Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo Baraka Zikatimu akitoa maelezo mafupi leo kabla hajamkaribisha Mwenyekiti kufungua kikao.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo Adam Malunkwi akifungua kikao cha Baraza la Madiwani leo.
Mkuu wa Wilaya ya Urambo Louis Bura akitoa salamu za Serikali wakati wa Kikao cha Kawaida cha Robo ya Kwanza cha Baraza la Madiwani.
leo.
Baadhi ya wajumbe wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo wakiwa katika Kikao cha Kawaida cha Robo ya Kwanza cha Baraza lao.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani akitoa salamu za Serikali wakati wa Kikao cha Kawaida cha Robo ya Kwanza cha Baraza la Madiwani.
Picha na Tiganya Vincent
*************************
NA TIGANYA VINCENT
MKUU wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani amewaagiza wasimamizi wa miradi ya ujenzi miundombinu inayotekelezwa chini ya Mpango wa Maendeleo kwa ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya UVIKO 19 kuwa makini na matumizi ya fedha hizo ili itekeze malengo yaliyokusudiwa.
Alisema ni vema kila hatua ya utekelezaji wa miradi hiyo wakawa na utaratibu wa kuchukua picha ya hali halisi ili kudhibiti udanganyifu unaoweza kufanywa na baadhi wasimamizi wasio waaminifu.
Balozi Dkt. Batilda alitoa kauli hiyo leo wakati kikao cha kawaida cha robo ya kwanza ya Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo.
Alisema picha zisipochukuliwa kabla ya ujenzi kuanza wapo baadhi ya watumishi wasio waaminifu wanaweza kukabati mamboma ya zamani na kudai wamejenga majengo mapya.
Balozi Dkt. Batilda alisema kila hatua ya utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa miundombinu inayotokana na fedha zilizotolewa na Serikali ya Awamu ya Sita inaoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan chini ya Mpango wa Maendeleo kwa ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya UVIKO 19 lazima ziwe wazi na miradi yote ipigwe picha.
“Tushirikiane kusimamia ujenzi wa miundombinu ili iwe na ubora kama alioulenga Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan la kuhakikisha anaboresha sekta ya elimu na afya .. hizo fedha mzione kama kaa la moto ni lazima zifanye kazi iliyokusdiwa” alisema
Balozi Dkt.Batilda alisema ili kufanikiwa hilo , kila Halmashauri lazima iunde Kamati ya uratibu na ufutiliaji na kila baada ya siku nne itote taarifa kwa Katibu Tawala Mkoa kuhusu maendeleo ya ujenzi wa miradi yao.
Aidha Mkuu huyo wa Mkoa wa Tabora aliwaagiza Wakurugenzi kuhakikisha miradi ya ujenzi wa miundombinu ya shule za Sekondari na Shule Shikizi inakamilika kabla ya Desemba mwaka huo.
Alisema lengo la Serikali ni kuhakikisha Watoto watakuwa wamechaguliwa kujiunga na Kidato cha Kwanza hapo mwakani wanaanza masomo kwa Pamoja na kuondokana na kuanza kwa awamu.