Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Uyui Said Ntahondi (wa pili kutoka kushoto)akisoma dua leo kabla ya kuanza kwa Kikao cha Robo ya Kwanza cha Baraza la Madiwani.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani (aliyesimama) akitoa salamu za Serikali leo wakati wa kikao cha robo ya kwanza cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Uyui.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani (kulia) akipokea barua ya kupongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan iliyotolewa na Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Uyui wakimshukuru kwa kuwapatia zaidi ya bilioni 3.6 za kuboresha miundombinu ya elimu. Barua hiyo imekabidhiwa kwa niaba yao na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Said Ntahondi(kushoto) wakati wa kikao cha robo ya kwanza cha Baraza la Madiwani.
Mkuu wa Wilaya ya Uyui Kisare Makori(aliyesimama) akitoa salamu za Serikali leo wakati wa kikao cha robo ya kwanza cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Uyui.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Uyui Said Ntahondi akifungua leo Kikao cha Robo ya Kwanza cha Baraza la Madiwani.
Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Uyui wakiimba wimbo wa Taifa leo kabla Mwenyekiti hajafungua leo Kikao cha Robo ya Kwanza cha Baraza la Madiwani
Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Uyui wakiwa leo katika Kikao cha Robo ya Kwanza cha Baraza la Madiwani
Mbunge wa Jimbo la Igalula Venant Protas akitoa mchango wake leo wakati wa Kikao cha Robo ya Kwanza cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Uyui
Picha na Tiganya Vincent
…………………………………………………..
NA TIGANYA VINCENT
Kauli hiyo imetolewa leo na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani wakati akihutubia kikao cha robo ya kwanza cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Uyui.
Alisema kati ya fedha hizo kiasi cha shilingi bilioni 11.7 zitakwenda kujenga madarasa 585 katika Sekondari za Halmashauri zote tayari kwa ajili ya kupokea wanafunzi ambao watakuwa wamechaguliwa kujiunga na Kidato cha kwanza hapo mwakani.
Balozi Dkt. Batilda alisema kiasi kingine cha shilingi bilioni 5.3 zitatumika katika ujenzi wa madarasa 266 katika Vituo vya Shikizi vya Shule za Msingi.
Aliongeza kuwa kiasi milioni 160 zitatumika katika ujenzi wa mabweni kwa shule za watoto wenye mahitaji maalum.
Balozi Dkt. Batilda alisema shilingi milioni 550.9 ni kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya upelekaji wa maji kwenye Shule ikiwemo ya kunawa mikono, uvunaji wa maji ya mvua , kuchimba visima katika shule 28 za Msingi na Sekondari .
“Kwa kweli ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan , sisi watu wa Tabora imetuheshimisha sana …kwa kipindi kifupi ya uongozi wa Mama Samia tumepata fedha nyingi kwa ajili ya uboreshaji wa upatikanaji wa huduma za afya , elimu, maji na barabara …tunasena Wabhezya sana Mama Samia Suluhu Hassan” alisisitiza.
Balozi Dkt. Batilda alisema kufuatia heshimiwa kubwa walioyopeta amesimamisha kwa muda safari za nje ya Mkoa kwa Watumishi wa umma katika kipindi cha utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa madarasa ya Sekondari na Shule Shikizi ili yakamilike kwa wakati.
Alisema watumishi hao wanatakiwa kwenda kwenye maeneo ya miradi ya ujenzi kwa ajili ya kuhakikisha wanasimamia ili imalizike kwa kabla ya Mwezi Desemba na kwa ubora uliokusudiwa.
Aidha Balozi Dkt. Batilda alisema Serikali haitamuonea huruma mtu yoyote atakayetumia fedha hizo kinyume cha malengo yake.