Wachezaji wa Timu ya Mpira wa Pete Wanawake Wizara ya Nishati wakifunga goli dhidi ya Sanaa katika Mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Wizara, Taasisi na Idara za Serikali (SHIMIWI) kwa hatua za Makundi, iliyochezwa katika uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro
Wachezaji wa Timu ya Mpira Wanaume, Wizara ya Nishati waliocheza katika mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Wizara, Taasisi na Idara za Serikali (SHIMIWI) kwa hatua za Makundi, iliyochezwa katika uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro,
………………………………………………………………
Ø Pete Nishati yafungwa kwa taabu Sana na Sanaa
Na Zuena Msuya, Morogoro
Timu ya Mpira wa Miguu ya Wizara ya Nishati imetoka sare ya kutokufungana na Timu ya Hazina, mpira uliochezwa kwa dakika 60 uwanjani katika mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Wizara, Taasisi na Idara za Serikali (SHIMIWI) kwa hatua za Makundi.
Mchezo huo umechezwa katika Uwanja wa Jamhuri Mkoani Morogoro Octoba 22, 2021 ikiwa ni mchezo wa kwanza kwa Timu ya Nishati na mchezo wa pili kwa Timu ya Hazina.
Kwa mujibu wa Nahodha wa timu ya Nishati, Fadhil Msigwa wachezaji wote wako salama kuendelea na mashindani hayo akieleza kuwa (kesho) Octoba 23, 2021, timu hiyo itacheza na Wakala wa Taifa wa Kuhifadhi Chakula(NFRA)
Kwa upande wa Mpira wa Pete, Timu ya Nishati imecheza Dakika 40 uwanjani dhidi ya Sanaa,Wizara ya Nishati imepata Magoli 21 dhidi ya mpinzani wake iliyepata magoli 23 katika mashindano hayo.
Nahodha wa Nishati, Fortunata Getele ameeleza kuwa timu yake imefanya vizuri sana lakini imeshindwa kutoka na ushindi kutokana kwakuwa na wachezaji majeruhi wengi.
Kesho Octoba 23, 2021 timu ya mpira wa pete itacheza na Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi.
Timu zote mbili ni Hazina na Sanaa wamecheza michezo miwili katika hatua za makundi.