Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani (kulia) akipokea barua ya kupongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan iliyotolewa na Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Uyui wakimshukuru kwa kuwapatia zaidi ya bilioni 3.6 za kuboresha miundombinu ya elimu. Barua hiyo imekabidhiwa kwa niaba yao na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Said Ntahondi(kushoto) wakati wa kikao cha robo ya kwanza cha Baraza la Madiwani.
……………………………………………………….
NA TIGANYA VINCENT
HALMASHAURI ya Wilaya ya Uyui imetuma barua ya pongeza kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuwapatia kiasi cha shilingi bilioni 3.6 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa vyumba 123 vya madarasa kupitia Mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano ya UVIKO 19 .
Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Said Ntahondi kwa niaba wenzake ameikabidhi barua hiyo leo kwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani kwa ajili ya kumfikishia Rais Samia.
Alisema kwa kipindi kifupi cha uongozi wa Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia , Uyui imepata fedha nyingi kwa ajili ya kuboresha sekta ya elimu, afya, maji na miundombinu ya barabara.
Alisema kati ya fedha hizo shilingi bilioni 2.4 ni kwa ajili ya ujenzi wa madarasa ya Sekondari na bilioni 1.1 kwa ajili ya vyumba vya madarasa katika Shule Shikizi.
Ntahondi alisema kuwa kiasi cha shilingi milioni 90 ni za ujenzi wa watumishi wa sekta ya afya na milioni 14.1 kwa ajili ya fedha za ufuatiliaji.
Alisema watahakikisha watumia kiasi cha milioni 20 kukamilisha darasa moja kama walivyoekelezwa na kiasi kibaki .
Ntahondi aliongeza hivi Madiwani na Watendaji wa Halmashauri hiyo wamejipanga kusimamia ili kuhakikisha fedha zinatumika kwa makusudio yalipangwa.
Aidha Mwenyekiti huyo alisema aliwafanyia Rais Samia ameshamaliza kazi