Mkurugenzi Mkuu Wakala wa Mbegu ASA Dkt, Sophia Kashenge akimkabidhi mfuko wa mbegu Mkuu wa mkoa wa Shinyanga ,Mheshimiwa Sophia Mjema Mkuu wa mkoa wa Shinyanga ,Mhe.Sophia Mjema akiwa na Mkurugenzi Mkuu Wakala wa Mbegu ASA Dkt, Sophia Kashenge na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Janista Mboneko
Na, Lucas Raphael,Shinyanga
Wakati serikali imetoa Taarifa ya kuwepo kwa mvua chache kwa msimu wa kilimo 2021/2022 Wakala wa Mbegu za kilimo ASA wameanza kusambaza Mbegu bora za kilimo zitakazo kabiliana na ukame huku zikiwa na mavuno mengi.
Akizingumza katika uzinduzi wa kituo cha usambazaji wa Mbegu bora za kilimo mkoani shinyanga na Kanda ya Ziwa Mkurugenzi Mkuu Wakala wa Mbegu ASA Dkt, Sophia Kashenge amesema Kama Wakala wameanza kusambaza Mbegu zinazohimili ukame kwa mazingira yote ya hapa Nchini.
Alisema Wakala unachukua tahadhari kubwa dhidi ya hali ya hewa iliyotangazwa na mamlaka husika kwa kuanza kuzindua vituo vya usambazaji wa Mbegu zitakazo wafikia wananchi kwa haraka na ukalibu Zaidi.
Akizingumzia swala la bei ya Mbegu hizo Dkt, Sophia alisema serikali imeweka bei rafiki kwa wakulima kila Mkulima anaweza kununua Mbegu hizo na kuzipanda.
Aliwataka wakulima kuzingatia kilimo bora kutokana na kupata Mbegu bora ambazo zitatoa mazao mengi kwa lengo la kupambana na umasikini.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga ,Sophia Mjema akizindua kituo Cha usambazaji wa Mbegu za kilimo ASA mkoani humo alisema mkoa umepokea Mbegu hizo ambazo zitasambazwa kwa wakulima na kuuzwa kwa bei nafuu.
Alisema Mbegu hizo zimefikia wakati muafaka kutokana na msimu wa Kanda ya Ziwa ni msimu wa kilimo ambapo wakulima wanakila sababu ya kuchangamkia Mbegu hizo.
Alisema Mbegu hizo ni kilo 190,000 ambapo kuna Mbegu za Alizeti,Mbegu za mahindi aina ya Situka M1 pamoja na T 105 Mbegu hizo zote zikipatikana mkoani shinyanga.
Mjema aliwataka maafisa ugani wa mkoa wa shinyanga kutokaa ofisini badala yake watoe maelekezo kwa wananchi ili waweze kunufaika na Mbegu hizo.
Aliongeza kusema kwamba Mbegu hizo za Wakala zinahimili ukame kwa mazingira yote nakuongeza kuwa kwa mkoa wa shinyanga Mbegu hizo ndio mahali pake.
Wakizumza kwa nyakati tofauti wakuu wa wilaya za mkoa wa Shinyanga wameahidi kuyafanyia kazi maelekezo yote yaliyotolewa na Mkuu wa mkoa wa huo
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Janista Mboneko alisema hata akikisha wakulima wanalima Mbegu hizo ilikukabiliana na hali ya ukame.