WAZIRI wa Afya,Mandeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,Dkt.Dorothy Gwajima,akizungumza kwenye hafla ya kilele cha maadhimisho ya siku ya afya ya Macho Duniani,pamoja na uzinduzi wa mwongozo wa kufundishia afya msingi na upokeaji wa taarifa ya Dunia kuhusu Uoni iliyofanyika leo Oktoba 21,2021 jijini Dodoma.
Mkurugenzi Msaidizi anayeshughulikia magonjwa yasiyoyakuambukiza kutoka Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt.James Kihologwe,akizungumza wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya afya ya Macho Duniani,yaliyofanyika leo Oktoba 21,2021 jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Shirika la Christian Blind Mission Tanzania (CBM) Bi Nesia Mahenge,akisoma risala fupi kwa niaba ya wadau wa huduma za afya ya macho nchni wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya afya ya Macho Duniani,yaliyofanyika leo Oktoba 21,2021 jijini Dodoma.
WAZIRI wa Afya,Mandeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,Dkt.Dorothy Gwajima,akipokea risala kutoka kwa Mkurugenzi wa Shirika la Christian Blind Mission Tanzania (CBM) Bi Nesia Mahenge,aliyesoma risala hiyo kwa niaba ya wadau wa huduma za afya ya macho nchni wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya afya ya Macho Duniani,yaliyofanyika leo Oktoba 21,2021 jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Shirika la Sightsavers,Godwin Kabalika,akisoma taarifa ya hali ya uoni Duniani wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya afya ya Macho Duniani,yaliyofanyika leo Oktoba 21,2021 jijini Dodoma.
Meneja Mpango wa Taifa wa Huduma za Macho kutoka Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt.Bernadetha Shilio,akizungumza wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya afya ya Macho Duniani,yaliyofanyika leo Oktoba 21,2021 jijini Dodoma.
Baadhi ya washiriki wakifatilia hotuba mbalimbali wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya afya ya Macho Duniani,yaliyofanyika leo Oktoba 21,2021 jijini Dodoma.
WAZIRI wa Afya,Mandeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,Dkt.Dorothy Gwajima,akizindua mwongozo wa kufundishia afya Msingi wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya afya ya Macho Duniani yaliyofanyika leo Oktoba 21,2021 jijini Dodoma.
WAZIRI wa Afya,Mandeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,Dkt.Dorothy Gwajima,akimkabidhi Meneja Mpango wa Taifa wa Huduma za Macho kutoka Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt.Bernadetha Shilio Mwongozo wa kufundishia afya Msingi wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya afya ya Macho Duniani yaliyofanyika leo Oktoba 21,2021 jijini Dodoma.
WAZIRI wa Afya,Mandeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,Dkt.Dorothy Gwajima,akimkabidhi Mkurugenzi wa Shirika la Brien Holden Vision Institute Bw.Eden Mashayo Mwongozo wa kufundishia afya Msingi wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya afya ya Macho Duniani yaliyofanyika leo Oktoba 21,2021 jijini Dodoma.
WAZIRI wa Afya,Mandeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,Dkt.Dorothy Gwajima,akimkabidhi Mkurugenzi wa Shirika la Christian Blind Mission Tanzania (CBM) Bi Nesia Mahenge, Mwongozo wa kufundishia afya Msingi wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya afya ya Macho Duniani yaliyofanyika leo Oktoba 21,2021 jijini Dodoma.
WAZIRI wa Afya,Mandeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,Dkt.Dorothy Gwajima,akimkabidhi Mwakilishi kutoka Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Kalidushi Charles Mwongozo wa kufundishia afya Msingi wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya afya ya Macho Duniani yaliyofanyika leo Oktoba 21,2021 jijini Dodoma.
WAZIRI wa Afya,Mandeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,Dkt.Dorothy Gwajima,akiwa katika picha ya pamoja na wadau mara baada ya kuzindua Mwongozo wa kufundishia afya msingi na upokeaji wa taarifa ya Dunia kuhusu Uoni wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya afya ya Macho Duniani yaliyofanyika leo Oktoba 21,2021 jijini Dodoma.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufunga kilele cha maadhimisho ya siku ya afya ya Macho Duniani,pamoja na uzinduzi wa mwongozo wa kufundishia afya msingi na upokeaji wa taarifa ya Dunia kuhusu Uoni iliyofanyika leo Oktoba 21,2021 jijini Dodoma.
