**************************
Na Mwamvua Mwinyi, Kibaha
MKUU wa mkoa wa Pwani , Abubakari Kunenge amemuagiza mkuu wa Wilaya ya Kibaha, kumfukuza kazi Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Twende Pamoja iliyopo kata ya Sofu,endapo atabainika kuchangisha fedha wanafunzi sh.300-1,000 kinyume na utaratibu .
Aidha ameeleza ,hiyo ni salamu kwa walimu wengine wa shule mkoani humo, zinazojihusisha kuchangisha michango holela mashuleni waache mchezo huo na wakibainika wasimamishwe kazi .
Akizungumzia suala hilo , Kunenge alisema amepokea simu Ikulu kuwa kuna malalamiko kutoka kwa wazazi ,wanaokerwa na michango inayowakandamiza na kuwapa wakati mgumu wanafunzi kupata elimu .
“Mkuu Wa Wilaya fuatilia hili ili tubaini ukweli wa suala hili ,na Mimi niweze kufahamisha mamlaka ya Juu ,Sheria inaruhusu kwa kufuata taratibu, kwakuwa Ni hiari inaruhusu lakini sio vinginevyo kwa manufaa ya mtu “
Kunenge aliagiza endapo akibainika Mwalimu Mkuu kuchangisha fedha kwa wanafunzi ,pia afisa elimu kata ,mtendaji kata nao waondolewe maana haiwezekani kuwepo na kero hizo na wao hawazishughulikii hadi zinafika Ikulu .
Akifafanua juu ya suala hilo ,Mwenyekiti wa halmashauri Kibaha Mjini Mussa Ndomba alisema ,taarifa zilizopo ipo michango ya sh .500 kila mwezi kwa ajili ya ulinzi na ujenzi kwa makubaliano ya wazazi .
Ndomba ambae pia Ni diwani wa Sofu alisema ishu ya kuchangisha sh.300-1,000 haijui labda ifuatiliwe kwa uongozi wa shule .
Kwa upande wa baadhi ya wazazi wa wanafunzi wa shule ya msingi Mkoani na Kambarage ,waliiomba serikali iwasaidie kuongea na walimu wapunguze kero kubwa ya michango kwa wanafunzi.
Walieleza ,wanafunzi wa Kambarage na Mkoani shule ya msingi wanachangisha sh .300 kwa Juma zima ,na sh .1,000 kila jumamosi kwa ajili ya mtihani pamoja na sh.5,000 kila wiki kwa ajili ya chakula .
Walisema fedha hiyo ni kwa mwanafunzi mmoja sh.7,500 kwa wiki Jambo ambalo kwa mwezi mzima linawaumiza ,kulingana na kipato chao.