********************************
Na Mwandishi Wetu, Morogoro
Timu ya Tamisemi leo imezoa medali 10 za dhahabu na nne za fedha katika mbio mbalimbali za michuano ya michezo ya Shirikisho la michezo ya Idara na Wizara za Serikali (SHIMIWI) iliyofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro.
Tamisemi yenye wachezaji wengi chipukizi, ilipata medali zake za dhahabu kwa upande wa wanawake katika mbio za mita 100 kupitia kwa Salome Luvanda, mita 200 Deltila Denadusi; mita 400 Tegemea Leah; mita 800 na 1,500 Nuru Mahomilisoli; na kukimbiza vijiti wakiwa ni Metrida Evarist, Salome Luvanda, Tegemea Leah na Beltina Genadius huku kurusha tufe ameshinda Neema Changolo.
Kwa upande wa wanaume waliotwaa medali za dhahabu ni pamoja na Atson Mbughi. kwenye mita 800 na 1,500 na mbio za kupokezana vijiti (x100 relay); wameshinda Edward Michael, Innocent Mbelwa, Lwitiko Mwasege na Ackson Mbugi.
Tamisemi pia ilipata medali za fedha kwa upande wa wanaume kupitia kwa Innocent Mbelwa mita 100 huku Azori Ruvanda kapata kwenye mbio za mita 400 na Lwitiko Mwasega kapata kwenye mita 200 na kurusha tufe.
Nayo timu ya Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali imepata medali za dhahabu kupitia kwa Adam Mahenge mita 200 wanaume, na Casian Luoga aliyerusha tufe kwa wanaume, huku Furaha Kaboneka ametwaa medali ya fedha katika mita 100 na 400.
Timu inashika nafasi ya pili kwa kuwa na medali za fedha kutoka kwa Ramadhani Mwakilongo mita 800 wanaume na Scolastica Hamis mita 1,500 huku medali za shaba zimepatikana kwenye mbio za mita 800 kupitia kwa Scolastica Hamis, na mbio za kupokezana vijini wanawake ambapo walikimbia Jamila Mkomwa, Johari Moshi, Scolastica Hamisi na Magreth Massawe.
Timu nyingine na medali walizopata zikiwa kwenye mabano ni pamoja na Wizara ya Elimu upande wa wanawake Yusta Wetson mita 800; kupokezana vijiti Yusta Wetson, Mary Nyonyi, Nerry Kibasi na Lidia Gasaya na upande wa wanaume mbio za vijiti waliokimbia ni Kulubone Shilie, Seleman Chamshama, Frank Asilia na Zawadi Sanga (medali ya fedha); naye Mary Nyonyi amepata medali ya shaba katika mbio za mita 400 wanawake.
Nayo timu ya Wizara ya Maji imepata medali fedha katika mita 200 wanawake kupitia kwa Jackline Daniel, na kurusha tufe wanaume Said Mmbaga na medali ya shaba kwenye mbio za kupokezana vijiti kwa wanaume kupitia kwa Yusuphu Muhema, Hamisi Samwel, Omary Gumbo na Swalehe Mbuma na Jackline Daniell ametwaa medali ya shaba katika mita 100.
Wizara ya Mifugo na Uvuvi wametwaa medali ya dhahabu kwa wanaume katika mita 100 kupitia kwa Jumanne Bunju, pia akipoata medali ya shaba katika mita 200 na Thabitha Kintingu aliyekimbia mita 1,500; nayo timu ya Hazina imetwaa medali ya dhahabu katika mbio za wazee wenye umri wa miaka 55 na kuendelea kwa upande wa wanaume kupitia kwa Suleiman Juma; na Ally Amoury katwaa medali ya shaba katika mita 400.
Timu nyingine ni Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam (RAS Dar) kupitia kwa Juma Ally ametwaa medali ya shaba katika mita 100; huku Omary Mwenda wa RAS Shinyanga katwaa dhahabu katika mita 400; huku Ezekiel Mhina wa RAS Tanga kwatwaa fedha katika mbio za mita 1,500; naye Sadiki Lusinda wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ametwaa medali ya shaba katika mbio za mita 1,500; huku Juma Ndemi wa Wizara ya Nishati akipata medali ya shaba katika mita 800 wanaume.naye Wilson Dede wa Idara ya Mahakama ametwaa medali ya fedha kwa upande wa wanaume Wazee huku Bitwalihath Magotha wa Tume ya Utumishi wa Walimu naye kapata medali ya shaba kwa wazee hao.
Timu ya Wiazra ya Madini imetwaa medali ya dhahabu kupitia kwa Veneranda Charles kwa upande wa wazee; huku Hilda Masange alitwaa medali ya shaba katika mbio za mita 200 wanawake; nayo timu ya Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) imetwaa medali ya fedha kupitia kwa Mary Kapinga aliyerusha tufe kwa wanawake na pia medali ya shaba kwa upande wa mbio za wazee; nayo timu ya Wizara ya Sheria na Katiba imepata medali ya fedha kwa wazee wanawake kupitia kwa Geogina Mkwenda; na Zena Waziri wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) ametwaa medali ya shaba katika mchezo wa kurusha tufe kwa wanawake.
Michuano hiyo inatarajia kufikia kilele tarehe 2 Novemba, 2021 inaendelea kwenye viwanja mbalimbali mkoani hapa.