Meneja wa bodi ya mikopo Tanzania ,Kanda ya kaskazini Arusha,Patrick Shoo(kushoto) akimkabithi tuzo Mkurugenzi wa chuo cha SAUT tawi la Arusha ,Padre Charles Rufyiriza (Happy Lazaro)
********************************
Happy Lazaro, Arusha
Bodi ya Mikopo kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu Tanzania (HESBL) imekabithi tuzo ya utendaji kazi bora katika kuratibu fedha za mikopo ya wanafunzi vyuoni katika chuo cha Mtakatifu Augustino tawi la Arusha .
Akizungumza wakati wa kukabithi tuzo hiyo chuoni hapo ,Meneja wa Bodi ya Mikopo Tanzania , Kanda ya kaskazini Arusha ,Patrick Shoo amesema kuwa utoaji wa tuzo hiyo umekutokana na maamuzi yaliyotolewa katika mkutano wa kikao kazi uliofanyika jijini Mwanza kwa ajili ya kuangalia na kutathmini utendaji kazi wa mwaka uliopita kwa vyuo na bodi ya mikopo ambapo katika kikao kazi hicho Saut tawi la Arusha iliibuka moja ya washindi kwa mara ya nne mfululizo kati ya vyuo vilivyofanya vizuri.
Shoo amesema kuwa, katika kuangalia vyuo hivyo chuo hicho kimefanikiwa kupata tuzo hiyo kwa mara ya nne sasa ,na hivyo kuonyesha namna wanavyotumia fedha za serikali vizuri na kwa mpangilio unaotakiwa na bodi ya mikopo.
Amesema kuwa, upataji wa tuzo hiyo kwa chuo hicho umezingatia katika makundi ya utunzaji wa kumbukumbu za fedha za mikopo ya elimu ya juu kila zinapoletwa chuoni hapo,kurejesha fedha zilizowasilishwa na bodi lakini hazikusainiwa kwa wakati kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo wanafunzi kutokuwemo vyuoni,na utoaji wa huduma rafiki kwa wanafunzi wanufaika wa mikopo .
“chuo hicho kimeonyesha mfano bora wa kuigwa kwani kimekuwa kikipokea tuzo kila wakati ikiwa ni mara ya nne Sasa na tumetoa kwa mkuu wa chuo Saut tawi la Arusha kuwakilisha wakuu wa vyuo wengine ambao vyuo vyao vimepata tuzo zilizokabidhiwa kwa Maofisa mikopo jijini Mwanza”amesema Shoo.
Amefafanua kuwa, katika chuo hicho kwa mwaka wa kwanza wa masomo jumla ya wanafunzi 282 wamepatiwa mkopo wa shs 97.4 milioni kutoka bodi ya mikopo sawa na asilimia 63.3.
Ameseema kuwa,wanategemea kutoa jumla ya shs 731,505 ,250 milioni kwa mwaka mzima kwa wanafunzi hao wa mwaka wa kwanza katika vipengele sita vya ukopeshaji, lengo likiwa ni kuwawezesha kuweza kusoma kwa bidii na kuwa na motisha zaidi ila kila mmoja aweze kufikia malengo ya ndoto zake na kujenga taifa.
“Kwa sasa hivi serikali inatoa fedha kwa wakati huku vyuo navyo vikijitahidi kuwapa wanafunzi hao kwa wakati , kwani mifumo ya utoaji wa mikopo imeboreshwa sana tofauti na zamani na ndiyo maana kauli mbiu ya ya mwaka huu ni Matumizi ya Tehama kwa Huduma Bora Kwa Wanufaika wa Mikopo “amesema Shoo.
Naye Mkurugenzi wa chuo cha SAUT tawi la Arusha,Pandre daktari Charles Rufyiriza ameseema kuwa,anashukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia bodi ya mikopo Tanzania kwa namna ambavyo wanasaidia wazazi kupunguza majukumu kwa kuwakopesha wanafunzi hao kwani asilimia kubwa hawana kipato cha kuwaendeleza wanafunzi wao.
Amesema kuwa,kwa mwaka wa kwanza wameweza kupata mkopo wa asilimia 63.3 kwa wanafunzi wanaosoma ualimu,utalii na sheria na utoaji wa mikopo hiyo kwa wakati unatoa motisha kubwa kwa wanafunzi kuendelea kusoma kwa bidii.
“Tunashukuru Sana kwa tuzo hii kwani tunajitahidi Sana kurejesha marejesho stahiki kwa wakati na tunashukuru Sana bodi kuendelea kutambua umuhimu wa chuo chetu kwa mara ya nne Sasa na wamefanya vizuri Sana na tutaendelea kuwa mfano wa kuigwa kila wakati.”amesema Padre Dokt Rufyiriza.