Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP Ulrich Matei akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mafunzo ya Watendaji na Wawakilishi wa Chama cha kuweka na kukopa cha Jeshi la Polisi (URA SACCOS). Mafunzo hayo yanaendelea jijini Mbeya kwa lengo la kuboresha utoaji huduma kwa Wananchama. Kushoto ni Meneja wa Chama hicho ACP Kim Mwemfula. (Picha na A/INSP Frank Lukwaro wa Jeshi la Polisi)
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP Ulrich Matei akisalimiana na Mjumbe wa Bodi ya Chama cha kuweka na kukopa cha Jeshi la Polisi (URA SACCOS) Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Moses Luvinga wakati alipokuwa akiwasili katika ukumbi wa mkutano kwa ajili ya kufungua Mafunzo ya Watendaji na Wawakilishi wa chama hicho yanayoendelea jijini Mbeya kwa lengo la kuboresha utoaji huduma kwa Wananchama. Wengine ni Maofisa wa Chama hicho. (Picha na A/INSP Frank Lukwaro wa Jeshi la Polisi)
Mjumbe wa Bodi ya Chama cha kuweka na kukopa cha Jeshi la Polisi (URA SACCOS) Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Moses Luvinga akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mafunzo ya Watendaji na Wawakilishi wa chama hicho yanayoendelea jijini Mbeya kwa lengo la kuboresha utoaji huduma kwa Wananchama. Wengine ni Maofisa wa Chama hicho. (Picha na A/INSP Frank Lukwaro wa Jeshi la Polisi)
Meneja wa Chama cha kuweka na kukopa cha Jeshi la Polisi (URA SACCOS) Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP ACP Kim Mwemfula.akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mafunzo ya Watendaji na Wawakilishi wa chama hicho yanayoendelea jijini Mbeya kwa lengo la kuboresha utoaji huduma kwa Wananchama. Wengine ni Maofisa wa Chama hicho. (Picha na A/INSP Frank Lukwaro wa Jeshi la Polisi)
Baadhi ya Watendaji na Wawakilishi wa Chama cha kuweka na kukopa cha Jeshi la Polisi (URA SACCOS) wakifuatilia mada mbalimbali katika Mafunzo yanayoendelea jijini Mbeya kwa lengo la kuboresha utoaji huduma kwa Wananchama wa Chama hicho. (Picha na A/INSP Frank Lukwaro wa Jeshi la Polisi)
*******************************
Na. A/INSP FRANK LUKWARO- JESHI LA POLISI
Watendaji na Wawakilishi wa Chama cha kuweka na kukopa cha Jeshi la Polisi (URA SACCOS) wametakiwa kuzingatia mafunzo wanayopatiwa ili yaweze kuleta tija na kuwavutia zaidi wanachama wapya kujiunga na mfuko huo ambao lengo lake ni kusaidia kuinua uchumi wa familia za Askari Polisi nchini.
Wito huo umetolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP Ulrich Matei wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku mbili kwa Watendaji na Wawakilishi wa Chama hicho kutoka Wilaya na matawi yote Tanzania bara na Zanzibar yanayofanyika Jijini Mbeya .
Kamanda Matei amesema mafunzo ya mara kwa mara kwa watendaji wa chama hicho ni muhimu na yataleta tija pale watendaji hao watakapozingatia na kuelewa yote watakayofundishwa kwa siku hizo mbili ili waweze kutoa huduma bora kwa wateja.
“Nawataka mzingatie mafunzo haya ili mtakaporudi katika maeneo yenu ya kazi mkatatue mapema changamoto zinazowakabili wateja wa mfuko huu na kuwashauri wengine ambao bado hawajajiunga kujiunga ili waweze kunufaika na huduma zinazotolewa na URA SACCOS” Alisema Kamanda Matei
Kwa upande wake Meneja wa URA SACCOS, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Kim Mwemfula amesema mafunzo hayo yanatolewa kila mwaka ili kuwajengea uwezo watendaji wa chama hicho kwakuwa katika maeneo ya kazi wakati mwingine hujitokeza changamoto hivyo mafunzo hayo yataenda kuboresha huduma za chama hicho.
ACP Mwemfula alisema mafunzo hayo yatafuatiwa na mkutano mkuu wa chama hicho utakaofanyika siku ya ijumaa na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali wakiwemo Wajumbe wa bodi ya Chama hicho.
Naye Mjumbe wa Bodi wa Chama hicho Kamishna Msaidizi wa Polisi Moses Luvinga alisema ushirika huo unaendelea kuimarika mwaka hadi mwaka na umekuwa ukifanya vizuiri katika kutoa huduma na wao kama bodi wataendelea kusimamia vyema ili kupata matokeo chanya.