Na Asila Twaha, Morogoro
TAMISEMI Sports Club imeendelea kuonesha ukubwa wake kwenye mashindano ya SHIMIWI kwa kushinda michezo mbalimbali iliyocheza bila kupoteza hata mchezo mmoja.
Katika michezo ya leo 0ktoba 28, 2021 timu ya mpira wa miguu ya TAMISEMI imeifunga timu ya Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC) magoli 4 – 0 katika mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa Chuo Kikuu cha Jordan Morogoro.
TAMISEMI Queens nao kama kawaida yao wakiendeleza rekodi ya ushindi kwa kuifunga Ras Ruvuma kwa magoli 57-12 mchezo huo ukichezwa katika uwanja wa Jamhuri Morogoro.
Kwa upande wa mchezo wa kuvuta kamba TAMISEMI Queens iliendeleza kichapo kwa kuwaburuza Wizara ya Katiba na Sheria kwa alama 2-0.
Doto Bintabara ameiwakilisha vyema timu yake ya TAMISEMI Queens akishiriki mchezo wa jadi (karata) kwa kuwa mshindi wa 3 kwa kupata alama 9 katika kundi C na mchezo huo unatarajiwa kuendelea tena kesho kwa mchezo wa drafti.
Baada ya matokeo ya leo timu ya TAMISEMI Sports Club imeweza kutinga hatua ya robo fainali ratiba ya kesho ikionesha kuwa timu ya TAMISEMI Queens mchezo wa Netiboli inatarajiwa kucheza na timu ya Hazina huku mchezo wa kuvuta kamba wakitarajiwa kucheza na Wizara ya Mambo ya Ndani.