Wachezaji wa Timu ya Mpira wa miguu kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi) waliovaa jezi ya njano, waibuka na ushindi baada ya kuifunga timu ya Wakala wa Usalama na Afya Mahala pa Kazi (OSHA), bao 1-0 Katika dimba la Chuo kikuu cha Jordan, Mkoani Morogoro.
******************************
Michuano ya Shimiwi inaendelea kushika kasi mkoani Morogoro ambako Timu ya mpira wa miguu, kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, (Sekta ya Ujenzi) wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Wakala wa Usalama na Afya Mahala pa Kazi (OSHA), Katika dimba la Chuo kikuu cha Jordan, Mkoani Morogoro.
Katika mchezo huo uliokuwa Na upinzani mkali, Timu ya Ujenzi ilifanikiwa kupata Goli la Ushindi kipindi cha pili katika dakika ya 48 kupitia kwa kiungo wao David mwamakula.
Kwa upande wa mchezo wa kuvuta kamba upande wa wanawake timu ya Wizara ya kilimo iliwachapa 2-0 Timu ya RAS Ruvuma na Ofisi ya Waziri Mkuu waliwashinda Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Uchukuzi) kwa idadi ya 2-0, Huku Wizara ya Maliasili na utalii wakiichapa Wizara ya mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa Mivuto 2-0.
Aidha Timu ya Wachezaji ya Wanawake katika upande wa Kuvuta Kamba (Sekta ya Ujenzi) imeangukia pua katika michuano hiyo baada ya kupoteza michezo yote mitatu tangu kuanza kwa mashindano ya SHIMIWI.
Katika michezo mingine ya kuvuta kamba kwa upande wa Wananume timu ya Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari walitoka suluhu ya 1-1 huku Wizara ya Ujenzi na uchukuzi (sekta ya Ujenzi) nao wakatoshana nguvu na Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa kufungana 1-1 katika mchezo uliopigwa katika dimba la Chuo kikuu cha Kilimo Cha Sokoine (SUA- Kampasi ya Mazimbu).
Michuano Ya SHIMIWI Inatarajiwa kufikia Tamati Novemba 2 ambapo Washindi watazawadiwa Zawadi Mbalimbali vikiwemo Vikombe.