Mtalaamu wa jiolojia John Bosco,akitoa mada mbalimbali wakati wa warsha ya kuwajengea uelewa wa sekta ya Nishati Jadidifu na Maendeleo ya Jamii waandishi wa habari iliyoandaliwa na HakiMadini kwa kushirikiana na wataalamu wa sheria kutoka Chuo kikuu cha Dar es salaam pamoja na Wizara ya Nishati kuhusu utafiti wa fursa na changamoto za nishati jadidifu na mchango wake katika kukuza uchumi wa nchi yaliyofanyika Bagamoyo Mkoani Pwani.
Mkufunzi kutoka HakiMadini,akitoa mada wakati wa warsha ya kuwajengea uelewa wa sekta ya Nishati Jadidifu na Maendeleo ya Jamii waandishi wa habari iliyoandaliwa na HakiMadini kwa kushirikiana na wataalamu wa sheria kutoka Chuo kikuu cha Dar es salaam pamoja na Wizara ya Nishati kuhusu utafiti wa fursa na changamoto za nishati jadidifu na mchango wake katika kukuza uchumi wa nchi yaliyofanyika Bagamoyo Mkoani Pwani.
Mtalamu wa masuala ya Nishati Mhandisi Arthur Karomba akilezea mada mbalimbali kuhusu umeme jua wakati wa warsha ya kuwajengea uelewa wa sekta ya Nishati Jadidifu na Maendeleo ya Jamii waandishi wa habari iliyoandaliwa na HakiMadini kwa kushirikiana na wataalamu wa sheria kutoka Chuo kikuu cha Dar es salaam pamoja na Wizara ya Nishati kuhusu utafiti wa fursa na changamoto za nishati jadidifu na mchango wake katika kukuza uchumi wa nchi. yaliyofanyika Bagamoyo Mkoani Pwani.
Baadhi ya waandishi wa habari wakifatilia mada mbalimbali wakati wa warsha ya kuwajengea uelewa wa sekta ya Nishati Jadidifu na Maendeleo ya Jamii waandishi wa habari iliyoandaliwa na HakiMadini kwa kushirikiana na wataalamu wa sheria kutoka Chuo kikuu cha Dar es salaam pamoja na Wizara ya Nishati kuhusu utafiti wa fursa na changamoto za nishati jadidifu na mchango wake katika kukuza uchumi wa nchi iliyofanyika Bagamoyo Mkoani Pwani.
Profesa Majombo kutoka Kitivo cha Sheria Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM)akifafanua jambo wakati wa semina wakati wa warsha ya kuwajengea uelewa wa sekta ya Nishati Jadidifu na Maendeleo ya Jamii waandishi wa habari iliyoandaliwa na HakiMadini kwa kushirikiana na wataalamu wa sheria kutoka Chuo kikuu cha Dar es salaam pamoja na Wizara ya Nishati kuhusu utafiti wa fursa na changamoto za nishati jadidifu na mchango wake katika kukuza uchumi wa nchi iliyofanyika Bagamoyo Mkoani Pwani.
Na.Alex Sonna
WAKATI Dunia ikikutana nchini Uingereza kwa ajili ya Mkutano 26 wa nchi wanachama wa Mkataba wa umoja wa mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi,ulioanza leo Oktoba 31, hadi Novemba 12,2021 Mtalaamu wa Jiolojia, John Bosco amesema Tanzania imebarikiwa kuwa na rasilimali ya kuzalisha nishati jadidifu ambayo ni muhimu katika kudhibiti mabadiliko ya tabianchi pamoja na kuongeza upatikanaji wa nishati mbalimbali hasa umeme kwa ajili ya uzalishaji katika viwanda.
Bosco amesema hayo wakati warsha ya kuwajengea uelewa waandishi wa habari kuhusu sekta ya Nishati Jadidifu iliyoandaliwa na HakiMadini.
Semina hiyo ilihusisha wakifunzi kutoka kada mbalimbali kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), pamoja na Wizara ya Nishati kuhusu utafiti wa fursa na changamoto za nishati jadidifu na mchango wake katika kukuza uchumi wa nchi iliyofanyika Bagamoyo Mkoani Pwani.
