Na Mwamvua Mwinyi,Pwani
MKUU Wa Mkoa wa Pwani , Abubakari Kunenge ,amekemea baadhi ya asasi na mashirika yasiyo ya kiserikali ya mfukoni na zile za kifamilia na badala yake ziweke kipaombele kuhudumia wananchi.
Amesema zipo baadhi ya asasi zinazochafua asasi nyingine kutokana na kushindwa kufuata misingi ya kazi zao .
Akizungumza na wawakilishi wa asasi na mashirika yasiyo ya kiserikali, Kunenge alisema asasi za aina hiyo zijipime kama zina msaada na tija kwa jamii .
Hata hivyo ,alitoa rai mashirika hayo yafanyekazi kwa uwazi ,na matumizi ya fedha kwa maslahi ya jamii, na hategemei kuwepo kwa asasi ama mashirika yasiyo ya kiserikali ya mfukoni yanayojinufaisha na familia zao pekee.
“Mzingatie wananchi kwanza ,sio uchumi wa familia zenu ,wekeni kipaombele kwa wananchi na kuishi kwa kuzingatia vibali vya kazi zenu ,”
“Mashirika yasiyo ya kiserikali yanategemeana na Serikali,Tushirikiane ,tukishafahamiana sote kuwa Ni muhimu ,na mkifuata Sheria ,Tutaenda Pamoja kufikia jamii,:;”!!!Na hapa lazima tuhakikishe mnajua mipaka ,na Serikali ina wajibu gani na kuweka mahusiano na Serikali tutaenda Pamoja “
“Bahati nzuri mahitaji ya wananchi wameshayaeleza mahitaji yao kwa Serikali yao ,Ndio maana katika Serikali tunatekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi ,kulingana na mahitaji ya wananchi”; alifafanua Kunenge.
Wakati huo huo Kunenge alielezea ,mkoa huo umedhamiria kuufungua mkoa kwa kufanya kazi Kama Timu moja kuanzia ngazi ya chini ili kuweza kufanya makubwa na kuwa mfano wa kuigwa ikiwa ni sehemu ya kumsaidia kwa vitendo Rais ,Samia Suluhu Hassan ambae anafanya juhudi kubwa kuinua maendeleo na uchumi wa Taifa.
Mkuu huyo wa mkoa alihimiza pia, wananchi kujitokeza kwenye zoezi la sensa ya watu na makazi ,linalotarajiwa kufanyika 2022.
Vilevile, aliwahimiza wananchi ambao bado hawajapata chanjo ya Uviko 19 , kujitokeza kuchanja katika awamu nyingine ya dozi 25,000 aina ya SINOPHARM kutoka China ili kupambana na ugonjwa huo.
Akizungumza kwa niaba ya Mashirika yasiyo ya kiserikali, Gidioni Haule alibainisha, kwa mkoa wa Pwani kuna asasi 390 ikiwa Ni sawa na asilimia 84 ambapo kati ya hizo zilizohakikiwa ni asilimia 33 .
Haule anaeleza,asasi hizo zinakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa elimu , upungufu wa fedha za miradi na wakati mwingine kukwama kwa kuendeleza mashirika yao kutokana na ufadhili kumalizika.