WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Mohamed Mchengerwa,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akitoa taarifa ya wizara yake kuhusu mafanikio yaliyopatika kwa kipindi cha miaka 60 ya Uhuru wa Tanganyika leo November 2,2021 jijini Dodoma
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Mohamed Mchengerwa,akisisitiza jambo wakati akitoa taarifa ya wizara yake kuhusu mafanikio yaliyopatika kwa kipindi cha miaka 60 ya Uhuru wa Tanganyika leo November 2,2021 jijini Dodoma
Baadhi ya waandishi wa habari wakifatilia hotuba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Mohamed Mchengerwa,wakati akitoa taarifa ya wizara yake kuhusu mafanikio yaliyopatika kwa kipindi cha miaka 60 ya Uhuru wa Tanganyika leo November 2,2021 jijini Dodoma.
………………………………………………………………
Na.Alex Sonna,Dodoma
KATIKA kipindi cha miaka 60 ya Uhuru Serikali imepata mafanikio mengi ambayo ni pamoja na kuongezeka kwa ajira katika utumishi wa umma kutoka watumishi 17,565 mwaka 1961 hadi 528,290 mwezi Oktoba, 2021.
Hayo yamesemwa leo November 2,2021 jijini Dodoma Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Mohamed Mchengerwa,wakati akitoa taarifa ya wizara yake kuhusu mafanikio yaliyopatika kwa kipindi cha miaka 60 ya Uhuru.
Mchengerwa amesema katika kipindi cha miaka 60 ya uhuru utumishi wa umma umeendelea kuwa uliotukuka katika kuchangia ustawi wa Taifa kwa kuongeza ajira nyingi zaidi.
“Kati ya hao watumishi wa sekta ya afya wamefika 72,961 sawa na asilimia 13.8 na walimu wamefika 281,729 sawa na asilimia 53.3”amesema
Amesema kuwa watu wengi hawajui kuwa Tanganyika ilipopata uhuru walikuwa na madaktari 12 tu nchi nzima na wahandisi wawili huku asilimia 58 wananchi walikuwa hawajui kusoma wala kuandika.
Waziri Mchengerwa ametaja mafanikio mengine ni kuboresha mfumo shiriki wa taarifa za kiutumishi na mishahara (HCMIS) na kujengewa uwezo wa watumishi kutoka Taasisi za serikali za 427 kutumia mfumo huo.
“Pia kuwaondoa kwenye orodha ya malipo ya mishahara watumishi 15,578 waliobainika kughushi vyeti vya kufaulu mtihani wa kidato cha nne, cha sita na ualimu kati ya watumishi 535,770 waliohakikiwa”amesisitiza
Aidha amesema kuwa wamewaondoa katika orodha ya malipo ya mishahara watumishi 5,335 walioajiriwa katika utumishi wa umma kinyume na sifa za miundo ya maendeleo ya kiutumishi.
Hata hivyo ameelezea kuwa wamewaondoa katika orodha ya malipo ya mishahara watumishi hewa 19,708 na kuiwezesha serikali kuokoa jumla ya Sh.bilioni 19.84.
“Kuimarika kwa mfumo wa kitaasisi wa usimamizi wa serikali mtandao kwa kuanzisha sheria ya serikali mtandao namba 10 ya mwaka 2019 na kanuni zake za mwaka 2020 zinazoweka utaratibu na masharti ya kisheria kuhusu utekelezaji,usimamizi na uendeshaji wa serikali mtandao nchini”amesema