Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Dk Leonard Akwilapo,akizungumza wakati wa uzinduzi wa mwongozo wa Kitaifa wa utoaji wa huduma ya chakula na lishe kwa wanafunzi wa elimumsingi ulioandaliwa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais TAMISEMI, Shirika lisilo la kiserikali la Project Concern International (PCI) kwa ufadhili wa Serikali ya Marekani kupitia Idara ya Kilimo(USDA) uliofanyika leo Oktoba 29,2021 jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika lisilo la kiserikali la Project Concern International (PCI) Nicholas Fod ambaye shirika hilo limeshirikiana na Serikali kuandaa mwongozo wa Kitaifa wa utoaji wa huduma ya chakula na lishe kwa wanafunzi wa elimumsingi hafla iliyofanyika leo Oktoba 29,2021 jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. James Mdoe, ,akizungumza wakati wa uzinduzi wa mwongozo wa Kitaifa wa utoaji wa huduma ya chakula na lishe kwa wanafunzi wa elimumsingi hafla iliyofanyika leo Oktoba 29,2021 jijini Dodoma.
Baadhi ya wanafunzi wakifatilia hotuba mbalimbali wakati wa uzinduzi wa mwongozo wa Kitaifa wa utoaji wa huduma ya chakula na lishe kwa wanafunzi wa elimumsingi hafla iliyofanyika leo Oktoba 29,2021 jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Dk Leonard Akwilapo,akizundua mwongozo wa Kitaifa wa utoaji wa huduma ya chakula na lishe kwa wanafunzi wa elimumsingi ulioandaliwa Wizara hiyo kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais TAMISEMI, Shirika lisilo la kiserikali la Project Concern International (PCI) kwa ufadhili wa Serikali ya Marekani kupitia Idara ya Kilimo(USDA) hafla iliyofanyika leo Oktoba 29,2021 jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Dk Leonard Akwilapo,akionyesha mwongozo wa Kitaifa wa utoaji wa huduma ya chakula na lishe kwa wanafunzi wa elimumsingi ulioandaliwa Wizara hiyo kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais TAMISEMI, Shirika lisilo la kiserikali la Project Concern International (PCI) kwa ufadhili wa Serikali ya Marekani kupitia Idara ya Kilimo(USDA) hafla iliyofanyika leo Oktoba 29,2021 jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Dk Leonard Akwilapo,akimkabidhi Mkurugenzi Mkazi wa Shirika lisilo la kiserikali la Project Concern International (PCI) Nicholas Fod Mwongozo wa Kitaifa wa utoaji wa huduma ya chakula na lishe kwa wanafunzi wa elimumsingi hafla iliyofanyika leo Oktoba 29,2021 jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Dk Leonard Akwilapo,akimkabidhi Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Prof. Riziki Shemdoe mwongozo wa Kitaifa wa utoaji wa huduma ya chakula na lishe kwa wanafunzi wa elimumsingi ulioandaliwa na Wizara hiyo kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais TAMISEMI, Shirika lisilo la kiserikali la Project Concern International (PCI) kwa ufadhili wa Serikali ya Marekani kupitia Idara ya Kilimo(USDA) hafla iliyofanyika leo Oktoba 29,2021 jijini Dodoma.
……………………………………………..
Na.Alex Sonna, Dodoma.
Serikali kupitia Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia kwa kushirikiana na Shirika lisilo la kiserikali la Project Concern International (PCI) imezindua mwongozo wa Kitaifa wa utoaji wa huduma ya chakula na lishe kwa wanafunzi wa elimumsingi.
Muongozo huo unalenga kuwaelekeza wasimamizi, watekelezaji na wadau namna bora ya kushiriki, kusimamia, kutekeleza na kuboresha utoaji huduma ya chakula na lishe kwa wanafunzi shuleni wa Elimumsingi.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Dk Leonard Akwilapo,amesema kuwa takwimu za mwaka 2021 zinaonesha kuna shule 23,835 za elimumsingi zenye wanafunzi 13,708,242, jambo linalochangia umuhimu wa utekelezaji wa mwongozo huo kuwaokoa wanafunzi na utoro na kuongeza ufaulu.
