Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo,akifungua Mkutano wa mwaka wa tathmini ya maendeleo ya sekta ya elimu ambao pamoja na mambo mengine utachambua hali halisi ya sekta ya elimu na maandalizi ya mpango wa tatu wa sekta hiyo kwa miaka mitano (2021/22 – 2025/26) ulioanza leo November 2,2021 jijini Dodoma
Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo,akisisitiza jambo kwa washiriki wakati wa Mkutano wa mwaka wa tathmini ya maendeleo ya sekta ya elimu ambao pamoja na mambo mengine utachambua hali halisi ya sekta ya elimu na maandalizi ya mpango wa tatu wa sekta hiyo kwa miaka mitano (2021/22 – 2025/26) ulioanza leo November 2,2021 jijini Dodoma
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Prof James Mdoe,akizungumza wakati wa Mkutano wa mwaka wa tathmini ya maendeleo ya sekta ya elimu ambao pamoja na mambo mengine utachambua hali halisi ya sekta ya elimu na maandalizi ya mpango wa tatu wa sekta hiyo kwa miaka mitano (2021/22 – 2025/26) ulioanza leo November 2,2021 jijini Dodoma
Naibu Katibu Mkuu anayeshughulika Elimu OR-TAMISEMI, Gerald Mweli,akizungumza wakati wa Mkutano wa mwaka wa tathmini ya maendeleo ya sekta ya elimu ambao pamoja na mambo mengine utachambua hali halisi ya sekta ya elimu na maandalizi ya mpango wa tatu wa sekta hiyo kwa miaka mitano (2021/22 – 2025/26) ulioanza leo November 2,2021 jijini Dodoma
Mwenyekiti wa Mtandao wa Mashirika yasiyo ya kiserikali yanayofanya kazi kwenye sekta ya elimu, ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la HakiElimu, Dk.John Kallaghe,akizungumza kwenye Mkutano wa mwaka wa tathmini ya maendeleo ya sekta ya elimu ambao pamoja na mambo mengine utachambua hali halisi ya sekta ya elimu na maandalizi ya mpango wa tatu wa sekta hiyo kwa miaka mitano (2021/22 – 2025/26) ulioanza leo November 2,2021 jijini Dodoma
Mwenyekiti wa Washirika wa Maendeleo, Dk.Daniel Baheta,akizungumza wakati wa Mkutano wa mwaka wa tathmini ya maendeleo ya sekta ya elimu ambao pamoja na mambo mengine utachambua hali halisi ya sekta ya elimu na maandalizi ya mpango wa tatu wa sekta hiyo kwa miaka mitano (2021/22 – 2025/26) ulioanza leo November 2,2021 jijini Dodoma
Baadhi ya washiriki wa Mkutano wakifatilia hotuba mbalimbali wakati wa Mkutano wa mwaka wa tathmini ya maendeleo ya sekta ya elimu ambao pamoja na mambo mengine utachambua hali halisi ya sekta ya elimu na maandalizi ya mpango wa tatu wa sekta hiyo kwa miaka mitano (2021/22 – 2025/26) ulioanza leo November 2,2021 jijini Dodoma
Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua Mkutano wa mwaka wa tathmini ya maendeleo ya sekta ya elimu ambao pamoja na mambo mengine utachambua hali halisi ya sekta ya elimu na maandalizi ya mpango wa tatu wa sekta hiyo kwa miaka mitano (2021/22 – 2025/26) ulioanza leo November 2,2021 jijini Dodoma
……………………………………………………………
Na.Alex Sonna,Dodoma
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo amewataka wadau wa elimu hapa nchini kushiriki ipasavyo katika mapitio ya Sera ya Elimu na Mafunzo ya elimu na kutoa maoni yao kwa uwazi ili kuendana na mahitaji ya sasa kwa maendeleo ya taifa.
Dkt. Akwilapo ameyasema hayo leo Novemba 2, 2021 jijini Dodoma wakati akifungua Mkutano wa mwaka wa tathmini ya maendeleo ya sekta ya elimu hapa nchini ambapo pamoja na mambo mengine utachambua hali halisi ya sekta ya elimu na maandalizi ya mpango wa tatu wa sekta hiyo kwa miaka mitano (2021/22 – 2025/26).
