Mwenyekiti wa Vituo vyote Kanisa Halisi la MUNGU BABA Ndani na Nje ya Nchi ya Tanzania, BABA Halisi akizungumza katika Ibada Maalumu ya kuwaombea Mama Ntilie na Baba Lishe iliyofanyika Makao Makuu ya Kanisa la MUNGU BABA Tegeta, Jijini Dar es Salaam
Mwenyekiti wa Vituo vyote Kanisa Halisi la MUNGU BABA Ndani na Nje ya Nchi ya Tanzania, BABA Halisi akiwabariki waumini wa kanisa hilo walioshiriki katika Ibada Maalumu ya kuwaombea Mama Ntilie na Baba Lishe iliyofanyika Makao Makuu ya Kanisa la MUNGU BABA Tegeta, Jijini Dar es Salaam
Waumini wa Kanisa la MUNGU BABA wakishiriki Ibada Maalumu ya kuwabariki na kuwaombea Mama Ntilie na Baba Lishe iliyofanyika Makao Makuu ya Kanisa hilo Tegeta, Jijini Dar es Salaam
………………………………………………………….
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM.
Kanisa la MUNGU BABA limefanya maombi maalamu ya kuwaombea na kuwabariki watu wanaofanya kazi ya kuuza chakula wanaojulikana kwa jina la Mama Ntilie na Baba lishe ili waweze kufanikiwa katika biashara na kupiga hatua katika nyanja mbalimbali za kiuchumi.
Akizungumza katika ibada maalumu ya kuwabariki Baba lishe na Mama Ntilie iliyofanyika Makao Makuu ya Kanisa la MUNGU BABA leo Jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa vituo vyote vya Kanisa hilo Ndani na Nje ya nchi ya Tanzania, BABA Halisi, amewatakia baraka katika biashara zao pamoja na Mwenyezi Mungu kuwaepusha na changamoto mbalimbali.
BABA Halisi amewataka Mama Ntilie na Baba Lishe waendelee kumtegemea Mwenyezi Mungu katika kipindi chote wakayi wanafanya biashara ya kuuza chakula jambo ambalo ni rafiki katika kuhakikisha wanapiga hatua katika uchumi.
Awali BABA Halisi alifanya ibada ya kumuombea mema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katika safari kwenda Glasgow, Scotland kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa 26 wa Umoja wa Mataifa.
Mhe. Rais Samia ameondoka nchini Oktoba 30 mwaka huu katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam kuelekea Glasgow, Scotland katika Mkutano wa 26 ambao utakaojadili kuhusu athari za mabadiliko ya tabia za nchi pamoja na jitihada za kupunguza uzalishaji wa hewa ya ukaa ili kupunguza joto Duniani.
BABA Halisi, amesema kuwa watanzania wanatakiwa kumuombe Rais katika safari yake ili aweze kwenda na kurudi salama.
BABA Halisi amesema kuwa Mhe. Rais Samia tunatakiwa kumuombea kila siku katika maombi yetu ili aendelea kuliongoza taifa la Tanzania na kupiga hatua katika nyanja mbalimbali za kimaendeleo.
Hata hivyo amesema kuwa pia ni vizuri kuendelea kuliombea Taifa ili Mungu aliepushe na changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa mvua.
Amesema kuwa watanzania wanatakiwa kuendelea na maombi katika kuhakikisha kunakuwa na mvua jambo ambalo litasaidia kuondoa ukame katika maeneo mbalimbali yenye upungufu wa mvua.
Oktoba 27 mwaka huu Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) ilitoa utabiri kutakuwa na upungufu wa mvua nchini katika maeneo yanayopata msimu mmoja hali itakayoathiri sekta za uchumi.
Kanisa Halisi la Mungu Baba limekuwa linahimiza waumimi wake kuzalisha kwa kuwapa kauli mbiu katika kila ibada kwamba “Ibada ni uzalishaji, Uzalishaji siyo aibu” pamoja na kuendelea kufanya kazi kwa bidii.
Ili kuhamasisha waumini wake kufanya kazi kanisa mara kwa mara limekuwa likifanya ibada maalumu kwa kuwaombea makundi mbalimbali yanaofanya kazi ya uzalishaji katika shughuli za kiuchumi.
Katika mwendelezo wa dhana hiyo, Kanisa hilo limekuwa likiandaa ibada maalum ya Mauzo na Uzalishaji, ilifanyika Jumapili, Oktoba 10, 2021 kwa kalenda ya Kanisa hilo ni (26 Abu Vol.2), ambapo wamekaribisha bila ubaguzi wa aina yoyote wazalishaji na wafanyabiashara wa bidhaa mbalimbali kwa ajili ya kuuza na kutangaza bidhaa zao.
Kuanzia siku kanisa Halisi la MUNGU BABA lilipoanza kufundisha kuwa Ibada ni Uzalishaji, kulitokea maswali ndani na nje ya Kanisa! Walioko ndani ya Kanisa walikutana na kile alichofanya Yesu alipoingia ndani ya Hekalu akakuta Meza za wafanyabiashara na kuzipiga mateke huku akisema nyumba ya Baba yake ni ya sala (Mathayo 21:12-13).
Hawakujua kuwa Yesu alikuwa na maana ya kufukuza wapangaji wabaya ndani ya Moyo, ambao wanatakiwa kufutika ili Mzalishaji azalishe utajiri kwa amani, wapangaji hao ni wale walioandikwa katika Marko7:21-23.
Walioko nje ya kanisa wao waliona ni mafundisho yasiyoeleweka kwa kuwa walifundishwa kuwa Kanisani ni mahali pa kwenda kumlilia MUNGU wakati wa shida na taabu peke yake.
Hawakukumbuka kuwa, wakati wa kuumba kwa mara ya kwanza, MUNGU BABA yaani chanzo cha mema na mazuri, alianza kwa kuweka heshima na utajiri ndani ya ule Moyo wa Mwanzo aliouengua kushoto kwake (Mithali 3:16).