Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima akizungumza na wanachama wa AZAKI kabla ya kutoa tuzo kwa Asasi zilizofanya vizuri katika hitimisho la Wiki ya AZAKI jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu akizungumza na wanachama wa AZAKI katika hafla ya utoaji tuzo za waliofanya vizuri, jijini Dodoma.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima akitoa tuzo kwa mmoja wa Wanaazaki aliyefanya vizuri katika Sekta ya Mawasiliano katika hitimisho la Wiki ya AZAKI jijini Dodoma.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima akiwa katika picha ya pamoja ya Wana AZAKI waliopata tuzo mbalimbali na katika hafla ya utoaji tuzo kwa AZAKI zilizofanya vizuri jijini Dodoma.
Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WAMJW
…………………………………………………………………….
Na Mwandishi Wetu Dodoma.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto,Dkt Doroth Gwajima amesema Serikali inazitambua Asasi zote za Kiraia kwa kazi nzuri zinazofanya kwa ajili ya manufaa ya jamii na taifa kwa ujumla.
Mhe. Gwajima ameyasema hayo wakati akitoa tuzo mbalimbali kwa baadhi ya Asasi za Kiraia zilizofanya vizuri zaidi katika hafla iliyofanyika jijini Dodoma baada ya kumalizika kwa wiki ya AZAKI.
Mhe. Dkt Gwajima alisema Asasi zote zinafanya vizuri lakini Tuzo hizo zimetolewa kwa wale walionesha ubunifu na kujitolea zaidi katika utendaji kazi zao katika kuhakikisha wananchi wanafaidika na miradi wanayoiendesha katika Mashirika yao.
“Tunapoikuza jamii yetu ya Kitanzania tunamsaidia Rais Samia Suluhu Hassan kutekeleza maono yake kwenyeTaifa hili na nipende kumshukuru kwa maono yake amekuwa akihamasisha tuzidi kuimarisha ushirikiano na Asasi za Kiraia” amesema Dkt. Gwajima.
Kwa upande wake, Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii, Dkt. Jingu ameipongeza AZAKI kwa midahalo iliyofanyika katika wiki yote ambayo ina lengo la kuimarisha utekelezaji wa majukumu yao na kufanya tathmini ya kuboresha katika utekelezaji wa majukumu hayo.
“Nyie kama Wadau wa Maendeleo mkaoneshe kweli kuwa nyie ni wadau kwa kulenga kuleta matokeo zaidi na kubuni namna ya kupata Rasilimali kwa ajili ya kuendeleza shughuli zenu” amesema Dkt. Jingu.
Amesema Wizara itaendelea kutoa ushirikiano kwa Asasi zote za Kiraia ikiwemo utoaji ya miongozo mbalimbali na kuwahimiza waendelee kufanya kazi kwa bidi kwa kuzingatia Sheria, taratibu na kanuni zilizopo.
Naye Rais wa Asasi za kiraia Dkt. Stigmata Tenga ameishukuru Serikali kwa kuthamini mchango wa AZAKI na kuwapa nafasi katika kuchangia maendeleo ya Taifa kupitia miradi mbalimbali inatotekelezwa na Asasi hizo katika maeneo tofauti nchini.
“Wizara imekua ikionesha kutusikiliza na kukaribisha mawazo yetu hivyo kututia moyo zaidi kuendelea kufanya kazi” amesema.