Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Prof.Abel Makubi,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akifungua mkutano ambao umezikutanisha Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) na mashirika yasiyokuwa ya Kiserikali (NG’Os) ambao ni wadau wa sekta ya afya kwa lengo la kushirikisha katika kukabiliana na ugonjwa wa UVIKO 19 uliofanyika leo Oktoba 26,2021 jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,(TAMISEMI) anaeshughulikia afya,Dk.Grace Magembe,akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari wakti wa Mkutano wa Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) na mashirika yasiyokuwa ya Kiserikali (NG’Os) ambao ni wadau wa sekta ya afya kwa lengo la kushirikisha katika kukabiliana na ugonjwa wa UVIKO 19 uliofanyika leo Oktoba 26,2021 jijini Dodoma.
……………………………………………
Alex Sonna
WIZARA ya Afya Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,imesema mpaka kufika Oktoba 23 mwaka huu jumla ya watu 20,000 wamechanja chanjo aina ya Sinopharm.
Pia imesema lengo ni kila siku watu 100,000 waweze kuchanja huku akieleza kuwa zaidi ya watu milioni moja wameweza kupata chanjo ya JJ ambayo ililetwa awali kutoka nchini Marekani.
Hayo yamesemwa leo Oktoba 25,2021 Jijini Dodoma na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo,Prof. Abel Makubi wakati akifungua mkutano ambao uzikutanisha Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) na mashirika yasiyokuwa ya Kiserikali (NG’Os) ambao ni wadau wa sekta ya afya kwa lengo la kushirikisha katika kukabiliana na ugonjwa wa UVIKO 19.
Prof.Makubi amesema wamekutana na wadau hao kufuatia hivi karibuni NGÓs kukutana na Rais Samia Suluhu Hassan na kusema kuwa wapo tayari kushirikiana na Serikali kutoa elimu na kuhamasisha watu kuchanja ili kukabiliana na ugonjwa wa UVIKO 19.
Prof.Makubi amesema mpaka kufika Oktoba 23 mwaka huu jumla ya watu 20,000 wamechanja chanjo aina ya Sinopharm ambapo imedai lengo ni kila siku watu 100,000 waweze kuchanja huku akitanabaisha kwamba zaidi ya watu milioni moja wameweza kupata chanjo ya JJ ambayo ililetwa awali kutoka nchini Marekani.
“Sasa wamechanja zaidi ya watu milioni moja kwenye zile zingine zimeisha na hizi za sasa hivi Sinopharm mpaka tarehe 23 tulikuwa tumechanja watu 20,000 sasa lengo letu kuchanja watu 100,000 kila siku tunataka kuongeza ushirikiano na wadau,”amesema Prof.Makubi
Amesema maeneo ambayo wanahitaji kushirkiana zaidi ni katika kuongeza suala la uchanjaji uweze kuwa juu zaidi ambapo sasa hivi wamefikia kiwango cha kuchanja wananchi 50,000 kwa siku kabla JJ haijaisha.
“Tumeona Serikali peke yetu hatuwezi hivyo ni lazima tuwashirikishe hawa wadau watatusaidia katika hili tunataka tuendelee kuongeza kuwapa elimu zaidi kuhusiana na kuchanja,”amesema.
Aidha,Prof.Makubi amesema Serikali kupitia Wizara yake itaendelea kuzisimamia NG’Os zote ambazo zimekuwa zikipata fedha kwa ajili ya kukabiliana na ugonjwa huo kwa kutaka ziende kwenye lengo lilokusudiwa.
“Tuna wajibu wa kufuatilia tumekuwa tukifanya hivyo ndio maana tumewaita,kama umepewa fedha mfadhili yoyote lazima tujue zinaenda kulenga kukabiliana na COVID 19 kinyume na hapo lazima tuwekeane mipaka kwamba hapo sio tuende njia hii tufuate muongozo wetu,”amesema.
Kwa upande wake,Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,(TAMISEMI) anaeshughulikia afya,Dk.Grace Magembe amesema wamefanikiwa katika chanjo awamu ya kwanza kwa kutoa elimu kwa makundi mbalimbali jinsi ya kukabiliana na ugonjwa huo.
”Tumejipanga kuendelea kutoa elimu kwa makundi mbalimbali ili jamii iendelee kupata chanjo huku akiwaomba Waandishi wa Habari kuendelea kupaza sauti juu ya umuhimu wa watu kuchanja”amesema Dk.Magembe
Naye Mwenyekiti wa Baraza la Mashirika Yasiyokuwa ya Kiserikali (NAcONGO) Lilian Badi amesema wao kama wadau wapo kwenye jamii hivyo wapo tayari kutoa elimu hivyo wanaomba wapewe nafasi ili waweze kuelimisha jamii kuhamaisha chanjo.