Na
Mwandishi wetu, Arusha
BENKI
ya Mwalimu (Mwalimu Commercial Bank Plc) imeishukuru Serikali kupitia Benki Kuu
ya Tanzania (BoT) kwa hatua zake za kukabiliana na madhara yatokanayo na
ugonjwa wa Uviko-19 kwani zilisaidia sekta ya mabenki kuimarika na kuendelea
kutoa huduma kuhakikisha uchumi wa nchi
hautetereki.
Hayo
yalisemwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Mwalimu Commercial Bank Plc,
Bw.Francis C. Ramadhani wakati akitoa Taarifa kwa wajumbe wa Mkutano Mkuu wa
Tano wa Wanahisa wa benki hiyo jijini Arusha leo Ijumaa Oktoba 22, 2021.
Alisema
Takwimu za Benki Kuu za mwaka 2020 zinaonyesha uchumi wa Tanzania ulikua kwa
asilimia 4.7 na unategemewa kukua kwa asilimia 6 katika mwaka 2021 na hii
inaonyesha kuimarika kwa sekta mbalimbali za uchumi baada ya janga la UVIKO-19.
“Kwa
upande mwingine mfumuko wa bei umeendelea kuwa chini kwa wastani wa asilimia
3.5 hii pia inadhihirisha uwepo wa mazingira mazuri ya biashara.” Alifafanua
Bw.Ramadhani.
Akizungumzia
mafanikio ambayo benki ya Mwalimu
imepata katika mwaka 2020 Bw. Ramadhani alisema benki hiyo iliingia
makubaliano na taasisi tatu kubwa ambazo zinamiliki hisa katika benki yaani
Chama Cha Waalimu Tanzania (CWT), Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) na
Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) ambao kwa pamoja walitoa kiasi cha fedha za kitanzania
shilingi bilioni 25 ikiwa ni fedha za kuonhgeza amana za kufanya biashara.
“Kwakweli
fedha hizi ndugu wanahisa zimeiwezesha benki yetu kuongeza kasi ya utoaji
mikopo kwa wateja wetu. Alifafanua.” Alisema Mwenyekiti huyo wa Bodi.
Alisema katika kipindi cha
kuanzia Oktoba 2020 hadi Septemba 2021 ambapo jumla ya mikopo yenye thamani ya
shilingi za kitanzania bilioni 42 imeweza kutolewa.” Alisisitiza Bw. Ramadhani.
Kwa
upande wake Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa
Benki hiyo Bw. Richard Makungwa alisema benki itaendelea kuimarisha miundo
mbinu yake ili kuweka mazingira mazuri ya biashara ambapo hadi hivi sasa licha
ya kuwa na matawi mawili ya Dar es Salaam, Benki imefungua ofisi za kikanda
zakutoa huduma katima mikoa ya Morogoro, Mwanza na Mbeya na ofisi zingine mpya
Makao Makuu Dodoma na Arusha.
“Katika
kuboresha utoaji huduma kupitia TEHAMA, benki ilizindua MwananchiCard VISA
ambapo wateja wetu wanaweza kupata huduma kupitia ATM zaidi ya 2,000 nchi
nzima, kufanya malipo kwa njia ya mtandao (Online payment) na kupitia mashine
za malipo (POS-point of sales) zilizopo sehemu mbalimbali za huduma ikijumuisha
maduka makubwa na mahoteli.
“Vilevile
tunaboresha huduma ya MwalimuMobile (*150*31#) kwenye huduma hii na pia idadi ya MwalimuWakala imeongezeka kufikia 250.”
Alifafanua Bw. Makungwa.
Alisema
Benki itaendelea kuweka mazingira mazuri ya biashara ili walimu binafsi wanahisa kwa
ujumla kutumia huduma za Benki hiyo katika kukata bima za mali na maisha yao
kupitia Benki ya Mwalimu ambayo sasa ni wakala wa bima.
kwa
kufanya hivyo Wanahisa wote kwa ujumla wahamasike kutumia huduma za benki hiyo
katika kufanyia shughuli zao zote za kifedha kuiwezesha Benki kujiongezea
mapato ili kuharakisha muda wa kutoa gawio kwa wanahisa.
“Benki
pia inategemea mapato kutoka katika miamala mbalimbali kama kutoa pesa kwenye
akaunti, kutuma fedha kupitia simu vile vile kutuma pesa kwa mfumo wa kibenki
(TISS/EFT) na huduma za kibenki kupitia mawakala wetu.” Alisisitiz Afisa
Mkuu Mtendaji.
Aidha
Bw. Makungwa alisema mipango mingine endelevu ya benki inatazamiwa kukuza amana
kutoka katika ikolojia ya Elimu (education ecosystem), fedha za pensheni ya
kustaafu na fedha kutoka miradi ya elimu.
Naye
Katibu Mkuu wa Chama Cha Walimu Tanzania
(CWT) Bw. Deus Seif. Alisem, “Walimu naomba tutumie benki yetu, kuna sehemu tulizembea kidogo, wakati viongozi wetu wa Chama Cha Walimu
wanaanzisha hii benki waliamini kwamba benki itakuwa na nguvu kuliko mabenki
yote kwasababu waliamini walimu wasiopungua 217,000 walioko kwenye pay roll ya
Januari 2015 wote watafungua akaunti na kuitumia benki yao. “Napenda niwaarifu sisi makao makuu ya CWT miamala yetu inapitia Mwalimu Commercial Bank.” na sisi sote kwa umoja wetu kama tutaweza kuweka tu amana kwenye benki naamini itakuwa benki kubwa na yenye nguvu.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Wakurugenzi benki ya Walimu (Mwalimu Commercial Bank Plc),
Bw.Francis C. Ramadhani (Watano kushoto) na Bodi nzima ya Wakurugenzi ya benki
hiyo, wakisherehekea miaka Mitano tangu kuanzishwa kwa benki hiyo iliyokwenda
sambamba na Mkutano Mkuu wa Tano wa Wanahisa wa Mwalimu Commercial Bank Plc)
jijini Arusha leo Ijumaa Oktoba 22, 2021.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Mwalimu Commercial Bank Plc. Bw. Francis C. Ramadhani akizungumza katika mkutano huo wa tano wa wanahisa wa benki hiyo jijini Arusha Oktoba 22, 2021
Usajili na uhakiki wa wanahisa ukiendelea
Mkuu wa Kitengo cha Ukuzaji Biashara na Masoko wa Mwalimu Commercial Bank Plc. Leticia Ndongole (kulia) akimpatia makabrasha mmoja wa wajumbe wa Mkutano huo
Wanahisa wakisikiliza yaliyokuwa yakizungumzwa na viongozi wao
Wanahisa wakiwa kwenye mkutano