Mchezaji Anna Msulwa (wa pili kulia) wa timu ya Ofisi ya Rais Ikulu akitafuta mbinu ya kumshinda Grace Mallya wa Wizara ya Madini (kushoto) katika mchezo wa karata wa hatua ya makundi wa michuano ya Shirikisho la michezo ya Idara na Wizara za Serikali (SHIMIWI) uliofanyika leo kwenye uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro,
Mchezaji Atilio Dafroza (GA) wa Tamisemi akirusha mpira mbele ya Mariam Mangara (GD) wa RAS Ruvuma katika mchezo wa netiboli wa michuano ya Shirikisho la michezo ya Idara na Wizara za Serikali (SHIMIWI) uliofanyika leo kwenye uwanja wa Jamhuri mkoani RAS Ruvuma, ambapo Tamisemi walishinda kwa magoli 57-12.
……………………………………………….
Na Mwandishi Wetu, Morogoro
Timu za Ofisi ya Rais Ikulu, Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali na Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Uchukuzi) zimefuzu hatua ya nane bora ya michezo ya netiboli, soka na kuvuta kamba kwenye michuano ya Shirikisho la Michezo ya Idara na Wizara za Serikali (SHIMIWI) inayofanyika mkoani Morogoro.
Timu hizo zimefuzu baada ya kuwafunga wapinzani wao katika hatua ya nane bora, ambapo Ikulu waliwafunga RAS Morogoro kwa magoli 46-17, huku Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali waliwachapa RAS Tanga katika soka kwa magoli 3-1 na Uchukuzi wanawake waliwavuta Wizara ya Kilimo kwa mvuto 1-0, katika mchezo mkali na wa kusisimua ambapo mivuto miwili ya awali walitoka sare ya mvuto 1-1, ikalazimika kwa mujibu wa kanuni za mchezo huo uongezwe mvuto mmoja na atakayeshinda ndio huvuka kwa hatua inayofuata..
Timu nyingine zilizotinga hatua hiyo ya nane bora katika mchezo wa netiboli ni Hazina,
Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi); Tamisemi, Wizara ya Katiba na Sheria
Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Wizara ya Elimu na Wizara Sanaa, Utamaduni na Michezo; wakati katika upande wa soka timu za Wizara ya Kilimo, Wizara ya Nishati, Wizara ya Ardhi, Tamisemi, Wizara ya Elimu, RAS Mara na Wizara ya Katiba na Sheria nazo zimetinga hatua ya nane bora.
Katika mchezo wa kamba wanawake timu nyingine zilizotinga hatua ya nane bora ni pamoja na RAS Iringa, Ofisi ya Waziri Mkuu, Hazina, Wizara ya Mifugo, Idara ya Mahakama, Tamisemi na Wizara ya Mambo ya Ndani.
Timu zilizofuzu kwa robo fainali kwa upande wa kamba wanaume ni Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi), Idara ya Mahakama, Wizara ya Mambo ya Ndani na Wizara ya Maliasili na Utalii.
Hatahivyo hatua hizo zitafanyika kesho kwa mechi za netiboli timu ya Ikulu kuumana na Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi); huku Hazina watakutana na Tamisemi, nayo Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali watapepetana na Wizara ya Katiba na Sheria, na Wizara ya Sanaa, Utamaduni na Michezo watakwaruzana na Wizara ya Elimu.
Katika mechi za kuvuta kamba kwa wanawake timu ya RAS Iringa watavutana na Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Uchukuzi), huku Ofisi ya Waziri Mkuu watakutana na Hazina, nayo Wizara ya Mifugo watacheza na Idara ya Mahakam ana Tamisemi kutoshana nguvu na Wizara ya Mambo ya Ndani. Katika michezo yar obo fainali kamba wanaume timu ya Wizara ya Mambo ya Ndani watavutana na Wizara ya Maliasili na Utalii; na Wizara ya Ujenzi; na Uchukuzi (Sekta ya Uchukuzi) watawakaribisha Idara ya Mahakama.
Wakati huo huo matokeo ya michezo iliyochezwa leo katika kuvuta kamba wanaume Wizara ya Mifugo 1 vs Sekta ya Ujenzi 0, Wizara ya Mambo ya Ndani 2 vs Hazina 0, Sekta ya Uchukuzi 2 vs Tume ya Uchaguzi 0, Idara ya Mahakama 2 vs Wizara ya Kilimo 0; kwa wanawake Ofisi ya Waziri Mkuu 2 vs Wizara ya Maji 0, Tamisemi 2 vs Wizara ya Katiba na Sheria 0, RAS Iringa 2 vs Tume ya Utumishi wa Walimu 0, Idara ya Mahakama 2 vs Wizara ya Maliasili na Utalii 0, Wizara ya Mifugo 2 vs Wizara ya Madini 0, Wizara ya Mambo ya Ndani 2 vs Tume ya Uchaguzi 0, Hazina 2 vs Wizara ya Sanaa, Utamaduni na Michezo 0.
Katika netiboli Sanaa, Utamaduni na Michezo 22 vs Wizara ya Ardhi 18, Hazina 33 vs Wizara ya Maji 20, Wizara ya Katiba na Sheria 19 vs Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) 14, Sekta ya Ujenzi 22 vs Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto 14, Wizara ya Elimu 39 vs Wizara ya Nishati 16, Tamisemi 57 vs RAS Ruvuma 12, Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali 54 vs Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) 15.
Katika soka Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali 3 vs RAS Tanga 1, Wizara ya Nishati 2 vs afya 1, Wizara ya Ardhi 1 vs Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki 0, Wizara ya Elimu 1 vs Ulinzi 0, Wizara ya Katiba na Sheria 2 vs Ofisi ya Waziri Mkuu 0, Wizara ya Kilimo 2 vs Wizara ya Mifugo 1,Tamisemi 4 vs Tume ya Utumishi wa Walimu 0; na RAS Mara 8 vs RAS Morogoro 7
Mwisho