…………………………………………….
Na Silvia Mchuruza,Kagera
Watu tisa raia wa Tanzania wanaofanya shughuli za uvuvi wameokolewa nchini Uganda baada ya kutelekezwa katikati ya ziwa Victoria kwa zaidi ya siku 20.
Akizungumza kwa niaba ya wengine mmoja ya wavuvi hao aliyejitambulisha kwa jina la mzee katika mapokezi yao mbele ya mkuu wa mkoa wa kagera meja jenerali Charles Mbuge na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa, katika bandari ya kastamu wameeleza kuwa walikataliwa kupewa msaada na mmoja ya watumishi wa serikali katika idara ya uvuvi mkoani kagera ambapo aliwanyanganya baadhi ya vifaa walivyokuwa wakitumia ambavyo vingewafanya kufika nchi kavu .
Mkuu wa mkoa wa kagera amesema kuwa mtuhumiwa amabaye ni afisa uvuvi mkoa wa kagera yupo mikononi mwa taasisiya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU na uchunguzi unaendelea .
“janga hili mimi mwenyewew nilipata taarifa tarehe 12 kwamba kuna wavuvi wametelekezwa ziwani wamechukuliwa matenki ya mafuta na kuachwa watu ilipo fika tarehe 13 mwezi huu nikafanya utaratibu wa kumuita muhusika mkuu ambae ni afisa uvuvi wa mkoa na viongozi wa takukuru tukamuliza akakana kitu kama hicho lakini wavuvi wengine waliokuwa wamewaoko walisema ukweli ikanibidi niamru akamatwe kwa uchunguzi zaidi”.
Aidha Mkuu wa mkoa wa kagera amekemea vikali watumishi wa umma wenye tabia za kuwaonea watanzania na kusema kuwa sheria kali zitachulia dhidi yao.
Kwa uapande wake Kamanda wa TAKUKURU mkoa wa kagera JOHN JOSEPH amesema tayari uchunguzi wa suala hilo upo katika hatua za mwisho na ukikamilika taarifa itatolewa.
Hata hivyo serikali ya mkoa kupitia kwa mkuu wa mkoa na kamati ya ulinzi na usalama wameishukuru serikali ya Uganda kwa kuwasaidia watanzania hao ambapo wamesema kuwa nikutokana na ushirikiano mzuri ulipo baina ya nchi hizo mbili.