Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) akivishwa medali na Mratibu wa Mashindano ya mbio za Rock City Marathon, Kasara Naftal katika mashindano ya mbio za Rock City Marathon zilizofanyika jijini Mwanza.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) na Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Ludovick Nduhiye (wa pili kutoka kulia) katika picha ya pamoja na wadau wa utalii katika mashindano ya mbio za Rock City Marathon zilizofanyika jijini Mwanza.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) (katikati) na Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Ludovick Nduhiye (wa pili kutoka kulia) wakifanya mazoezi ya viungo pamoja na washiriki wa mashindano ya mbio za Rock City Marathon zilizofanyika jijini Mwanza.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa mashindano ya mbio za Rock City Marathon zilizofanyika jijini Mwanza.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) akikabidhi zawadi kwa mshindi wa kwanza wa mbio za watoto za kilomita 2.5 katika mashindano ya mbio za Rock City Marathon zilizofanyika jijini Mwanza.
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Ludovick Nduhiye akimpa mkono wa pongezi mshindi wa pili wa mbio za kilomita 21 kwa upande wa wanawake Neema Msuhadi katika mashindano ya mbio za Rock City Marathon zilizofanyika kwenye jijini Mwanza.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) akimvisha medali ya dhahabu mshindi wa tatu wa mbio za kilomita 21 Shigande Giniki kwa upande wa wanaume kwenye mashindano ya mbio za Rock City Marathon zilizofanyika jijini Mwanza.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) akimpa tuzo Mwakilishi wa Benki ya KCB kwa kudhamini mashindano ya mbio za Rock City Marathon zilizofanyika jijini Mwanza.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) akizungumza na washiriki wa mashindano ya mbio za Rock City Marathon (hawapo pichani) katika viwanja vya Rock City Mall jijini Mwanza.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) akimkabidhi medali ya dhahabu mshindi wa kwanza wa mbio za kilomita 21 kwa upande wa wanawake Isgani Chameo kutoka Kenya baada ya mashindano ya mbio za Rock City Marathon jijini Mwanza. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Mhe. Hassan Masala na kushoto ni Rais wa Shirikisho la Riadha Tanzania, Silas Isangi,
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Ludovick Nduhiye akimvisha medali Mshindi wa Sita wa mbio za kilomita 21 kwa upande wa wanaume Lubega Robert kutoka Uganda baada ya mashindano ya mbio za Rock City Marathon jijini Mwanza.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) (katikati) na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Ludovick Nduhiye (wa pili kutoka kulia) katika picha ya pamoja na washindi wa mbio za kilomita 21 kwa upande wa wanaume baada ya mashindano ya mbio hizo jijini Mwanza. Wengine ni Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Mhe. Hassan Masala (wa tatu kutoka kulia) na Rais wa Shirikisho la Riadha Tanzania, Silas Isangi (wa pili kutoka kulia) na waandaaji wa mashindano hayo.
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Ludovick Nduhiye akimpa mkono wa pongezi Mshindi wa kwanza mbio za kilomita 21 kwa upande wa wanaume Alphonce Simbu kutoka Tanzania katika mashindano ya mbio za Rock City Marathon yaliyofanyika jijini Mwanza. Katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Mhe. Hassan Masala.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) akimvisha medali ya dhahabu mshindi wa kwanza wa mbio za kilomita 21 kwa upande wa wanaume Alphonce Simbu kutoka Tanzania katika mashindano ya mbio za Rock City Marathon yaliyofanyika kwenye viwanja vya Rock City Mall jijini Mwanza. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Mhe. Hassan Masala na kushoto ni Rais wa Shirikisho la Riadha Tanzania Silas Isangi.
Washiriki wa mashindano ya mbio za Rock City Marathon wakifanya mazoezi ya viungo kwenye viwanja vya Rock City Mall jijini Mwanza.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) akimsikiliza Mkuu wa Kanda ya Ziwa wa TTB, Gloria Munhambo (kulia) akitoa maelezo kuhusu juhudi za Serikali za kutangaza utalii alipotembelea banda la Wizara ya Maliasili na Utalii katika mashindano ya mbio za Rock City Marathon yaliyofanyika jijini Mwanza. Wa pili kutoka kulia ni Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Ludovick Nduhiye.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) akizungumza na watoto wenye ulemavu wa ngozi kutoka Kituo cha Mitindo Misungwi walioshiriki mbio za kilomita 5 za Rock City Marathon ambapo amewaahidi kulipia gharama za masomo kwa watakaofanya vizuri zaidi. Alisema hayo alipotembelea banda la Unilever kwenye viwanja vya Rock City Mall leo jijini Mwanza.
***********************************
Na Happiness Shayo- WMU
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) amewahimiza wadau wa michezo nchini kujenga tabia ya kushiriki michezo mbalimbali hasa mbio za marathon zinazoandaliwa kwa nyakati tofauti tofauti.
Alisema hayo jana baada ya kumalizika kwa Mashindano ya Mbio za Rock City Marathon yaliyofanyika jijini Mwanza.
“Kushiriki katika mashindano kama haya hakusaidii tu kupata zawadi mbalimbali bali ni njia mojawapo ya njia ya kuimarisha afya ” Mhe. Masanja amesema.
Ameongeza kuwa mashindano ya mbio za marathon yatasaidia kuhamasisha utalii, kukuza pato la mwananchi mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla kutokana na washiriki kuchangia katika kulipia huduma mbalimbali za malazi, vyakula nk.
Aidha, Mhe. Masanja amesema Wizara yake itaendelea kutoa ushirikiano kwa sekta binafsi inayoandaa mashindano kama hayo na amewaelekeza watendaji kushiriki kikamilifu katika maandalizi ya mashindano ya mbio za Marathon mara yanapojitokeza.
Katika mashindano hayo, Mhe. Mary Masanja alikabidhi zawadi na medali kwa washindi wakiongozwa na Mwanariadha wa Kimataifa kutoka nchini Tanzania Alphonce Simbu aliyeibuka mshindi wa kwanza kwenye mbio za kilomita 21 kwa upande wa wanaume, akifuatiwa na mshiriki kutoka Kenya Benard Musau.
Kwa upande wa wanawake katika mbio za kilomita 21 ziliongozwa na Isgani Chameo kutoka Kenya akifuatiwa na Neema Msuhadi na Tunu Andrew kutoka Tanzania.
Awali akimkaribisha mgeni rasmi, Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Mhe. Hassan Masala alisema kuwa mbio hizo ni nyenzo muhimu ya kuwaandaa wanariadha nchini kuwa katika nafasi ya kufanya vizuri katika michuano ya Kimataifa itakaoipa heshima nchi ya Tanzania.
Naye Mratibu wa Mashindano hayo Kasara Naftal alisema kuwa mbio hizo zimefanyika kwa mafanikio makubwa kutokana na ushirikiano alioupata kutoka kwa uongozi wa Mkoa wa Mwanza, Shirikisho la Riadha Taifa, Chama cha Riadha Mkoa wa Mwanza na wadhamini mbalimbali.