Home Mchanganyiko WAZAZI WA WANAFUZI WANAOSOMA SUN ACADEMY WATAKIWA KUTOA USHIRIKIANO KWA WALIMU

WAZAZI WA WANAFUZI WANAOSOMA SUN ACADEMY WATAKIWA KUTOA USHIRIKIANO KWA WALIMU

0

Mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo akitoa cheti cha pongezi kwa mwanafunzi aliyefanya vizuri darasani kuliko wengine

Mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo akitoa cheti cha pongezi kwa mwanafunzi aliyefanya vizuri kwa upande wa wanafunzi wa kike

 


Na Fredy Mgunda,Iringa.

 

MKUU wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo amewataka wazazi wa wilaya hiyo kutoa ushirikiano kikamilifu kwa walimu ili kujua maendeleo ya kielimu na maisha mengine ya watoto wao wawapo shuleni

 

Akizungumza kwenye mahafari ya kwanza ya kidato cha nne katika shule ya sekondari ya Sun Academy,Mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo alisema kumekuwa na tatizo kubwa ambalo limejengeka wa baadhi ya wazazi wa wilaya hiyo kutofaatilia taarifa za kimasomo za watoto wao.

 

Alisema wazazi wengi wamekuwa hawatoe ushirikiano kwa walimu kwa kutofika shuleni kufuatilia maendeleo ya watoto kitaaluma ikiwa ni pamoja na kutochukua matokeo ya mitihani ambayo watoto hao wamekuwa wakifanya mara kwa mara.

 

Moyo alisema kuwa wazazi wengi wamekuwa hawashiriki katika majukumu ya kuwanunulia watoto vifaa vya kujifunzia kama vile daftari,vitabu,kalamu na mahitaji mengine muhimu kwa watoto.

 

Alisema kuwa wazazi wengi wamekuwa wanashindwa kuwakemea watoto wao juu ya swala la wanafunzi wengi kuwa watoro na wengine kutofika shuleni mara kwa mara bila taarifa kwa walimu husika huku wazazi hao wakiwa wanafumbia macho jukumu hilo kubwa kwao.

 

Moyo alisema kuwa wazazi na wananchi wengine wanatakiwa kuendelea kutoa elimu ya kupinga ukatili wa kijinsia ambao umekuwa unaleta madhara makubwa kwa jamii na kizazi cha sasa.

 

Aidha Moyo alilitumia jukwa hilo kutoa elimu ya umuhimu wa zoezi la sensa na kuwaomba wananchi wa wilaya ya Iringa kujitokeza kwa wingi kwenda kuchanja ili kujikinga na ugonjwa wa UVIKO 19.

 

Moyo alitumia fursa hiyo kwa kuupongeza uongozi wa shule ya Sekondari ya Sun Academy kwa kufanya vizuri kwenye taaluma kwa kutoa elimu bora ambayo imekuwa inawasaidia wanafunzi wanaosoma katika shule hiyo kufanya vizuri kwenye mitihani mbalimbali ambayo wamekuwa wakiifanya.

 

Awali mkurugenzi wa shule za Sun Academy Nguvu Chengula alisema kuwa shule hizo zimekuwa zinafanya vizuri kutokana na mpangilio mzuri wa masomo ambayo unatekelezwa na walimu wa shule hizo.

 

Alisema kuwa walimu wa shule hizo wamekuwa wanafundisha kwa bidii kubwa kwa kuonyesha uzalendo uliotukuka na kuwawekea ulinzi mzuri wanafunzi wote wanaosoma katika shule hizo ndio siri ya mafanikio ya shule hizo.

 

Nguvu alisema kuwa jumla ya wanafunzi kumi na tisa (19) wanatarajia kufanya mtihani wa taifa wa kidato cha nne waka huu ambao mara kadhaa kwenye mitihani ya majaribia ambayo wamekuwa wanaifanya wamekuwa wakifanya vizuri sana.

 

Alisema kuwa kwenye mtihani wa mock wa manispaa ya Iringa walifaulu kwa division 1 na 2 na kufanikiwa kushika nafasi ya kwanza katika ya shule 31 na katika mtihani wa mock ngazi ya mkoa wa Iringa walifaulu kwa kupata division 1 na 2 na kushika nafasi ya kumi (10) kati ya shule 171.

 

Nguvu alisema kuwa wanatarajia wanafunzi hao kumi na tisa watafanya vizuri kwenye mitihani ya kuhitimu kidato cha nne mwaka huu kwa kupata alama ya kwanza tu (division 1) katika mtihani wa taifa ambao unatajiwa kufanyika 15/10/2020.

 

Lakini pia Mkurugenzi huyo wa Sun Academy Nguvu alimwambia mkuu wa wilaya ya Iringa kuwa shule hiyo itakuwa mfano bora kwa shule nyingine kwa kutoa elimu bora na kufaulisha wanafunzi wengi kwa alama nzuri tu.

 

Nguvu alimalizia kwa kusema kuwa lengo la shule hiyo ni kuwa na wanafunzi wa kidato cha tano na sita ambapo itasaidia kutoa elimu bora kwa wanafunzi wanaotarajia kwenye chuo kikuu hapo baadae.