Home Mchanganyiko CHAMA CHA MAOFISA UHUSIANO WA UMMA TANZANIA (PRST) KUFANYA MKUTANO MKUU OKTOBA...

CHAMA CHA MAOFISA UHUSIANO WA UMMA TANZANIA (PRST) KUFANYA MKUTANO MKUU OKTOBA 28-29-2021

0

 Loth Makuzi rais wa Chama cha Maafisa Uhusino wa Umma Tanzania, PRST, akizungumza na waandishi wa habari kwenye hoteli ya Kebbys Mwenge jijini Dar es Salaam leo wakati alipotangaza Mkutano mkuu wa chama hicho unaotarajiwa kufanyika Oktoba 28 na 29, 2021 jijini Dar es Salaam, kushoto ni Katibu Mkuu wa chama hicho Bw. Ndege Makura

Katibu Mkuu wa chama hicho Bw. Ndege Makura akifafanua baadhi ya mambo katika mkutano huo kulia ni Loth Makuzi rais wa Chama cha Maafisa Uhusino wa Umma Tanzania, PRST.

Bi Mary Kafyome Mwenyekiti wa kamati ya Maandalizi ya mkutano huo akitoa maelezo kuhusu maandalizi ya mkutano huo kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa chama hicho Bw. Ndege Makura na katikati ni Loth Makuzi rais wa Chama cha Maafisa Uhusino wa Umma Tanzania, PRST.

…………………………………….

Bw. Loth Makuzi rais wa Chama cha Maafisa Uhusino wa Umma Tanzania, PRST amesema Mkutano wa mkuu wa chama hicho  utafanyika Oktoba 28 na 29, 2021 jijini Dar es Salaam ambapo washiriki mbalimbali kutoka Tanzania na nje ya Tanzania wanatarajiwa kuhudhuria.

Amesema Chama hicho kinatarajia kupokea ugeni kutoka nchini Kenya na Afrika Kusini ambapo Marais wa vyama vyao vya Maafisa Uhusino wa Umma katika nchi zao wanatarajiwa kushiriki katika mkutano huo na pia kutoa mada.

Makuzi ameyasema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye mkutano uliofanyika katika hoteli ya Kebbys jijini Dar es Salaam.

Akifafanua zaidi kuhusu mkutano huo Makuza amesema mgeni rasmi katika kitano huo wa siku mbili atakuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt Jim Yonazi.

Aidha ameongeza kuwa katika mkutano mkuu wa chama hicho cha maafisa uhusino kwa umma Tanzania, PRST, yatafafanuliwa mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kujadili changamoto na mafanikio ya chama hichi ambapo pia amewakaribisha wadau wote katika tasnia hiyo kwa ajili ya kuijadili na kuitafutia ufumbuzi pale ambapo kutawasilishwa changamoto.

Makuzi amesema mkutano huo utawahusu wadau wote wa Habari, mahusiano, mawasiliano, masoko na TEHAMA ambapo utakuwa na mjadala mpana kuangalia na kutatua changamoto zinazoikabili tasnia hiyo.

“Hatujawahi kufanya mkutano mkubwa kama huu, huu ni mkutano wa watu wote waandishi wa habari, watu wa mahusiano, mawasiliano, masoko na TEHAMA,tutakuwa na mijadal mipana kuijadili taaluma na kuitetea”, amesema Makuzi.

Amesema mkutano huo pia unalenga kujenga mahusiano mazuri kati ya waandishi wa habari na maafisa uhusiano kwa ajili ya kutatua changamoto mbalimbali katika taasisi na jamii kwa ujumla.

“Mkutano huu utajadili pia masuala mtambuka ya tasnia hii, kuangalia wapi tumeanguka na namna gani tufanye ili tuboreshe mazingira na kutoa kilichobora kwa jamii” alisema Makuzi.

Amesema katika mkutano huo pia  kutafanyika  kufanya uchaguzi wa viongozi wa chama hicho.