Amesema Tanzania inaweza kutumia rasilimali nyingi za nishati jadidifu ambazo hazijatumika ambazo ni jua, upepo, taka, makaa ya mawe, joto ardhi, chuma na nyingine nyingi ambazo zikitumika ipasavyo kutakuwa na umeme wa uhakika, mazingira yatatunzwa na uchumi utakuwa.
”Kwa sasa vyanzo vya umeme vinavyozalishwa nchini huchangia zaidi ya silimia 60 ya umeme ambao upo kwenye gridi ya taifa, umeme wa jua ambao unaweza kuzalisha hadi megawati 100 katika mikoa ya Dodoma, Singida, Manyara, Shinyanga, Simiyu, Iringa,” amesema Bosco.
Pia amewataka waandishi wa habari kuelimisha jamii zaidi kuhusu utajiri wa asili ambao Tanzania inayo ambao unaweza kutumika kubadilisha njia za uzalishaji wa nishati na kukuza uzalishaji na maisha ya watu wa kawaida.
Aidha, amesema kuwa mikoa hiyo pia ina fursa ya kuzalisha umeme unaotokana na upepo hali ambayo itaongeza vyanzo vingi vya umeme na kuifanya nchi kuwa na umeme wa uhakika kama Rais Samia Suluhu Hassan alivyoweka bayana kuwa ni vyanzo muhimu.
“Kutokana na kasi ya mabadiliko ya tabianchi, tunahitaji kuchanganya vyanzo vya nishati ili kuwa na uhakika wakati wote. Hivyo basi tuangalie uwezekano wa kutekeleza miradi ya nishati jadidifu (jua, upepo, jotoardhi), kwa kuwa vyanzo hivi ni endelevu, tunatarajia kutoka katika miaka hii mitano kuzalisha Megawati 1,100 kupitia vyanzo hivyo,”alisema Samia.
Katika upande wa taka Tanzania inazalisha zaidi ya tani 30,000 kwa siku huku uwezo wa kuzisafisha ukiwa ni chini ya asilimia 50 kwa kila mkoa.
Kwa mujibu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Dar es Salaam pekee inatarijiwa kuzalisha taka mara dufu hadi tani zaidi ya elfu 12 ikifika mwaka 2025.
Uchafu wa majumbani ni asilimia 75 ya taka zote zinazozalishwa jijini Dar es Salaam na sehemu kubwa ya taka hizo hutupwa kiholela kutokana na kuwa na utaratibu mbovu wa ukusanyaji na uteketezaji wa taka.
”Katika mazingira hayo tunaamini kuwa nishati jadidifu nchini ni lulu iliyojificha hivyo siku ikionekana na kuwepo uwekezaji itaweza kufanya mapinduzi ya maendeleo, uchumi na jamii.”amesisitiza
Ukiangalia matumizi ya nishati jadidifu kwenye nchi zilizoendelea kama Marekani ni wazi sekta hiyo ni fursa adhimu ambayo inahitaji uwekezaji mkubwa ili kuweza kumkomboa Mtanzania.
“Kwa Marekani takwimu zinaonesha kuwa vyanzo vya umeme vinatokana na mafuta asilimia 35, gesi asilia asilimia 34, nyuklia asilimia 9, makaa ya mawe asilimia 10 na nishati jadidifu asilimia 12.
Kutokana na faida zinazoonekana katika nchi zilizoendelea ni wazi kuwa ili Tanzania ipate maendeleo ya haraka hakuna njia mbadala tofauti na uwekezaji katika miradi mikubwa ya nishati ikiwemo nishati jadidifu.
Mafunzo hayo yalidhamiria kutoa elimu endelevu kwa waandishi wa habari ili kutoa chachu kwa viongozi husika na jamii kujua na kubuni njia za uzalishaji wa nishati jadidifu ambayo zaidi ya kurahisisha maisha ya Mtanzania lakini pia inaweza kutumika kama chanzo cha biashara.