Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Bw. Dotto James akizungumza katika mkutano huo.Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF Bw. Francis Nanai akizungumza katika mkutano huo
Dr.Godwil Wanga – Mtendaji Mkuu wa Baraza la Biashara Taifa ( TNBC)
**********************
Tanzania ni moja kati ya nchi 191 zinazoshiriki katika Maonesho ya Dunia ya Expo 2020 Dubai katika nchi za Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) yaliyoanza rasmi tarehe 1 Oktoba, 2021 na yanayotarajiwa kuhitimishwa tarehe 31 Machi, 2022.
Akizungumza na waandishi wa habari hivi karibuni Katibu Mkuu Wizara wa Viwanda na Biashara Mhe.Dotto James amesema walitembelea Banda la Tanzania lililopo katika eneo la Mobility na kujionea maudhui mbalimbali yaliyowekwa kwenye banda hilo.
“Tulikagua namna tulivyojipanga kutangaza fursa mbalimbali zilizopo nchini kwenye sekta za Madini, Utalii, Nishati, Kilimo, Miundombinu na Miradi ya Kimkakati”. Amesema
Amesema walipata fursa ya kutembelea baadhi ya mabanda ya nchi mbalimbali ili kujifunza na kuona nchi nyingine zinazoshiriki ambazo zimeleta fursa toka maeneo mbalimbali ulimwenguni.
Aidha amesema walifanikiwa kutembelea nchi za Afrika zikiwemo Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Botswana, Ghana na Nigeria Pamoja na mabanda mengine yakiwemo banda la Uingereza, Marekani na Banda la Wanawake.
“Baada ya ziara tuliweza kujiridhisha umuhimu wa ushiriki wa Sekta za Umma, Sekta Binafsi na Vyombo vya Habari ili kupata matokeo bora na yenye tija kwa Taifa”. Ameeleza.