kuwajengea uwezo vijana wa Skauti kutoa elimu ya rushwa ili kupanua wigo zaidi kueneza elimu ya rushwa kwa makundi mengine uliofanyika leo November 3,2021 jijini Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Bw. Antony Mtaka wa pili kutoka kushoto waliokaa akiwa katika picha ya pamoja na vijana wa skauti wakati uzinduzi wa muongozo wa mafunzo yaliyolenga kuwajengea uwezo vijana wa Skauti kutoa elimu ya rushwa ili kupanua wigo zaidi kueneza elimu ya rushwa kwa makundi mengine.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Bw. Antony Mtaka wa pili kutoka kushoto waliokaa akiwa katika picha ya pamoja na wakuu wa TAKUKURU Wilaya za Dodoma wakati uzinduzi wa muongozo wa mafunzo yaliyolenga kuwajengea uwezo vijana wa Skauti kutoa elimu ya rushwa ili kupanua wigo zaidi kueneza elimu ya rushwa kwa makundi mengine.
…………………………………………………………………….
Na.Alex Sonna,Dodoma
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma bw. Antony Mtaka amezindua mafunzo ya muongozo wa wawezeshaji kufundisha vijana wa skauti elimu ya rushwa huku akisisitiza TAKUKURU kueneza zaidi mafunzo ya rushwa na kuhakikisha klabu za wapinga rushwa zinaanzishwa katika shule na vyuo vyote Mkoani Dodoma.
Akizungumza wakati alipokuwa akizindua muongozo wa mafunzo hayo yaliyolenga kuwajengea uwezo vijana wa Skauti kutoa elimu ya rushwa Mtaka amesema lazima wapanue wigo zaidi kueneza elimu ya rushwa kwa makundi mengine.
“Nipongeze ushirikiano huu utasaidia sana kuenea kwa elimu hiyo skauti ni vijana wazalendo hivyo elimu ya rushwa wanayoipata itaenea zaidi na ni watu sahihi katika kutoa elimu hii,
Hapa Mkoa wa Dodoma tuna shule takribani 1000 hizi shule zote zikiwa na klabu za wapinga rushwa tutakuwa na kizazi kizuri cha baadaye kinachochukia rushwa na sio kufundishwa elimu ya rushwa mtu akiwa tayari kaajiliwa” amesema.
Amewataka TAKUKURU kuongeza zaidi elimu hasa kwa wanafunzi katika ngazi za chini kwa kuwa ndio waajili na waajiliwa wa baadaye elimu ikitolewa nzuri tutapunguza kwa kiasi kikubwa vitendo vya rushwa na kujenga kizazi chenye maadili.
“Unajua kwanini ukristo na uislamu havifi ni kwa sababu wamewekeza tangu watoto wanakuwa na kufundishwa hivyo hivyo kwenye rushwa mkiwekeza kikamilifu kwa wanafunzi mtajenga jamii imara inayochukia rushwa” amesema.
Kwa upande wake Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Dodoma Bw. Sosthenes Kibwengo amesema wameamua kuingia kuwapa mafunzo vijana wa skauti kwa kuwa misingi na wajibu wao ni uzalendo, uwajibikaji, na uadilifu hivyo wakipewa mafunzo litakuwa jambo jema kwa kueneza zaidi elimu hiyo kwa jamii.
“Ukiangalia misingi ya Skauti kwanza ni kundi la watoto miaka mitano hadi hadi ishirini na sita tuliona hili ni kundi muhimu na ukizingatia misingi ya kazi zao ukaona ni watu sahihi wa kutoa elimu ya rushwa katika mkoa wa Dodoma” amesema Kibwengo.
Amesema katika mafunzo hayo watatoa maada mbalimbali kwa vijana wa skauti ikiwamo TAKUKURU na ushirikishwaji wa umma katika mapambano ya rushwa, misingi na mbinu za skauti kujenga uzalendo, uadilifu na uwajibikaji, muundo wa matumizi ya muongozo wawezeshaji kujenga uzalendo uadilifu na uwajibikaji kwa vijana wa skauti.
Amesema katika kuendelea kutoa elimu ya rushwa wamefanya semina mbalimbali katika makundi mbalimbali na kufungua klabu 26 mpya katika shule na vyuo na kuendelea kuimarisha klabu za wapinga rushwa ili kupanua wigo zaidi wa utoaji wa elimu ya rushwa.
Ameongeza kuwa “Elimu tunayotoa imesaidia sana kama unavyojua tulitoa elimu katika ofisi za umma na binafsi kuwa na mifumo ya kushughulikia vitendo vya rushwa imeanza kuzaa matunda ambapo tumeona chuo kikuu cha Dodoma mkufunzi aliyekutwa na kosa la rushwa ya ngono kachukuliwa hatua” amesema.
Amebainisha kuwa kwa hapa Dodoma kuna miradi mingi ya kimkakati hivyo wanatoa elimu hasa kwa vijana kutoa taarifa za kitendo vya rushwa wanapofika katika miradi hiyo kuomba nafasi na kuombwa rushwa ili waripoti vitendo hivyo.
Nae kamishna wa Skauti Mkoa wa Dodoma Salama Katunda amesema Skauti ni chama cha hiari ambacho hakifungamani na dini wala chama cha siasa na itikadi yoyote kikiwa na lengo la kulea vijana kimaadili, ukakamavu na uzalendo.
Amesema kwa mwaka 2021 chama hicho kwa Mkoa wa Dodoma kimefanikiwa kupata mafunzo ya uokoaji kwa kushirikiana na jeshi la zimamoto na uokoaji na kushirikiana na kitengo cha maafa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu ikiwa ni kuwajengea uwezo kwa kupambana na majanga mbalimbali.
Ameongeza kuwa “Wao kama Skauti watahakikisha wanashirikiana na TAKUKURU katika kufikia malengo ya kuhakikisha elimu ya rushwa inawafikia watu wengi hasa kundi la vijana” amesema Salama.