Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Tanzania (DCEA) Gerlad Kusaya akiwa na ujumbe wake wakishiriki katika mkutano wa 64 wa majadiliano ya majadiliano ya Kamisheni ya Kimataifa ya Kudhibiti Dawa za Kulevya Duniani ulioanza Oktoba 18 – 21 Mwaka huu Jijini Vienna Nchini Austria.
Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Tanzania (DCEA) Gerlad Kusaya (Wa kwanza Kushoto), Mwenyekiti wa Mkutano wa UNCND Balozi Dominika Chrois (wa katikati) na Katibu Mtendaji wa UNCND Bibi Jo Bedeyne- Amann (wa kwanza Kulia) wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa mkutano huo.
*************************
Na Mwandishi Wetu, Vienna Nchini Austria
Oktoba 21, 202
Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Gerald Kusaya akiambatana na maafisa wengine ameiwakilisha Tanzania katika Mkutano wa 64 wa Majadiliano ya Kamisheni ya Kimataifa ya Kudhibiti Dawa za Kulevya Duniani ulioanza Oktoba 18 – 21 Mwaka huu Jijini Vienna Nchini Austria.
Mkutano huo wenye lengo la kubadilishana uzoefu, kuimarisha ushirikiano wa Kikanda na Kimataifa pamoja na kutatua changamoto zinazojitokeza katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya.
Pia, Mkutano huo ulijadili namna bora ya kupambana na tatizo la dawa za kulevya na makosa mengine ya uhalifu wa kupangwa ikiwepo ya Ugaidi, Utakatishaji fedha, Usafirishaji haramu wa Binadamu na Uhalifu wa kimtandao na kuimarisha ushirikiano wa Kikanda na Kimataifa pamoja nakutatua changamoto zinazojitokeza katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya Duniani.