Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Kheri Mahimbali akizungumza wakati wa kikao cha Wizara ya Nishati na Taasisi ya Natural Resource Governance Institute, kilichofanyika katika ofisi za Wizara ya Nishati, zilizopo katika mji wa Serikali, jijini Dodoma. Oktoba 29,2021.
Mkurugenzi wa Sera na Mipango, Petro Lyatuu (kwanza-kulia) Kamishna Msaidizi wa Nishati Jadidifu, Edward Ishegoma (katikati) Kamishna Msaidizi wa Gesi, Mohamed Fakihi (kwanza-kushoto) wakimsikiza muwasilishaji wa utafiti wa kuhusiana na rasilimali ya Gesi Asilia nchini Tanzania, Silas Okin’g (hayupo pichani),katika kikao cha Wizara ya Nishati na Taasisi ya Natural Resource Governance Institute, kilichofanyika katika ofisi za Wizara ya Nishati, zilizopo katika mji wa Serikali, jijini Dodoma. Oktoba 29,2021.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Kheri Mahimbali (katikati) akiendesha kikao cha Wizara ya Nishati na Taasisi ya Natural Resource Governance Institute, kilichofanyika katika ofisi za Wizara ya Nishati, zilizopo katika mji wa Serikali, jijini Dodoma. Oktoba 29,2021.
Muwasilishaji wa utafiti wa kuhusiana na rasilimali ya Gesi Asilia nchini Tanzania, Silas Okin’g (kwanza-kulia) akiwasilisha tafiti katika kikao cha Wizara ya Nishati na Taasisi ya Natural Resource Governance Institute kilichofanyika katika ofisi za Wizara ya Nishati, zilizopo katika mji wa Serikali, jijini Dodoma. Oktoba 29,2021. Wengine watumishi mbalimbali wa Wizara ya Nishati na Taasisi zake.
Picha za washiriki mbalimbali kwenye kikao cha Wizara ya Nishati na Taasisi ya Natural Resource Governance Institute kilichofanyika katika ofisi za Wizara ya Nishati, zilizopo katika mji wa Serikali, jijini Dodoma
****************************
Hafsa Omar-Dodoma
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Kheri Mahimbali ameitaka Taasisi inayojishughulisha na utafiti ya (Natural Resource Governance Institute) kuishirikisha Serikali kwenye tafiti zinazohusu Serikali ili kuwa na usahihi wa takwimu zinazotolewa.
Ameyasema hayo, Oktoba 29,2021 wakati wa kikao cha Wizara ya Nishati na Taasisi hiyo kilichofanyika katika ofisi za Wizara ya Nishati, zilizopo katika mji wa Serikali, jijini Dodoma ambapo Taasisi hiyo iliwasilisha tafiti yao kuhusiana na rasilimali ya Gesi Asilia nchini Tanzania.
Aidha, alisema ushirikiano wa Serikali na Taasisi hizo utasaidia kupata takwimu zilizo sahihi ambazo zitakuwa zenye manufaa kwa Taifa kiujumla.
“Haipendeza tafiti mbalimbali kusambazwa kwa wananchi bila ya Serikali kushirikishwa na kutoa maoni yao unapofanya tafiti lazima ungalie na upande wa pili ambao ni Serikali,” alisisitiza Mahimbali.
Alisema, Serikali itaendelea kufanya kazi na kushirikiana na Taasisi hiyo katika tafiti mbalimbali na kwakuwa inaisadia Serikali kupata takwimu mbalimbali muhimu.
Kikao hicho, kilihudhiriwa na Kamishna Msaidizi wa Gesi, Mohamed Fakihi, Kamishna Msaidizi wa Nishati Jadidifu, Edward Ishegoma, Mkurugenzi wa Sera Mipango Petro Lyatuu pamoja na watumishi mbalimbali wa Wizara ya Nishati na Taasisi zilizopo chini yake.