Kaimu postamasta mkuu wa shirika la Posta Tanzania, Macrice Mbodo (katikati)akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha .
Meneja Tehama wa shirika la Posta Tanzania ,Inspekta Reuben Komba akizungumza na vyombo vya habari jijini Arusha
(Happy Lazaro)
………………………………………………………………….
Happy Lazaro,Arusha
Arusha.Wananchi wametakiwa kupenda kutumia huduma za posta ya hapa kwetu nchini huku wakitakiwa kupenda vitu vya nyumbani kwani posta ya Sasa imebadilika hivyo ni vizuri wakaunga mkono kutumia huduma za posta hapa kwetu kwani kwa Sasa huduma zimeboreshwa kidigitali kupitia Tehama .
Hayo yamesemwa na Kaimu postamasta Mkuu shirika la posta Tanzania,Macrice Mbodo wakati akizungumza katika mkutano wa wadau wa Tehama unaofanyika mjini hapa.
“kwa nini tukatumie maposta ya nchi zingine wakati tuna Posta yetu hapa nyumbani na Posta yetu Sasa hivi imebadilika Sana tunatoa huduma zote kidigitali hivyo nawaomba Sana wananchi waunge mkono kwa kutumia huduma za nyumbani za Posta.”amesema Mbodo.
Ameongeza kuwa ,huduma zinazotolewa na Posta Sasa hivi ni za kidigitali na zinatoa mwanya wa kila mwananchi kupata huduma popote pale alipo kwani wao ndo wanamfuata mwananchi na hawasubiri mwananchi awafuate.
Amesema kuwa,Serikali ya awamu ya sita chini ya Mheshimiwa Samia suluhu Hassan imejipanga kutumia Tehema kurahisisha utoaji wa huduma za serikali kwa wananchi kupitia vituo vya huduma pamoja.
Ameongeza kuwa,Serikali imejipanga kupitia shirika la posta Tanzania kuhakikisha kuwa huduma mbalimbali za serikali zinatolewa chini ya dari Moja kupitia vituo vya huduma pamoja.
“madhumuni makuu ya kushiriki mkutano huu ni ili kuonyesha fursa ya kidigitali zinazotumiwa na posta kwani posta tuliyonayo .sasa hivi sio ile ya zamani ,hivyo wananchi wanapaswa kuitumia kwa shughuli mbalimbali.”amesema .
Ameongeza kuwa ,posta ya kidigitali inamwezesha mwananchi kuwa na duka mtandao ambapo inamwezesha mwananchi kuuza na kununua bidhaa zao kote duniani kupitia.duka hilo .
Amefafanua kuwa,posta ya sasa ipo kwa ajili ya kumfuata mwananchi kwani huduma za shirika zinapatikana kupitia simu za mkononi ambapo sasa hivi mwananchi anaweza kutumia namba ya simu kuwa anuani yake tofauti na zamani kwenda ofisi za posta.
Mbondo amesema kuwa, kwa Sasa hivi kuna mabadiliko makubwa ambayo yamepatikana kwani unaweza kuagiza bidhaa mbalimbali mikoa nyingine na unafikishiwa hapo hapo ulipo kila mmoja anapaswa kutambua kuwa hii ni posta ambayo imebadilika .
“Ukituma mzigo wako leo ukaweka namba ya simu utapokea meseji kuwa mzigo umepata hii ni zaidi ya Posta tofauti na kipindi kile hivyo naomba wananchi waitumie Posta vizuri.”amesema
Amefafanua kuwa, kama shirika wana fursa ya kukua zaidi kwa kuhakikisha wao ndo wasafirishaji wakuu hapa Tanzania lengo kuhakikisha usafirishaji ndani ya Tanzania unafanyika kupitia shirika la Posta.
Ameongeza kuwa, hapa Arusha Tanzania ni makao makuu ya Umoja wa posta Afrika na wamejipanga kuhakikisha posta ya Tanzania inakuwa mfano wa kuigwa kwa posta zote za Umoja wa Afrika ili waje kujifunza hapa.
Kwa upande wake Meneja Tehama wa shirika la Posta Tanzania ,Inspekta Reuben Komba amesema kuwa, Posta wameunganisha ofisi katika maeneo mbalimbali na zinatoa huduma kidigitali na zimeweza kupiga hatua kubwa kwa kufikia watu mbalimbali.
Komba amesema kuwa,kupitia huduma za duka mtandao zinawawezesha wafanyabiashara wadogo kuweza kujisajili na kuuza huduma zao sehemu yoyote mtandaoni na mwitikio ni mkubwa Sana.
“kwa kweli kupitia huduma ya kimtandao inasaidia kuunganisha wateja mbalimbali na kuweza kupata fursa ya kuuza na kununua bidhaa zao duniani kupitia duka mtandao “amesema Inspekta Komba.