**********************************
– Awataka Wanaofanya biashara maeneo yaliyokatazwa kuwahi nafasi hizo.
– Awaumbua baadhi ya Wafanyabiashara wanaopotosha Kuwa nafasi zimejaa.
-Asema mwisho wa kuhama maeneo yaliyokatazwa ni Kesho.
– Asema Serikali itashughulikia changamoto zote zinazowakabili.
– Wafanyabiashara Wampongeza zoezi la kuwapanga kufanyika pasipo uvunjifu wa amani.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla amewataka Wafanyabiashara Wanaofanya biashara maeneo yaliyokatazwa hususani Kariakoo kufika Soko la Machinga complex kwaajili ya kupatiwa nafasi Kutokana na Soko hilo kusaliwa na nafasi 2,400 za Wafanyabiashara.
RC Makalla amesema hayo alipotembelea Soko hilo na kueleza kuwa mpaka Sasa Zaidi ya Wafanyabiashara 2,200 wamepatiwa maeneo ya kufanyia biashara na wanafurahia biashara zinakwenda vizuri sokoni apo.
Aidha RC Makalla amesema Serikali imedhamiria kutatua changamoto zote za kibiashara kwenye maeneo walipopelekw Wafanyabiashara ikiwa ni pamoja na kuelekeza LATRA kufikisha huduma ya Usafiri wa Daladala kwenye maeneo hayo ikiwemo Soko la Machinga ili kuchochea Biashara.
Hata hivyo RC Makalla amesema ifikapo siku ya kesho ndio mwisho wa watu kufanya biashara kwenye maeneo yaliyokatazwa Kutokana na muda wa siku 12 alizoongeza kufikia kikomo.
Pamoja na hayo RC Makalla amesema zoezi la kuwapanga vizuri Machinga kwa Mkoa huo linakwenda vizuri na kwa utulivu wa Hali ya juu Kutokana na elimu iliyotolewa na Serikali na Viongozi wa Machinga.