“Kuna uhusiano mkubwa sana kati ya afya ya mwanafunzi na maendeleo yake kitaaluma, kuna madhara makubwa kwa wanafunzi kukosa chakula shuleni ikiwa ni pamoja na kukosekana kwa usikivu wakati wa ujifunzaji”. Amesema Dkt Akwilapo.
“Upatikanaji wa chakula na lishe bora mashuleni utaongeza hali ya wanafunzi kukaa shuleni kwa usikivu na kuwa tayari kujifunza” amesema.
Aidha Dkt. Akwilapo amefafanua kuwa sera ya elimu na mafunzo ya mwaka 2014 inatamka wazi utoaji wa huduma muhimu kama hizo na ni muhimu zikazingatiwa katika shule zote zilizosajiliwa hapa nchini na kuzitaka kila idara za elimu kufuata muongozo huo.
“Utoaji wa huduma umekuwa ukitekelezwa kwa namna na viwango tofauti, baadhi ya wanafunzi wamekuwa wakinufaika sasa serikali imeandaa mwongozo huu wa kisera ili kuleta uratibu wa kitaifa ambao utanufaisha wanafunzi wote wa shule zote nchini,” amesema.
Amesema kuwa utaratibu wa upatikanaji wa chakula, vyanzo vya upatikanaji wa chakula, mifumo ya uchangiaji, aina ya vyakula, mahitaji muhimu, wajibu na majukumu ya watekelezaji, ufuatiliaji na tathmini.
Dkt.Akwilapo amesema kuwa lengo la uzinduzi wa muongozo huu ni kuufahamisha umma, watendaji Wakuu na wadau wote katika ngazi zote kuhusu uwepo wa muongozo unaoelekeza namna bora ya utoaji, usimamiaji na ufuatiliaji wa huduma ya chakula na lishe shuleni. Uzinduzi huu unalenga kutoa hamasa kwa wadau mbalimbali kuona umuhimu wa kushiriki katika kutoa huduma ya chakula shuleni.
“Nitoe wito kwa wadau wote wa elimu kushiriki kuchangia utoaji wa chakula na lishe kwa kuwa suala hili ni mtambuka linahitaji ushirikiano, ni matumaini yangu kuwa kila mmoja atasoma mwongozo huu na kutekeleza majukumu yote ipasavyo” amesema.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkazi wa PCI, Nicolas Ford amesema Shirika hilo lilitekeleza mpango wa chakula kwa elimu Mkoani Mara ambao umeonesha mafanikio mbalimbali ikiwamo kupunguza utoro na kuboresha mahudhurio kwa asilimia 89 kutoka asilimia 84.5 mwaka 2017.
Ameongeza kuwa mpango umesaidia kuongezeka kwa uelewa wa wazazi na kuongeza kiwango cha uchangiaji mazao ya chakula hadi kufikia tani 1,662 mnamo Septemba 2021.
Nae Kamishna wa Elimu hapa nchini Dkt. Lyabwene Mtahabwa amesema pamoja na juhudi za serikali za kuboresha miundombinu ya ujifunzaji na ufundishaji hazitatoa matokeo tarajaji kama litasahaulika suala la upatikanaji wa chakula kwa wanafunzi.
Awali, Mwakilishi wa Balozi wa Marekani hapa nchini , Benjamin Mtaki ametoa maelezo ya Shirika la USDA, amesema Dola za Marekani milioni 67 zimetumika kwa miaka 10 kutekeleza Mpango wa chakula kwa elimu(FFE) ambao ulitekelezwa kwa awamu tangu mwaka 2010.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hudum za Jamii, Stanslaus Nyongo amepongeza juhudi za Serikali katika kuimarisha Afya ya akili ya wanafunzi huku akiahidi kwa niaba ya Wabunge wenzake kuwa mstari wa mbele kuhamasisha muongozo huo.
” Tunampongeza Rais Samia kwa muongozo huu ambao naamini sasa unakwenda kuboresha Afya ya akili ya wanafunzi wetu, watoto wetu watasoma vizuri kwa sababu ya miundombinu inayowekwa na Serikali yetu lakini pia watakula vizuri.
Nitoe wito kwa viongozi wenzangu wakiwemo Wabunge na Madiwani kusimamia kidete utekelezaji wa muongozo huu na kuunga mkono, tuhamasishe na tusiwe wa kwanza kukwamisha,” Amesema Nyongo.