Amesema Serikali inathamini sana maoni ya wadau ili kuboresha hali ya sekta ya elimu hapa nchini ili kuinua kiwango cha elimu inayotolewa hapa nchini.
“Wizara itashirikisha wadau wote kwenye zoezi la kuandika Sera mpya ya elimu, kazi ambayo imeanza kwa vikao vya ndani, muda mfupi ujao tutakuja kwenu wadau ili nanyi mtoe mchango wenu kwenye zoezi hili muhimu sana kwa wananchi wa Tanzania.” Amesema Dkt. Akwilapo.
Amesema Serikali imekuwa ikifanya kila jitihada katika kuboresha elimu katika hilo serikali kwa mwaka 2020/21 imewarudisha kuendelea na masomo wanafunzi wa kike na kiume 3,956 walioacha shule kwa sababu mbalimbali lengo ni kuhakikisha jamii inapata elimu.
“Kwa mwaka 2020/21 wanafunzi 3,668 wamerudi na kufanya mitihani wa Darasa la 7 na kujiunga na Kidato cha Kwanza (Wavulana 2353, Wasichana ni 1315) katika maeneo mbalimbali hapa nchini.
Pia amebainisha kuwa waliwarudisha shuleni kwa ngazi ya kidato cha tano jumla ya wanafunzi 288 (Wasichana ni 149, Wavulana ni 139) waliokuwa wameacha shule katika ngazi ya sekondari juhudi zetu hazitaishia hapo tutaziendeleza ili tuwarudishe wengi zaidi shuleni,”amesema Dkt Akwilapo.
“Naamini mnatambua namna Rais wetu, Mhe. Samia Suluhu Hassan anavyothamini sekta yetu ya elimu kwa kweli ametutendea mengi katika muda huu mfupi, hakutuacha pia katika fedha za hivi karibuni za IMF, ambapo mmesikia jinsi tutakavyopata idadi kubwa ya madarasa” amesema.
Amesema ujenzi wa madarasa elfu 15 hapa nchini utaondoa uhaba wa madarasa kwani kuna ongezeko kubwa la wanafunzi katika kidato cha kwanza kama mlivyoona kwenye matokeo ya mtihani wa darasa la 7, yaliyotangazwa juzi jumla ya wanafunzi 907,802 wamefaulu na wanapaswa kuendelea na masomo ya sekondari,” amesema.
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu anayeshughulika Elimu OR-TAMISEMI, Gerald Mweli, amesema ofisi yake itahakikisha inasimamia ipasavyo miundombinu ya elimu na watashirikiana na Wizara ya elimu kuhakikisha elimu inakuwa na ubora mkubwa hapa nchini.
Naye Mwenyekiti wa Washirika wa Maendeleo, Dk.Daniel Baheta,amepongeza jitihada za serikali za kuboresha sekta hiyo na wao watahakikisha wanasaidia utoaji wa elimu bora kwa watoto wa kitanzania.
Awali Mwenyekiti wa Mtandao wa Mashirika yasiyo ya kiserikali yanayofanya kazi kwenye sekta ya elimu, ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la HakiElimu, Dkt.John Kallaghe, amesema kumekuwa na mafanikio makubwa yaliyopatikana kwenye mpango uliopita ikiwamo ongezeko la bajeti ya sekta hiyo kutoka Sh.Trilioni 4.7 hadi takribani 5.2.
“Uamuzi wa serikali wa kujenga shule 300 za kata ni uamuzi mzuri ambao utasaidia wanaomaliza darasa la saba kuendelea na masomo ya sekondari, mtakumbuka kwamba udahili umeongezeka kwa kiasi kikubwa kwa mfano watoto wote ambao wapo elimu ya awali hadi sekondari wameongezeka kutoka milioni 14.7 hadi 15.2,” Amesema.
Amesema wao kama wadau wa elimu wamependekeza umuhimu wa kuongeza uwekezaji kwenye bajeti ya elimu kwenye mapato ya ndani kutokana na wafadhili kuathiriwa na Uviko-19 ni vyema serikali kupitia mapato ya ndani ikaongeza uwezo.