Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Martine Shigela akisalimiana na wachezaji wa timu ya netiboli ya Ofisi ya Rais Ikulu wakati wa mechi yao dhidi ya timu ya RAS Morogoro leo Oktoba 28, 2021 katika uwanja wa Jamhuri Morogoro ambapo Timu ya Ofisi ya Rais Ikulu wameifunga timu ya RAS Morogoro kwa jumla ya magoli 45-17 wakati wa Mashindano ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) yanayoendelea mkoani Morogoro.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Martine Shigela akisalimiana na wachezaji wa timu ya netiboli ya timu ya RAS Morogoro katika uwanja wa Jamhuri Morogoro ambapo Timu ya Ofisi ya Rais Ikulu wameifunga timu ya RAS Morogoro kwa jumla ya magoli 45-17 wakati wa Mashindano ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) yanayoendelea mkoani Morogoro.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Martine Shigela akisalimiana na wachezaji wa timu ya netiboli ya Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) wakati wa mechi yao dhidi ya timu ya RAS Morogoro leo Oktoba 28, 2021 katika uwanja wa Jamhuri Morogoro ambapo TAMISEMI wameifunga timu ya RAS Ruvuma kwa jumla ya magoli 57-12 wakati wa Mashindano ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) yanayoendelea mkoani Morogoro.
Mchezaji wa timu ya netiboli ya Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Mwajuma Banyasa (GS) akiudhibiti mpira dhidi ya mchezaji Jamila Awadhi wa timu. Hadi mwisho wa mchezo Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo wameifunga timu ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Mkazi kwa jumla ya magoli 22-18 wakati wa Mashindano ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) yanayoendelea mkoani Morogoro.
Mchezaji wa timu ya netiboli ya RAS Morogoro Neema Manugwa (GK) akimdhibiti mchezaji wa timu ya Ofisi ya Rais Ikulu Lilian Sylidion (GS) ambapo timu ya Ofisi ya Rais Ikulu iliibika kidedea kwa kuwafunga RAS Morogoro kwa jumla ya magoli 45-17 leo Oktoba 28, 2021 katika uwanja wa Jamhuri Morogoro wakati wa Mashindano ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) yanayoendelea mkoani humo.
Mchezaji wa timu ya netiboli ya Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Dafroza Atilio (GA) akiudhibiti mpira mbele ya mpinzani wake Irene Chitimbe wa timu ya RAS Ruvuma wakati wa Mashindano ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) yanayoendelea mkoani Morogoro.
Picha na Eleuteri Mangi, Morogoro
………………………………………………………………………….
Na Eleuteri Mangi, Morogoro
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Martine Shigela amesema hakuna sababu mwaka ujao wa 2022 timu zote za Wizara, Wakala, taasisi, Idara za Serikali pamoja na mikoa ya kutoshiriki Mashindano ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) ambayo hufanyika kila mwaka hapa nchini.
Mkuu wa mkoa Shigela amesema hayo leo Oktoba 28, 2021 mara baada ya kukagua timu za mpira wa netiboli kati ya Ofisi ya Rais Ikulu waliocheza dhidi ya RAS Morogoro pamoja na mechi kati ya timu ya Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) ambao walicheza na timu ya RAS Ruvuma katika uwanja wa Jamhuri Morogoro.
Mhe. Shigela amesema kuwa kufanyika kwa michezo hiyo ni utekelezaji wa maagizo ya Mhe. Makamu wa Rais wa Jmhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango aliyoyatoa Oktoba 23, 2021 wakati akifungua mashindao hayo mkoani Morogoro.
Mkuu wa mkoa ameongeza kuwa watumishi wanapopata fursa na nafasi ya kushiriki Mashindano ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) ni wanamichezo na wanapata wasaa wa kuongeza uwezo wa ubongo kufanyakazi ili kuboresha utendaji wao wa kazi mahala pa kazi ikizingatiwa michezo ni afya.
“Mfanyakazi anapokuja kwenye mashindano haya anajengewa uwezo wa kufanya maamuzi haraka, kwa hiyo wanapokuja kucheza hawaji kwenye anasa, wanakuja kujenga uwezo wa kufanya maamuzi ya sahihi, haraka na kwa wakati” amesema Mkuu huyo wa Mkoa.
Aidha, Mhe. Shigela amesema kuwa Serikali ya mkoa huo wamekubalia na wapo tayari kuendelea kuwa wenyeji wa mashindano hayo kwa kuwahakikishia wanamichezo ulinzi na usalama wakati wote itakapofanyika michezo hiyo.
Mashindano hayo ya mwaka huu yanaendelea mkoani humo ambapo yamefikia hatua ya timu nane bora kwa mchezo wa netiboli ambazo zitashindana kuingia hatua ya timu nne ili kupata washindi watakaocheza nusu fainali na hatimaye fainali ya mashindano hayo.
Timu zilizoingia hatua ya timu nane bora katika mchezo wa netiboli ni Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo ambao wameifunga timu ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Mkazi kwa jumla ya magoli 22-18, timu ya Hazina wameifunga timu ya Wizara ya Maji kwa magoli 33-20, timu ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Ujenzi) wameifunga Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto wameifunga timu ya kwa magoli 22-14, Wizara ya Katiba na Sheria wameifunga timu ya Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA) kwa jumla ya magoli 19-14.
Timu nyingine ambazo zimetinga hatua ya timu nane bora kwa mchezo wa netiboli ni Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ambao wameifunga timu ya Wizara ya Nishati kwa jumla ya magoli 39-16, Timu ya Ofisi ya Rais Ikulu wameifunga timu ya RAS Morogoro kwa jumla ya magoli 45-17, timu ya Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali wameifunga timu ya Wakala wa Hifadhi ya Taifa ya Chakula (NFRA) kwa jumla ya magoli 54-15 na timu ya Ofisi ya Rais TAMISEMI wameifunga timu ya RAS Ruvuma kwa jumla ya magoli 57-12.
Mashindano hayo yanatarajiwa kuhitimishwa Novemba 02, 2021 mkoani Morogoro ambapo inatarajiwa kufanyika fainali za mpira wa miguu, netiboli na mchezo wa kuvuta kamba pamoja na hafla za ufungaji wa mashindano hayo.