Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Christian Blind Mission Tanzania (CBM) Bi Nesia Mahenge,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Oktoba 23,2021 wakati akitoa taarifa kuelekea Wiki ya Maonyesho ya AZAKI 2021 yanayotarajia kuanza kesho Oktoba 23 hadi 28,2021 jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mtendaji United Nations Association of Tanzania Reynald Maeda,akielezea Wiki ya Maonyesho ya AZAKI 2021 yanayotarajia kuanza kesho Oktoba 23 hadi 28,2021 jijini Dodoma.
Baadhi ya Waandishi wa habari wakifatilia taarifa ya Wiki ya Maonyesho ya AZAKI 2021 yanayotarajia kuanza kesho Oktoba 23 hadi 28,2021 jijini Dodoma.
………………………………………………….
Na.Alex Sonna,Dodoma
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Christian Blind Mission Tanzania (CBM) Bi Nesia Mahenge,amewataka wadau mbalimbali kuhudhuria maonyesho ya wiki ya Asasi za Kiraia (AZAKI) ambayo inatarajiwa kuanza kesho ili kujionea mchango wa AZAKI katika maendeleo ya Taifa.
Hayo ameyasema leo Oktoba 22,2021 wakati akizungumza na waandisi wa habari kuhusu wiki ya AZAKI ambayo inatarajia kuanza kesho Oktoba 23,2021 jijini Dodoma na kufunguliwa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai.
Mahenge amesema kuwa jumla ya Asasi zaidi ya 150 zitashiriki katika maonyesho hayo lengo likiwa ni kuonyesha mchango wake katika maendeleo ya Taifa.
Aidha amesema kuwa wiki hiyo inawaleta wadau mbalimbali wa Maendeleo nchini ikiwemo Wananchi,Serikali,AZAKI na sekta binafsi kwa pamoja ili kujadili na kusherehekea mchango wa AZAKI katika kuleta maendeleo nchini.
“Tunawaita wadau mbalimbali wa maendeleo kujumuika nasi kwa ajili ya kujifunza mambo mbalimbali ikiwemo ushauri wa kisheria,kufahamu kazi tunazofanya na kusherehekea kwa pamoja ,”amesema Mahenge
Amesema kuwa katika uzinduzi wa wiki ya AZAKI utahudhuriwa na wahisani wa maendeleo wakiwemo ubalozi wa Denmark Utakaowakilishwa na Sascha Mulla na Ubalozi wa Canada útawakikishwa na Ms.Helen Fytche.
Hata hivyo Mahenge amesema kuwa Asasi za kiraia zipo katika mchakato wa kufanya utafiti ni mchango kiasi gani wameutoa katika shughuli mbalimbali.
Amesema wamekuwa wakifanya shughuli mbalimbali za kuleta maendeleo kwa kushirkiana na Serikali na kwamba wamepewa miongozo mbalimbali na Serikali katika kuingia ubia wa kuleta maendeleo.
Amesema wanafanya shughuli mbalimbali katika sekta za elimu,kilimo,afya na masuala ya ajira, kuwajengea uwezo na maeneo mengine mengi.
“Na kuna tafiti tunataka kuufanya na tumeishaanza mchakato kuweza kuangalia kwa takwimu maalum ni michango ya kiasi gani kama ni rasilimali fedha,watu,vifaa mbalimbali ambavyo vinatolewa na huduma ambazo zinatolewa kuweza kujua tumefanya kwa kiasi gani.
“Nadhani huo utafiti utasaidia sana kutoa picha kamili kuweza kuonesha mchango ambao tunatoa katika Nchi ya Tanzania,”amesema
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa United Nations Association (UNA) Reynald Maeda amewataja Viongozi na wageni mbalimbali kutoka Serikalini watakaoshiriki katika uzinduzi huo ni pmaoja na Mkuu wa mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka,Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Jabir Shekimweri,Meya wa Jiji la Dodoma Prof.Davis Mwamfupe na mwakili kutoka Wizara ya Afya Vickness Mayao.
“Katika kusherehekea mafanikio ya sekta ya AZAKI na ubia Wetu baina ya wananchi maonyesho yatakayofanyika tarehe 23 hadi 24 Oktoba Katika ukumbi wa Jakaya Kikwete na kutakuwa na burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali kama Profesa Jay,Sheta,Barnabas,Gnako,na wasanii wa Dodoma,”amesema.
Amesema kuwa wiki ya AZAKI hukutanisha wadau wa maendeleo kujadili masuala ya masingi kuhusu ustawi wa sekta pamoja na maendeleo ya Taifa Kwa ujumla.