Mwakilishi kutoka Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Kalidushi Charles,akitoa neno la shukrani kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima (hayupo pichani) wakati wa hafla ya kilele cha maadhimisho ya siku ya afya ya Macho Duniani,pamoja na uzinduzi wa mwongozo wa kufundishia afya msingi na upokeaji wa taarifa ya Dunia kuhusu Uoni iliyofanyika leo Oktoba 21,2021 jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Shirika la Brien Holden Vision Institute Bw.Eden Mashayo,akitoa neno la shukrani kwa niaba ya wadau kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dorothy G Gwajima,(hayupo pichani) wakati wa hafla ya kilele cha maadhimisho ya siku ya afya ya Macho Duniani,pamoja na uzinduzi wa mwongozo wa kufundishia afya msingi na upokeaji wa taarifa ya Dunia kuhusu Uoni iliyofanyika leo Oktoba 21,2021 jijini Dodoma.
WAZIRI wa Afya,Mandeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,Dkt.Dorothy Gwajima,akiwaaga washiriki mara baada ya kufunga kilele cha maadhimisho ya siku ya afya ya Macho Duniani,pamoja na uzinduzi wa mwongozo wa kufundishia afya msingi na upokeaji wa taarifa ya Dunia kuhusu Uoni iliyofanyika leo Oktoba 21,2021 jijini Dodoma.
………………………………………………………………………………………….
Na.Alex Sonna,Dodoma
WAZIRI wa Afya,Mandeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,Dkt.Dorothy Gwajima,ameeleza kuwa Tanzania ina watu zaidi ya milioni 2.4 wenye matatizo ya kutokuona huku asilimia 55 ya matatizo haya yanawaathiri wanawake.
Pia amesema visababishi vikubwa vya ulemavu wa kutokuona na upungufu wa kuona unaoweza kuzuilika kama vile upeo mdogo wa macho kuona na uoni hafifu vinavyorekebishika kwa miwani, mtoto wa jicho na shinikizo la jicho.
Kauli hiyo ameitoa leo Oktoba 21,2021,Jijini Dodoma wakati akizungumza kwenye kilele cha siku ya afya ya macho Duniani Waziri Gwajima amesema taarifa ya Shirika la Afya Duniani imeonyesha kuwa idadi kubwa ya watu wenye matatizo ya kutokuona asilimia 89 wanaishi katika nchi za uchumi wa kati na wa chini, Tanzania ikiwa miongoni mwa hizo.
Amesema pamoja na kuwa kiwango cha matatizo ya kuona yanayoepukika kwa ujumla kimepungua duniani, Tanzania inakadiriwa kuwa na watu 640,000 wasioona.
Aidha, watu wenye matatizo ya kutokuona kwa viwango cha kati na cha juu wanakadiriwa kuwa ni mara tatu ya watu wasioona ambao ni takriban watu milioni 1.8.
“Kwa ujumla Tanzania ina watu zaidi ya milioni 2.4 wenye matatizo ya kutokuona. Asilimia 55 ya matatizo haya yanawaathiri wanawake. Visababishi vikubwa vya ulemavu wa kutokuona na upungufu wa kuona unaoweza kuzuilika kama vile Upeo mdogo wa Macho kuona na uoni hafifu vinavyorekebishika kwa miwani, mtoto wa jicho na Shinikizo la jicho,”amesema.
Dkt.Gwajima amesema Takwimu za hapa Tanzania zinaonyesha watu milioni 1.2 tu kwa mwaka 2020 ndio walifikiwa na huduma za macho katika vituo vyetu vya kutolea huduma za afya ikilinganishwa na uhitaji wa takribani watu milioni 12,000,000.
“Na kati yao, asilimia 32% wanakuwa tayari wana upungufu wa kuona ikijumuisha ulemavu wa kutokuona. Upasuaji wa mtoto wa jicho kwa mwaka jana ulifanyika kwa wastani wa macho 200 tu kwa kila watu milioni 1, ikilinganishwa na macho 2,000 kwa kila watu milioni 1 kama inavyoshauriwa na Shirika la Afya Duniani,”amesema.
