Meneja Huduma kwa wateja Tanga Uwasa Alawi Ahmed akizungumza wakati wa semina ya
ya wadau wa Tanga Uwasa kwa kundi Maalumu la Viongozi wa Serikali za Mitaa ambao ni Wakina Mama iliyofanyika ofisi za Mamlaka hiyo kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja Tanga Uwasa Rogers
Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja Tanga Uwasa Rogers akizungumza wakati wa semina |
AFISA Uhusiano wa Tanga Uwasa Devotha Mayalla akizungumza wakati wa semina hiyo
AFISA Uhusiano Msaidizi wa Tanga Uwasa Anna Makange akisisitiza jambo wakati wa semina hiyo
Mkutano ukiendelea |
Sehemu ya Washiriki wa semina hiyo wakifuatilia matukio mbalimbali
NA OSCAR ASSENGA,TANGA
MAMLAKA ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (Tanga Uwasa) imesema kwamba itawasilisha ombi kwa Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Spora Liana ya kuwaomba wenyeviti wa serikali za mitaa wakati wa mikutano yao wazungumzie suala la huduma ya maji safi na usafi wa mazingira.
Hayo yalisemwa na Meneja Huduma kwa wateja Tanga Uwasa Alawi Ahmed wakati semina ya wadau wa Tanga Uwasa kwa kundi Maalumu la Viongozi wa Serikali za Mitaa ambao ni Wakina Mama iliyofanyika ofisi za Mamlaka hiyo ambapo alisema viongozi hao wapo karibu sana na wananchi na ndio wanajua kero zao za kila siku.
Semina hiyo ilihusu matumizi Sahihi ya Maji Safi na Mtandao wa Maji Taka,Haki na wajibu wa Mteja wa Tanga Uwasa sambamba na kuelezwa haki na wajibu wa Tanga Uwasa iliyofanyika kwenye ofisi za Mamlaka hiyo zilizopo Mtaa wa Swahili Jijini humo.
Alisema wanafanya hivyo kwa sababu viongozi hao wapo karibu sana na wananchi ndio ambao wanajua kero za kila wakati na serikali kuu inazijua kupitia serikali za mitaa na Taasisi mbalimbali zinazoenda kuratibu mambo mbalimbali lakini wao wana nafasi wa kujua kero za wananchi.
“Lakini niwaambie kwamba nyinyi viongozi wa serikali za mitaa ni kiunganishi cha kero za wananchi kutatuliwa niwaombe na hili ombi tutalipeleka Halmashauri ya Jiji kwa nia nzuri ya kuweza kuwasaidia wananchi kila kwenye mkutano wa serikali za mtaa zungumzieni suala la huduma ya maji safi na usafi wa mazingira”Alisema
Alisema wameamua kufanya semina hiyo ili kutaka kufanya huduma ya maji iwe bora na endelevu kila wakati na watawaeleza kwamba wanatakiwa kufanya nini ili huduma hiyo iweze kuwa endelevu ili kama wananchi na viongozi waweze kutoa ushirikiano kwa mmalaka ya maji na serikali kufanya huduma iwe bora.
“Ushirikishwaji wa Jamii ni muhimu kwa sababu wao ndio watumiaji maji,walinzi wa huduma za maji wao ndio wanatarajia kusema kwamba nini kifanyike lakini ningependa kila mtu atambue wajibu wake,haki zake zilizopo kwenye huduma ya maji na naamini mambo yatakwenda vizuri “Alisema
Awali akizungumza katika semina hiyo wakati akifunga Afisa Uhusiano wa Tanga Uwasa Devotha Mayalla aliwataka wenyeviti hao watakapokuwa wakifanya mikutano yao wawaite.
Aliwataka pia wahakikisha wanafikisha elimu waliyoipata kwa wasichana wao wa kazi na watoto wao huku akieleza maoni yao wameyapokea na watakwenda kuyafanyia kazi .
“Niwashukuru sana na ninaimani tutaendelea kushirikiana na msiache kutoa taarifa za changamoto za maji mnazokutana nazo lakini pia mnapofanya mikutano yenu ya mitaa tuiteni”Alisema Afisa Uhusiano huyo.
Hata hivyo mshiriki kutoka Mtaa wa Muungano B Kata Ngamiani Kusini Tunu Ally Rashidi alisema elimu waliyoipata watakwenda kuwahamisha wananchi kuhusu matumizi sahihi ya maji safi na mtandao wa maji taka.
Aidha alisema pia watakwenda kueneza elimu hiyo kwa wananchi wengine ili kuweza kuona umuhimu wa matumizi sahihi ya maji katika maeneo yao.