Mrajisi wa Vyama vya Ushirika nchini Dkt Benson Ndiege akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Chama cha kuweka na kukopa cha Polisi (URA SACCOS) jijini Mbeya (Picha na A/INSP Frank Lukwaro wa Jeshi la Polisi)
Mwenyekiti wa Bodi ya Chama cha kuweka na kukopa cha Polisi (URA SACCOS) Kamishna wa Polisi Benedict Wakulyamba akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 13 wa chama hicho jijini Mbeya (Picha na A/INSP Frank Lukwaro wa Jeshi la Polisi)
Mrajisi wa Vyama vya Ushirika nchini Dkt Benson Ndiege akisalimiana na Mwenyekiti wa Bodi ya Chama cha kuweka na kukopa cha Polisi (URA SACCOS) Kamishna wa Polisi Benedict Wakulyamba (Kulia) wakati alipowasili kwa ajili ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 13 wa chama hicho jijini Mbeya (Picha na A/INSP Frank Lukwaro wa Jeshi la Polisi)
Baadhi ya Wajumbe wa Mkutano mkuu wa Chama kuweka na kukopa cha Polisi (URA SACCOS) wakiwa katika picha ya pamoja baada ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 13 wa chama hicho jijini Mbeya (Picha na A/INSP Frank Lukwaro wa Jeshi la Polisi)
*********************************
Leo tarehe 29.10.2021 Mrajis Mkuu wa vyama vya ushirika nchini Dkt. BENSON NDIEGE amefungua mkutano mkuu wa 13 wa chama cha kuweka na kukopa cha Jeshi la Polisi nchini (URA SACCOS LTD) ambao kitaifa mkutano huo unafanyikia mkoa wa Mbeya katika ukumbi wa mikutano wa “Modern Mbeya Highlands Hotel”.
Akifungua mkutano huo, Mgeni rasmi Dkt. Ndiege ameipongeza bodi ya URA SACCOS LTD, wajumbe, watendaji na wawakilishi kwa mafanikio waliyofikia tangu kuanzishwa kwa chama hicho 2006.
Aidha amewataka kuangalia uwezekano wa kuendelea kupunguza riba kutoka asilimia 8 ya sasa hadi 7 ili wanachama waweze kufaidika zaidi kwa kukopa na kufanya maendeleo zaidi.
Pia amewaomba wajumbe wa mkutano kuhakikisha wanatoa elimu kwa wanachama kuhusiana na umuhimu wa ushirika, faida zake ili kila mwanachama aweze kujiimarisha kiuchumi kwa kuanzisha miradi mbalimbali yenye tija kwake na taifa kwa ujumla.
Mwisho, ametoa pongezi za dhati kwa mlezi wa ushirika ambaye ni Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini {IGP} Simon Sirro kwa kuendelea kusimamia ushirika hadi kupata mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kupata hati safi ya ukaguzi wa hesabu za chama na tuzo mbalimbali za vyama vya ushirika nchini.
Mkutano umehudhuriwa na Mrajis msaidizi, m/kiti wa bodi taifa Kamishna wa Polis Utawala na Rasilimali Watu BENEDICT M. WAKULYAMBA, Makamu M/kiti Naibu Kamishna wa Polisi FAUSTINE SHILOGILE, Katibu wa bodi Kamishna Msaidizi wa Polisi KIM MWEMFULA, wajumbe wa bodi akiwemo Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi DAVID MISIME ambaye pia ni msemaji wa Jeshi la Polisi, watendaji na wawakilishi wa URA SACCOS LTD toka mikoa na wilaya zote za Tanzania bara na visiwani pamoja na wawakilishi toka vyama vya ushirika marafiki ambavyo ni ngome na uhamiaji.
KAULI MBIU YA MWAKA HUU NI “KUJIIMARISHA KIFEDHA KWA USTAWI WA SIKU ZIJAZO”