Mkuu wa wilaya ya Longido Nurdin Babu akizungumza katika mkutano huo uliofanyika jijini Arusha na kuwashirikisha wadau mbalimbali.(Happy Lazaro)
Baadhi ya washiriki wa mkutano huo wakifuatilia mada mbalimbali za kuhusu mabadiliko ya tabia ya nchi jijini Arusha (Happy Lazaro)
************************
Happy Lazaro, Arusha.
Arusha.Mkuu wa wilaya ya Longido Nurdin Babu amesema kuwa mabadiliko ya tabia ya nchi yanachochea kuongezeka kwa changamoto ya kati ya binadamu na wanyama ambapo wameshuhudia yakileta madhara kwa wananchi waishio pembezoni mwa hifadhi mbalimbali.
Babu ameyasema hayo wakati akifungua kikao cha wadau wa mradi wa mabadiliko ya tabia ya nchi kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Arusha John Mongela, mkutano uliofanyika mkoani Arusha.
Babu amesema kuwa, mabadiliko ya tabia ya nchi yamekuwa ni changamoto kubwa kwa maisha ya binadamu na maendeleo ya kiuchumi ya mtu mmoja mmoja na nchi kwa ujumla.
“Wanyama wanakosa maji na chakula porini jambo linalosababisha wanasogea karibu na makazi ya watu lakini nao binadamu kwa kutafuta ardhi yenye rutuba kwa ajili ya kilimo na mifugo wanajikuta wanasogea zaidi karibu na maeneo ya hifadhi jambo linaloleta muingiliano na migogoro Kati ya binadamu na wanyama pori,” amesema Babu .
Amesema kuwa, mradi wa mabadiliko ya tabia ya nchi umewezesha ujenzi wa Malambo ambao utasaidia kupunguza muingiliano kati ya binadamu na wanyama hasa pale yanapopatikana maji ya kutosha kwa ajili ya wanyama pori na mifugo ambapo zimetengenezwa pampu za maji zinazotumia umeme wa jua,pamoja na kuweka uzio wa kuzuia wanyamapori kuvamia maeneo ya makazi na mashamba.
“Mradi huu umetekelezwa kwa muda mfupi na ipo katika kiwango kinachokidhi vigezo na mahitaji na kwa kweli binafsi na kwa niaba ya serikali niwashukuru kwa kujitolea katika kukamislisha kazi hii nafahamu wapo walioufanya kazi usiku na mchana kuhakikisha mradi unakamika,” amesema .
Amewaagiza wananchi waliopo katika maeneo ambayo miradi hiyo imetekelezwa kuhakikisha wanatunza miradi hiyo na kutumika kukidhi malengo yaliyokusudiwa kwani WWF wamewasaidia lakini hawategemei warudi kuja kusimamia miradi hiyo kwani kwa sasa ni ya kwao ,hivyo wailinde ,waihudumie na kuitunza ili iwasaidie kupunguza makali ya mabadiliko ya tabia ya nchi.
Babu amesema kuwa, mradi huo unafikia mwisho lakini bado wanahitaji msaada mwingine katika kuhakikisha wanaibua miradi mingine ili wananchi weweze kunufaika lakini kwa wakati mwingine hizi WMA zisimame zenyewe kusiwe na visingizio kwani jamii nyingi zinategemea maliasili kiuchumi na kimaendeleo.
Naye Meneja wa mradi huo ,Novat Kessy amesema kuwa, mradi huo unatekelezwa na shirika la uhifadhi wa mazingira (WWF) ambapo wamefanya mradi huo ili kuzijengea jamii uwezo wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi ambapo katika maeneo ya Kaskazini madhara makubwa ni ukame na wamekuja na mkakati wa kuwewezesha kukabiliana nayo.
Amesema kuwa, jamii wanazofanya nazo kazi ni wafugaji na wamekuwa wakitembea umbali mrefu kufuata maji ambapo wamewasaidia kwa kuwajengea mabwawa makubwa(Malambo) kwani wamekuwa wakipata mvua chache na ili maji yake yasipotee mabwa hayo yanatumika kwa kuhifadhia maji yatayotumika wakati wa ukame.
Naye Mtaalamu wa wanyapori kutoka WWF Tanzania ,Profesa Noah Sitati amesema kuwa, hadi sasa Kuna maji katika maeneo yote ambayo wamefanyia mradi huo na wananchi wamenufaika kwa kiasi kikubwa sana na kuondokana na changamoto mbalimbali zilizokuwa zinawakabili.
Amefafanua kuwa, kumalizika kwa mradi huo umepelekea kuanzishwa kwa mradi mwingine wa miaka mitatu utakaoanza January 2022 ambao utahusika na masuala ya Tembo na maradi huo unaanziswa mahususi kutokana ongezeko kubwa la idadi ya tembo ambao wanavamia makazi ya watu kutokana na wingi wao.