Mmoja wa askari wa uhifadhi ya Taifa Mikumia akitoa elimu kwa abiria kuhusu utapaji hovyo wa takataka na vyakula katika barabara inayopita katika hifadhi hiyo iliyopo Mikumi Mkoani Morogoro.
Mmoja wa askari wa Uhifadhi akisimamisha gari katika harakati za kuhakikisha wanadhibiti mwendokasi katika barabara inayopita katika hifadhi ya Taifa mikumi iliyopo mkoani Morogoro kuondokana na ajari hasa kugongwa kwa wanyama kwenye hifadhi hiyo.
Afisa Mhifadhi Mwandamizi,Kitengo cha Utalii, hifadhi ya Taifa ya Mikumi Bi.Happiness Kiyemi akizungumza na waandishi wa habari namna walivyojidhatiti kuhakikisha wanadhibiti ajari katika barabara iliyopita katika Hifadhi ya Taifa Mikumi.
************************
NA EMMANUEL MBATILO
Hifadhi ya Taifa Mikumi imeendelea kuwatia nguvuni wale wote ambao wanavunja sheria katika barabara ya hifadhi hiyo hasa kwa kupita kwa mwendokasi, kugonga wanyama na kutupa taka katika hifadhi hiyo.
Akizungumza na waandishi wa Habari katika Hifadhi hiyo iliyopo katika Mkoa wa Morogoro,, Afisa Mhifadhi Mwandamizi,Kitengo cha Utalii, hifadhi ya Taifa ya Mikumi Bi.Happiness Kiyemi amesema watumiaji wa barabara hiyo wamekuwa wakipita kwa mwendokasi na kusababisha ajali za binadamu na kwa wanyama ambao mara nyingi wanapita katika barabara hiyo.
“Hifadhi imeamua kuweka kikosi maalumu ambacho kinapita kwenye barabara na kusimamia magari yaweze kupita kwa mwendo ambao umewekwa lakini pia kutoa elimu kwa jamii ambayo hutumia barabara hii ili waweze kufuata utaratibu na kuepusha ajali”. Amesema
Amesema watumiaji wa barabara wamekuwa wakitupa taka katika hifadhi na kusababisha kubadili tabia kwa baadhi ya wanyama ambao mara nyingine wanakuwepo kwenye barabara hasa jamii ya nyani.
“Tunawahamasisha Watanzania na watu wote ambao wanatumia barabara hii, tumeweka mabqngo makubwa ambayo yanaainisha wazi vitendo ambavyo hawatakiwi kuvifanya na faini ambazo watatozwa mara atakapopatikana na makosa”.
Hifadhi ya Taifa Mikumi imepitiwa na barabara yenye urefu wa kilomita 50 ambayo inapita katikati ya hifadhi,wakati mwingine watumiaji wa barabara hii wanaendesha kwa mwendokasi kuliko kile kiwango ambacho kimeainishwa.