Amesema asilimia 38 tu ya watu wenye uhitaji wa miwani ya kurekebisha uoni ndiyo waliweza kupata miwani hiyo kutoka kwenye vituo vya tiba.
Aidha,Dkt. Gwajima amesema kwa mwaka huu, Wizara ilipanga kuelimisha jamii na viongozi pia kuhimiza watu kupima macho kupitia vituo mbalimbali.
“Maadhimisho ya siku ya kuona duniani ya mwaka huu yamekuwa tofauti sana kwa sababu ni mwaka mwingine tangu kuisha kwa utekelezaji wa Mkakati wa Kimataifa wa Dira ya mwaka 2020. Mkakati mpya umeandaliwa uliojikita kwenye Mapendekezo Taarifa ya Dunia ya Uoni iliyoandaliwa na ya Shirika la Afya Duniani,”amesema.
Waziri Gwajima amewaasa wananchi kujizuia kupata matatizo ya macho,kuepuka kuweka kwenye macho dawa ambazo hujaandikiwa na wataalamu kutoka kwenye Hospitali na vituo vya tiba au dawa zisizo rasmi.
Hata hivyo amesema kuwa kuhifadhi hali ya uoni ikiwa ni pamoja na kupanga angalao siku moja kwa mwaka kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa kina wa afya ya macho yako yaani kupimwa uwezo wa kuona, upeo wa macho kuona na pia kipimo cha ndani ya jicho.
“Ifanye Afya ya Macho kuwa kipaumbele, hakikisha kuwa swala la upimani wa macho ni sehemu ya huduma ya Afya inayotolewa kwenye eneo lako.Penda Macho yak ni Utume wa Maisha,”amesema
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika la Christian Blind Mission Tanzania (CBM) Bi Nesia Mahenge amesema tatizo la uoni hafifu na upofu linapelekea jamii kushindwa kushiriki kikamilifu katika shughuli mbali mbali za kiuchumi na maendeleo ya jamii na kuzidi kuongeza tatizo la umaskini Tanzania.
Pia,amesema Tanzania kuna changamoto ya upungufu wa rasilimali watu wa kutoa huduma ya afya ya machoa ambapo amedai Takwimu zinaonyesha kuwa zaidi ya asilimia 75 ya matatizo ya uoni hafifu na upofu Tanzania yanazuilika.
“Tunaiomba Serikali kwenye sera ya Afya na miongozo ya kuandaa bajeti na mahitaji ya Afya ya Macho iainishe vema kipengele cha Afya ya Macho na kukipa uzito unaostahili. Wadau tunaiomba Serikali ihakikishe kuna uwepo wa rasilimali watu kwenye ngazi zote za Taifa ili kurahisisha wadau kufika maeneo,”amesema.
Akisoma taarifa ya hali ya uoni duniani,Mkurugenzi wa Shirika la Sightsavers,Godwin Kabalika amesema uoni unabaki kuwa mlango mkubwa wa fahamu katika kila hatua ya maisha ya mwanadamu.
“Mtoto anayezaliwa anategemea uoni kutambua na kuweka mahusiano karibu na mama mtoto anaeanza kutembea pia anahitaji uoni ili aweze kujifunza na hatua zake hali kadhalika mtoto wa shule anapoenda shule na vijana wanahitaji uoni ili kujitegemea hata watu wazima wanahitaji uoni,”amesema.
Amesema matatizo ya macho bado yapo na kwa kiasi kikubwa kila mmoja hupata tatizo la macho amedai kwa miaka ijayo idadi ya tatizo litaendelea kukua kutokana na uongezeko la watu mabadiliko ya tabia Nchi.
Amesema Mifumo ya afya inakabiliwa na changamoto ya kufikia uhitaji wa sasa na unaotarajiwa duniani
Amesema ili kukabiliana na ongezeko hilo kunahitajika kuongezeka kasi za afua kukabiliana na changamoto hizo
“Mapendekezo ya taarifa hiyo ni pamoja na afya macho iwe sehemu afya kwa wote,kujumuisha afya ya macho kwenye huduma za afya kwa kumlenga mhitaji ,kuhamasisha tafiti ya utekelezaji wa viwango vya juu na kuongeza uelewa,kufanya ufuatiliati na tathimini ya maendeleo,kuongeza uelewa na kushirikishwa watu na jamii,”amesema.